Naomba kujuzwa idadi ya maswali inayoruhusiwa kuuliza kwenye baraza la kata

DENAMWE

JF-Expert Member
Dec 29, 2019
806
805
Naomba kufahami haya mtu anapokuwa kwenye Baraza la ardhi la Kata.

i] Kuna idadi maalum ya maswali ya kumuuliza shahidi anapomaliza kutoka ushahidi?

ii] Iwapo mdai/mdaiwa/shahidi anapotoa maelezo, naruhusiwa kuchukua kumbukumbu kwa kuandika ili niweze kuuliza swali/maswali?
 
i. Hakuna idadi kamili iliyotajwa na sheria, ila jitahidi kuuliza maswali ya msingi katika kuijenga kesi yako.
ii. Unaruhusiwa, lakini hakikisha huondoi utulivu wa baraza.
 
i. Hakuna idadi kamili iliyotajwa na sheria, ila jitahidi kuuliza maswali ya msingi katika kuijenga kesi yako.
ii. Unaruhusiwa, lakini hakikisha huondoi utulivu wa baraza.
Asante sana.
 
NB: Wingi au uchache wa maswali haukupi ushindi mahakamani.

MUHIMU: Uliza maswali yatakayokujengea umiliki wa ardhi husika yaani maswali yatakayokuwa na faida kwako hasa juu ya kiini cha mgogoro na umiliki.
Mf. Ulivyopata umiliki, Ukubwa wa eneo, umeoa au kuolewa na mwaka gani, eneo lilipo na vitu kama ivyo.

Usilipe Baraza kazi kuanza kufikiria na wewe umelenga nini, jambo muhimu ni uliza maswali wazi kabisa usilete kona kona hazina maana kabisa.

Ungefafanua kidogo ishu yako ungepata mengi zaidi, ila hayo zingatia.

MWISHO: Fahamu kuwa Baraza la Kata halina mjumbe yoyote ambaye ni mtaalamu wa sheria kwaio kuwa wazi na jitahidi ueleweke sana sana sana.
 
Back
Top Bottom