Naomba kujuzwa haya kuhusu kuanzisha NGO

ntita

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
512
250
WanaJF

Kati ya ndoto zangu kubwa katika maisha ni kuanzisha NGO yenye kujihusisha na mambo ya elimu.

Ukiachana na taratibu za kisheria za usajili{ambazo nimeshazisoma} je ni mambo gani mengine natakiwa kuzingatia?

Ni kwa namna gani NGO zinapata fedha kwa namna gani? je, kuna ruzuku NGO zinapata kutoka serikalini? ni kwa namna gani ninaweza pata internship ktk NGO ili kupata uzoefu wa uendeshaji wa NGO?
 

probaraka

Member
Jul 8, 2017
15
45
wanajf
kati ya ndoto zangu kubwa katika maisha ni kuanzisha NGO yenye kujihusisha na mambo ya elimu.

ukiachana na taratibu za kisheria za usajili{ambazo nimeshazisoma} je ni mambo gani mengine natakiwa kuzingatia?
ni kwa namna gani NGO zinapata fedha kwa namna gani? je, kuna ruzuku NGO zinapata kutoka serikalini? ni kwa namna gani ninaweza pata internship ktk NGO ili kupata uzoefu wa uendeshaji wa NGO?
Sina uelewa kiivo ila kuna NGO's kama CHAWATA nathani hupata ufathili kutoka ktk mashirika mbalimbali na makampuni makubwa ila ruzuku serikali sijajua ndg yang

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Hongera Sana kwanza kwa akili hiyo ya kuwaza kujitolea katika ofisi /NGO na kuanzisha NGO,

Back to business,
1. NGO hazina /hazipewi hela kutoka serikalini mfano, ruzuku hiyo hakuna isipokuwa pana miradi inayotekelezwa na serikali kupitia wahisani ndani ya serikali hapo ndipo unaweza pata hela kutoka serikalini ila ni kutoka kwa wahisani/wafadhili.

2. Kuhusu internship, unahitaji kufika katika NGO yoyote unayopenda /hitaji kufanya internship na kujieleza Kwa wahusika kuwa unahitaji kujitolea (kumbuka, NGO hawatoi mshahara Kwa interns ila pana viposho vya hapa na pale kwa hiyo usitegemee kutoka na maburungutu kwenye NGO Kama ya IPTL na Escrow. Hapana , tafuta iliyo karibu nawe au jiandae kifedha ).

Ama NGO zingine wanatangaza nafasi za watu /wanafunzi kujitolea au kufanya internship hivyo jenga utaratibu wa kusoma tovuti /websites mbalimbali za NGO ambazo ungependa kujitolea. Mfano, UN agencies huwa wanatangaza mara nyingi miezi ya Feb, March na.April Kwa ajili ya kuanza kujitolea mwezi wa June, July, August hadi September na tena wanatangaza, October Kwa ajili ya watakaojitolea mwezi wa Feb, March April etc.

Kumbuka, kwa Tanzania, NGO /ofisi nyingi wanatangaza nafasi hizo mapema ili wanafunzi /wanaohitaji kujitolea waanze mwezi wa June, July na August Kwa sababu, NGO wanafuata mihula ya shule :- vyuo na taasisi mbalimbali za elimu za hapo Tanzania wanapokuwa wamefunga rikizo ndefu .

3. NGO wanayopata fedha - NGO wanaandika madodoso/ proposal kuomba hela kutoka kwa wafadhili mbalimbali duniani na hii ipo Kwa namna kuu mbili :-
(a) . Wafadhili mbalimbali hutangaza kufadhili projects maeneo mbalimbali duniani hasa Africa, kwa hiyo NGO huandika dodoso kujibu lile tangazo la wafadhili kuwa wao wapo tayari kufanya kazi hiyo na wafadhili huja kutathimini uwezo wa NGO hasa raslimali watu, miradi ambayo hiyo NGO yako imewahi kutekeleza kutokana na hela za wafadhili wengine hapo awali , na ofisi yako (physical location of the office ) na wakiona unauwezo huo basi wanakupa hiyo hela.

(b) Ni wewe Kama NGO kuandika dodoso/proposal na kutuma katika ofisi mbalimbali mfano, hapo nchini Unaangalia vipaumbele vya balozi zilizopo hapo Tanzania na nchi marafiki zetu, kisha unaandika dodoso kulingana na vipaumbele vya ubalozi huo kisha unatuma kuomba ufadhili wa kifedha ili utekeleze mojawapo au vipaumbele vyote vya ubalozi husika,mfano mzuri hapo Tanzania ni USA Embassy.

Ila kumbuka, fedha hizo wanatoa Kwa awamu, na wanakuwa a watchdog - monitoring and evaluation after each stage of the implementation of the project proposed/initiated.

Naamini nimekujibu, japo mambo ni mengi katika NGO na wengine wataongezea.

Nitarudi tena toleo lijalo.
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Still finding out on how to start mining companies

Private geologist

1.Register your company whether it's small, medium or international.

2. Inject the finances or outsource the external funds.
Remember, Former Minister of Energy and Minerals, Prof Muhongo, once said, "watanzania hawana fedha za kuwekeza kwenye mafuta na gesi ' bali wanafedha za kuwekeza kwenye juice na maji...... " and the like.
So, get enough capital then, the road is very clear and smooth especially in this era of His Exec. President Dr . Magufuli

Congrats for having a great dream it's your effort to realize it into a reality.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom