Naomba kujuzwa hali ya maisha Korogwe Vijijini

Mark mod

JF-Expert Member
Mar 10, 2019
291
550
Habari wakuu!

Mimi ni mtumishi wa umma idara ya Elimu sekondari nipo Simiyu Wilaya ya itilima nataka kubadilisha mazingira yaani nihame huku! Sasa nimepata mtu wa kubadilishana naye!

Yeye yuko Korogwe vijijin! lengo la kuja kwenu ni kwamba naomba mnifahamishe hali ya maisha ya huko nilinganishe na huku.

Najua humu kuna wenyeji wengi tu.

Natanguliza shukrani.
 
No hatubagui mkuu mwenzangu ye ndo kaniomba kubadilishana na mimi ye anataka kuja huku simiyu.Sasa nami si mwenyeji korogwe ndo maana nauliza mkuu so kwa nia mbaya.
Tanzania ni yetu sote, tusiwe wabaguzi wa maeneo ya kazi.
 
Korogwe kilimo kipo vizuri sana lakini pia ni mjini kiasi
Wewe unaijua Korogwe Mjini lakini Korogwe inasambaa mpaka kwenye mpaka na Kenya. KWA SEMANGUBE ndani ndani huko! Mm naamini maisha popote tu. Niliwahi kwenda Nanyumbu/Mangaka Chaka huko watu wavivuu nikawakutanisha wachaga wananunua mashamba kwa bei chee. eg. Heka 1 = Tsh. 50,000/= jamaa wanalima mikorosho Kama wanakufa kesho. Wewe umeng'ang'ania kuhamia Korogwe as if hiyo Korogwe imekua DUBAI
 
Shule ninayohamia inaitwa BUNA SEKONDARI kuna mwenyeji yeyote mwenye kuifahamu labda
Nakupa dondoo
Buna Sekondari iko kando kando ya barabara ya lami (Korogwe-Arusha).
Ni kabla ya kufika Mombo, nadhani pale ni eneo la Kwasunga kabla ya Makuyuni, baada ya Makuyuni ndo unafika Mombo.

Kwa ujumla sio mbali na Korogwe mjini, maisha ni ya kawaida tu, watu wa Korogwe ni wakarimu, vyakula sio bei ghali, fursa unaweza kulima, kufanya biashara eg. Samaki n.k

Nakutakia kila la heri ndugu yangu

Ni kutokana na uzoefu wangu, niliwahi kukaa Korogwe (M) pale town kabisa so huko napajua jua kidogo.
 
[SUB]Kama hiyo shule iko ule ukanda wa Mombo, utapata unafuu maana ni bondeni na miundombinu yake mfano barabara, huduma za kiafya, nk. ni rafiki. Ila kama iko milimani tutanakoishi sisi, hakika utatendea haki.[/SUB]

[SUB] Karibu sana Korogwe vijijini. Wasambaa hatuna mambo mengi, ingawa huwa hatupendi kuzinguliwa na wahamiaji a.k.a Wanyika. [/SUB]
 
Back
Top Bottom