Naomba kujuzwa haki za Mtumishi wa Serikali aliyefukuzwa Kazi

Gushleviv

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
3,432
5,140
Wasalaam, naomba kujuzwa haki za mtumishi wa Serikali ambaye amefukuzwa kazi huku akiwa na Malimbikizo ya Mshahara ambayo hakulipwa. Je utaratibu ni upi?

Na kipindi aliposimamishwa alikuwa akilipwa Nusu ya Mshahara je baada yabkufukuzwa analipwa kiasi cha nusu alichokuwa akikatwa wakati wa uchunguzi wa Shauri lake?
 
Tafadhali eleza kwa kina, kosa lilisababisha kufukuzwa kazi, taratibu zilizochukuliwa dhidi yako mpaka kufikia maamuzi ya kufukuzwa kazi n.k
 
Umeuliza mambo mawili issue ya Kwanza kama anamalimbikizo na hakupewa anatakiwa aende kwa mawakili wamua dikie demand letter ikidai apewe hiyo mishahara ambayo hakupewa within muda fulani wakikaidi mnawapeleka CMA unajaza fomu pale kw ajiri ya shauri
 
Issue ya pili kw habari ya nusu mshahara ndio watakapo kuwa wankokotoa watakokoa mpak pale alipokuw analipw nusu mshahara
 
Wasalaam, naomba kujuzwa haki za mtumishi wa Serikali ambaye amefukuzwa kazi huku akiwa na Malimbikizo ya Mshahara ambayo hakulipwa. Je utaratibu ni upi?

Na kipindi aliposimamishwa alikuwa akilipwa Nusu ya Mshahara je baada yabkufukuzwa analipwa kiasi cha nusu alichokuwa akikatwa wakati wa uchunguzi wa Shauri lake?
1. Malimbikizo ya mshahara, yataendelea kubaki kama deni. Kwa kuwa haya hulipwa kama mshahara na kwa kuwa baada ya kufukuzwa kazi mshahara umekoma, malimbikizo hayo yatakumbushwa kwa barua kwenda kwa mwajiri kama madai na yatapaswa kulipwa kama madai mengine yalivyo serikalini (kama fedha za kujikimu nk)

2. Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi za Umma za mwaka 2003, Nusu ya mshahara iliyokuwa inabaki wakati wa kusimamishwa kazi hulipwa kwa mtumishi endapo tu makosa aliyotuhumiwa nayo yatashindwa kuthibitishwa. Anapokutwa na hatia na kufukuzwa kazi hastahili kulipwa ile nusu ya mshahara ambayo hakulipwa.

3. Haki nyingine ni kulipwa fedha za kusafirisha mizigo au kupewa usafiri utaosafirisha mizigo yake kwenda nyumbani kwake (domicile). Mizigo isiyozidi tani 3, kulipwa nauli ya kumsafirisha yeye, mwenza wake na watoto wake wasiozidi 4 (kama wapo) kwenda nyumbani kwao mtumishi
 
Maelezo muafaka.Nina swali la nyongeza:
Kuhusu mchakato wa fedha za mfuko wa hifadhi ya jamii anapataje?I nakokotolewaje?
 
Ikiwa aliajiriwa kama mtumishi asiye afisa (digrii) anapewa michango yake yote, ila kama alikuwa ni afisa (digrii) anapata 1/3 kama sikosei ya michango yake na ikipita miaka 3 hajapata ajira atafikiriwa kupewa michango iliyobaki (yote au kiasi tu)
 
Back
Top Bottom