Naomba kujuzwa haki ya Mtuhumiwa wakati wa kukamatwa

Mtaunaki

Member
Jan 2, 2021
14
5
Habarini,

Napenda kujua ni kwa namna gani mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kisheria? Na mkamataji ana wajibu wa kufanya nini kwanza kwa mtuhumiwa kabla ya kumkamata?
 
Sheria zipo ila hawa Polisi wetu ukiwaletea Mambo ya sheria kwenye kukukamata utachezea virungu vya ugoko hadi ujikojolee..
 
Mkuu hizo haki zipo kwenye makaratasi tu na kwa wenye pesa...kama mwenzangu na mimi achana nazo maana Polisi watakuua hao.
 
Habarini,

Napenda kujua ni kwa namna gani mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kisheria? Na mkamataji ana wajibu wa kufanya nini kwanza kwa mtuhumiwa kabla ya kumkamata?
Polisi wa kitanzania hawajui hizo sheria wengi wanatumia mabavu na huwezi kuwashtaki, wanavyokuja kukukamata wanatakiwa wawe na arrest warrant lakini wengi hawajui hilo
 
Kwa hawa Polisi wetu, sidhani kama wanakuja mtuhumiwa ana haki zake.
Haki zipo kwenye makabrasha tu. Imenenwa kuwa haki ahera sheria duniani
IMG_20210103_203526_404.jpg
 
Habarini,

Napenda kujua ni kwa namna gani mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kisheria? Na mkamataji ana wajibu wa kufanya nini kwanza kwa mtuhumiwa kabla ya kumkamata?

Hizi ni baadhi ya haki za msingi za mtuhumiwa anapokamatwa na Polisi.

Mtuhumiwa ana haki ya kusomewa haki zake.

Mtuhumiwa ana haki ya kikatiba ya kutambuliwa kwamba hana hatia mpaka atakapopatikana na hatia na mahakama, na kuarifiwa hivyo anapokamatwa.

Mtuhumiwa ana haki ya kuwa na mwanasheria wake.

Mtuhumiwa ana haki ya kukataa kujibu swali lolote analoulizwa kabla ya kuwa na mwanasheria wake.

Mtuhumiwa ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi masaa 48 baada ya kukamatwa.
 
Habarini,

Napenda kujua ni kwa namna gani mtuhumiwa anatakiwa kukamatwa kisheria? Na mkamataji ana wajibu wa kufanya nini kwanza kwa mtuhumiwa kabla ya kumkamata?

Kwa tanzania
Introduction
Tanganyika jeki,pingu kwanza ukibisha mabao
Alafu
“Twende utajua huko huko”
Ukileta ubishi maulizo sana ndio kesi inazidi kuwa ngumu kwako.
Conclusion
Duniani hakuna haki kwa mwanadamu hipo mbinguni bali kubali wanavo taka ili ukatokee mahakamani kama itafika
 
mtuhumiwa yupo na haki nyingi...
>>lazima aonyeshwe hati ya kukamatiwa
>>kuambiwa sababu zinazopelekea yeye kukamatwa na ni haki yake pia kukubali au kukataa kufungwa pingu

ila ikumbukwe kuwa haki za mtuhumiwa huwa zinapungua kutokana na uzito wa kosa
 
Back
Top Bottom