Naomba kujuzwa hadhi ya makazi ya Mbezi Makabe

nguvusimba

JF-Expert Member
Feb 17, 2020
1,116
1,824
Wadau na wakazi wa Mbezi Makabe naomba kufahamu hadhi ya makazi ya maeneo haya, je kumepimwa? Kuna lami? Kuna biashara ya nyumba za kupanda na guest au lodge? PIA NAOMBA KUFAHAMU BEI YA VIWANJA 20/20.

Tafadhali nitashukuru sana kufahamu hayo kwa uchache.
 
Mtoa mada kama unalengo lako na hilo eneo we nenda tu kwa mifumo yetu ya bongo hakuna sehemu serikali wamepeleka maji,barbara,shule,hospitali nk hali ya kuwa hakuna nyumba za watu mfano mzuri ni maeneo ya mbagala na viunga vyake muda huo hadi
Nyani walikuwepo na kila mtu alikuwa anakudharau lakin watu walikomaa kujenga mdogomdogo mpaka sasa serikali wanapeleka huduma na kupata hadhi fulani.
 
Shida kubwa ya Mbezi ni aina ya maeneo yalivyo maana 90% kuna milima na mabonde. Bora upate eneo lililo kwenye mwinuko ukipata eneo lililo kwenye bonde aiseee na nyumba zinavozidi kujengwa lazima itakuja kuondoka na maji. Kibaya zaidi watu wanapozidi kukata majaji hata udongo wake mbovu sana unapasuka pasuka. .

Ujenzi maeneo ya mbezi ni wa gharama na aina yake ndo maana unaona nyumba nyingi zinawekwa matoleo ya maji kuepusha zisibomoke mapema. Pamoja na hayo yote kwa mtazamo wangu Mbezi Makabe ni kama nyuma ya mgongo. Watu wengi hata wakiwa wanaoga huwa wanajisahau kuosha mgongo. Kuna shida ya maji bado sana, usafiri wa shida halafu kuna zile gari zilizopigwa marufuku mjini zinaitwa vipanya, wakati wa mvua hakuridhishi sana, na neno makabe lilitokana na mkabe kulikuwa na wezi balaa. .

Shida kubwa ya Mbezi hakuna vituo vya kutosha vya polisi hivyo majambazi walikuwa wanapita nyumba mpaka nyumba yani wanakaba mtaa mzima na hakuna polisi. .
 
changamoto kubwa ni kipato lakini hakuna nyumba nzuri kama zinazojengwa kwenye miinuko yani wenzetu hizi ndio mahali wanapenda kabisa

EFH S, Doren _ Vorarlberger Holzbaukunst.jpg
In praise of the modern.jpg
K-pop_interracial& Imagines(AMBW).jpg
Moderne schicke Treppen Beleuchtung! - Archzine_net.jpg
the patricinha and the popular 💫 •Babictor.jpg
 
Mimi nimejenga Mbezi Makabe tangu mwk 2014 japo sijahamia bado. Kimsingi kunazidi kukua. Ninavyopaona kutakuja kuwa pazuri sana. Sasahivi wapo kwenye mchakato wa kuwekwa lami.

Kumbuka Goba kulivyokuwa kunaogopesha kipindi hicho kabla ya Lami, kumbuka MalambaMawili kulivyodharaulika kabla ya Lami.

Pia miinuko na mabonde ya Makabe sio mikubwa na haijakaa kihasara kama ya Goba, Kumara, Bonyokwa au King'ongo. Binafsi naona Makabe kumekaa vizuri sana. Na siku si nyingi kutapendeza sana hasa baada ya miundo mbinu ya Barbara/Lami na Maji kukaa sawa.

Kikubwa tu unapotaka kujenga unatakiwa ujipange hasa Msingi wa nyumba.

Karibu sana Mdau achana na Comments za waliopanga makabe.
 
Hizi zote zipo Mbezi Makabe, ndiyo majambazi walikuwa wanakaba mtaa mzima.

Everyday is Saturday.............................. 😎
hapana mkuu nilimjibu jamaa anasema tatizo la mbezi kuna milimandio nikamwambia hakuna nyumba nzuri kama zinazojengwa kwenye milima, anyway ukitoka ubongo kuelekea chalinze hakuna eneo la tambalale moja kwa moja eneo kubwa ni mabonde na miinuko
 
Ujenzi wa kwenye miinuko ni wa gharama sana, na ule udongo wa mfinyanzi, kiukweli hii nchi watu ni matajiri...ukijenga nyumba 1 ni sawa na Njombe ukijenga nyumba 3. Tunakomaa tu na jiji!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom