Naomba kujuzwa gharama za kupima Afya ya uzazi

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,398
2,000
Unachotaka kupima haswa ni nini?

Follicle Stimulating Hormone (FSH), Prolactin bei yake huwa ni 35,000 kila kimoja.

Sperm count kwa mwanaume huwa ni 15,000.

Gharama inaweza kuwa juu au chini kutegemeana na mahali unapofanyia.
 

mwanamatumbi

Member
May 14, 2020
29
100
Andaa Kama laki 3 kwa Private hospital.
Maana Kuna vipimo itatakiwa mfanyiwe wote wawili.
Endapo vipimo vya awali vikitoa majibu basi gharama zitapungua.
Ila endapo italazimu bibie apigwe X-ray gharama zitakuwa si chini ya laki3.
 

Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
2,435
2,000
Pole sana! Shida zetu zinafanana. Mimi mwezi August natimiza 2yrs.

Huna bima ya afya? Mimi nilitumia bima kufanya vipimo vya sperm , sikufuatilia gharama zake.

Wife hana bima, zilinitoka zaidi ya 300k. Wanawake wana vipimo vingi na vina gharama kubwa. Kipimo kimoja kiligharimu 125k!

Lakini pia bei zinategemea ubora wa hospitali na huduma zake, epuka kabisa hospitali ndogo kama za wilaya hizo, nenda hospitali za rufaa au zile za private zenye standards. Mimi nilifanyia hospitali ya wahindi inaitwa Shree Hindu Mandal ipo jirani na Bugando.

Wahi vipimo ili mjue tatizo na namna ya utatuzi kwa maana kuna matatizo kadri unavyochelewa yanazidi kukomaa na kuwa sugu. Mungu awape wepesi. Hii ishu ni ya kusikia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Luvh

Member
May 8, 2021
28
45
Habari Wakuu nina mwaka wa pili sasa tokea nimeoa hamna kitu naomba kujua gharama za kupima afya ya uzazi kwa Me na Ke.

Ahsanteni
Kama unatumia bima nenda hospital na bima zenu Ila Kama hutumii bima andae Ela kwa wawili Kama lak 3 hivi sababu wewe utapimwa sperm analysis ni 15000
Mkeo ajiandae kwa vipimo Kama ultra sound kuangalia kizazi, kipimo Cha hormones kuangalia Kama zko sawa, pia daktari atamchek kizazi Kama hakina shda kikawaida ,na mwsho ataambiwa atafanyiwa kipimo Cha mirija(kinauma hiki Ila atavumilia ni maumiv ya dakika tu)...mkikutwa na tatzo mtashauriwa na kuanza matibabu mkikutwa mko poa Basi mrilax huenda wakat wa Mungu bado...All the best na Mungu awajaalie mapacha dabodabo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom