Naomba kujuzwa dawa ya jino bila kun'goa

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,382
1,208
Nasumbuliwa na jino linauma balaa sitaki kulin'goa maana mapengo niliyonayo yanatosha, alafu Kuna mtu kanitisha kaniambia ukienda kun'goa jino umri huu 30+ unaweza kupata shida kwenye macho.

Kama Kuna mtu anajua dawa ya jino anisaidie jana sijalalaa, nikila chakula cha moto maumivu maji ya baridi maumivu.

Dawa ya jino bila kun'goa jino.
 
Nasumbuliwa na jino linauma balaa sitaki kulin'goa maana mapengo niliyonayo yanatosha, alafu Kuna mtu kanitisha kaniambia ukienda kun'goa jino umri huu 30+ unaweza kupata shida kwenye macho...
Nenda kwa wataam wa meno, Kuna utaalam wa kuziba Kama Kuna tundu. Then unapewa dawa, inabak kupiga mswak daily mara mbil, jino halitosumbua tena
 
Tumemzika mtu wiki hii kwa kugoma kung'oa jino, kuja kushtuka yule mdudu alikua ameharibu fizi vibaya sana, amefariki maskini.
 
Tumemzika mtu wiki hii kwa kugoma kung'oa jino, kuja kushtuka yule mdudu alikua ameharibu fizi vibaya sana, amefariki maskini.
Basi na mimi nitafariki maana meno yangu karibu yote ni mabovu huwa yanalegea bila kuuma na kutoka yenyewe ila hili linauma na Kuna lingine ukiligusa linauma pia
 
Nenda kwa wataam wa meno, Kuna utaalam wa kuziba Kama Kuna tundu. Then unapewa dawa, inabak kupiga mswak daily mara mbil, jino halitosumbua tena
Miaka ya nyuma nikiwa mdogo meno mawili ya juu ya mbele yaliweka tobo nikapelekwa hospitali wakaziba kilichotokea pale walipoziba siku zilivyokuwa zinaenda pakabanduka alafu pakatengeneza kama mwanya mpaka saiv hayo meno mawili yamepukutika yenyewe na kubaki pengo bila kuuma bila kun'goa Kama kuna mdudu anashambulia huyo mdudu ni hatari bado unanishauri nikazibe?
 
Nenda hosptal kujua shida ya meno yako. Huenda shida haiko kwenye jino. Wataalamu watakwambia ufanye nini
 
Tiba za asili hazina guarantee utatumia gharama nyingi sana hadi siku utakapokuja kuibahatisha dawa sahihi.
Maana utakuwa unajaribu kwa wataalamu mbalimbali hadi umpate mtaalamu mkweli
Ndo maana anaomba ushauri ili apate dawa sahihi bila kutumia gharama kubwa Kama ulivyosema mababu zetu walitumia dawa za asili walikuwa very strong.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom