Naomba kujuzwa dawa ya ganzi

Mdadamwema.

Senior Member
Aug 7, 2014
150
169
Nawasalimu wakuu.

Mwenye kujuwa dawa ya hii shida naomba anisaidie tafadhali.

Ninashida ya kufa ganzi viganja vya mikono hasa kwenye vidole yaani huwa vinapokezana,vinaweza kufa ganzi vidole viwili vya mwisho au vya Kati tu au wakati mwingine kiganja kizima, na mikono pia hupokezana,na hii hutokea nikiwa usingizini,nikishituka mara nyingi huwa nakutana na hii hali,nikivitikisa tikisa Hali hiyo hupotea.

Hali hii ilinianza miaka miwili iliyopita baada tu yakufanyiwa upasuaji kwenye kizazi kwa ajili ya kuondolewa uvimbe/ fibroids, baada ya upasuaji huo nilipatagwa na hali fulani ya kushoka Sana na udhaifu mkubwa ila baadae ni ka recover na ndipo nilipoanza kuhisi hali hii, hali hii huja na kutoweka, yaani wakati mwingine hutoweka kabisaa na baadaye kurejea tena,naona sasa hivi imenirejea tena, niliwahi kwenda hospital Dr akaniandikia dawa ni nuro support, lakini hata sijapona, yaani ganzi huwa inajiondokea yenywe na kurudi tena, naona sasa hivi imenianza tena, mwenye kujuwa dawa naomba anisaidie wakuu.
 
Pole sana kwa shida hiyo, no vyema ukamuona neurologist na ukafanya uchunguzi wa kina.

Shida inaweza kusababishwa na vitu vidogo kama kuvaa saa inayobana kwa muda mrefu au shida kubwa kama nerve impingement kwenye shingo/uti wa mgongo.

Mara nyingi physiotherapy na baadhi ya dawa husaidia kupunguza tatizo hili
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako nitaufanyia kazi.
 
Kama ulivyoelezwa, ni vyema kuwaona madaktari kati ya neurophisian/daktari wa mishipa ya fahamu au physician/daktari bingwa wa magonjwa ya ndani.

Unahitaji kusikilizwa na kuangaliwa vyema, tatizo laweza kuhusisha mambo kama:

A: mishipa ya damu
B: mishipa ya fahamu
C: Ukosefu wa vitamins
D: kubanwa kwa mishipa/mshipa wa fahamu
E: Tatizo la mfumo wa kinga mwilini
F: Aina ya kazi mfano: typing
G: kiasi cha mafuta mwilini etc.

Sasa ili kutanabaisha na kupata tiba njema na ushauri unaoendana na tatizo ni vyema kupata watu wa msingi huo hapo juu.
 
pole bidada wadau watakupa mawili matatu utapata ufumbuzi,mimi ushauri wangu,inaweza kuwa upungufu wa vitamin esp zinazohusika na nerves hivyo unaweza kutumia suppliment inaitwa NAT B ingrendient yake ni kubwa inaweza saidia kuristo mapema au ukikosa hiyo tumia GINKGo BILOBA nayo itakufa vizuri kwenye ubongo cranial nerves ni hayo tu.
 
Nawasalimu wakuu.

Mwenye kujuwa dawa ya hii shida naomba anisaidie tafadhali.

Ninashida ya kufa ganzi viganja vya mikono hasa kwenye vidole yaani huwa vinapokezana,vinaweza kufa ganzi vidole viwili vya mwisho au vya Kati tu au wakati mwingine kiganja kizima, na mikono pia hupokezana,na hii hutokea nikiwa usingizini,nikishituka mara nyingi huwa nakutana na hii hali,nikivitikisa tikisa Hali hiyo hupotea.

Hali hii ilinianza miaka miwili iliyopita baada tu yakufanyiwa upasuaji kwenye kizazi kwa ajili ya kuondolewa uvimbe/ fibroids, baada ya upasuaji huo nilipatagwa na hali fulani ya kushoka Sana na udhaifu mkubwa ila baadae ni ka recover na ndipo nilipoanza kuhisi hali hii, hali hii huja na kutoweka, yaani wakati mwingine hutoweka kabisaa na baadaye kurejea tena,naona sasa hivi imenirejea tena, niliwahi kwenda hospital Dr akaniandikia dawa ni nuro support, lakini hata sijapona, yaani ganzi huwa inajiondokea yenywe na kurudi tena, naona sasa hivi imenianza tena, mwenye kujuwa dawa naomba anisaidie wakuu.
Pole sana mkuu nitafute kwa wakati ili nipate kukutibia maradhi yako upate kupona.
 
Back
Top Bottom