Naomba kujuzwa bei ya PSU (Power Supply Unit)

Decodier

Member
Jul 3, 2020
55
125
Lengo la huu uzi ni kutaka msaada kama kuna watu ambao wana ufahamu na uzoefu juu ya biashara za vifaa vya kompyuta. Mimi sio mzoefu wa mambo ya computer hardware.

Naomba kujua bei ya power supply ya DELL ambayo ni used je ninaweza kuiuza kuanzia shilingi ngapi? Maana nawafahamu vizuri mafundi wa simu na kompyuta ni walanguzi kwelikweli.

Pia mbali kwa mafundi wa kompyuta ni sehemu ipi nyingine ambayo ninaweza kwenda kuiuza.
 

ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,975
2,000
Powersupply za kichina , mpya zinauzwa kati ya 20,000 hadi 40,000. Hapo naongelea zile za computer za kawaida zenye watts takriban 300w - 550w.

Sasa kama hiyo yako ni ile original kabisa inayokuja na pc kutoka kiwandani, basi unaweza kuuza bei kama 35000/ . Hayo ndio makadirio yangu.
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,010
2,000
1. Unatakiwa ujue ina watts ngapi ukisoma kwa juu hapo utaona.

2. Sababu kampuni kama Dell wanatumia proprietary power supply mara nyingi unatakiwa pia ujue ina pin ngapi, hapa angalia mwisho kwenye waya za kuchomekea.

3.size ya hiyo power supply maana hizi comouter kuna small form factor vidogo, mid tower za size ya kati na tower zile kubwa, unaweza piga picha watu wakaona muundo.

Kuhusu bei inategemea na hayo mambo hapo juuu, ila psu za dell ikifika watts 300 ama zaidi unaweza uza laki na kuendelea, nyingi ni watts 180 mpaka 240 na hazina issue kivile sababu haziruhusu upgrade ya maana.
 

ymollel

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,975
2,000
Powersupply almost zote za tower zinaanzia 300W. Bila kujali ni ya kisasa au ni ya zamani. Powersupply yoyote iliyo chini ya 300W ni ya aidha chini ya pentium 4 au ni hizi desktop za kulaza mezani/mini tower.

Angalia hapo nimeweka ya 305W ni ya optiplex 745 na hiyo ya 240W ni ya mini tower
 

Attachments

 • IMG_20200720_092902.jpg
  File size
  452.9 KB
  Views
  0
 • IMG_20200720_092846.jpg
  File size
  316.3 KB
  Views
  0
 • IMG_20200720_092742.jpg
  File size
  371.8 KB
  Views
  0
 • IMG_20200720_092722.jpg
  File size
  474.7 KB
  Views
  0

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,010
2,000
Powersupply almost zote za tower zinaanzia 300W. Bila kujali ni ya kisasa au ni ya zamani. Powersupply yoyote iliyo chini ya 300W ni ya aidha chini ya pentium 4 au ni hizi desktop za kulaza mezani/mini tower.

Angalia hapo nimeweka ya 305W ni ya optiplex 745 na hiyo ya 240W ni ya mini tower
Kuna tower kibao zina hadi 180w, most of time wanaweka psu kutokana na Gpu/cpu iliopo ndani.

Hii 230w ya tower
Dell R8042 Optiplex GX520, 210 Tower 230W Power Supply Unit 0R8042 H230P-00 | eBay
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom