Naomba kujulishwa TRA

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
622
582
Salaam!

Kwa ufahamu wangu kuhusu TRA kama una malimbikizo ya kodi, wanakuja na barua ya wito kisha unakwenda ofisini kwao kwa ufafanuzi.

Sasa hili la wafanyakazi wa TRA kwa kushirikiana na Polisi na TISS kuvamia viwanda, magala au ofisi za wafanya biashara usiku wa manane tena siku sio ya kazi ni sahihi kweli?

Hebu nifafanulieni hili kwanza kisheria na kiutendaji kazi.

Asante
 
images01.jpg
 
hili la TRA kama halijakukuta unaweza kulibeza lakini ni kweli wanasumbua wafanyabiashara kiasi cha kuatarisha hata matarajio ya makusanyo ya mbeleni kuwa mashakani. Kuna matukio mengi ya kuweka zuio kwenye accounts za mabenki za makampuni. Kufungia makampuni accounts za benki nalo si jambo dogo! Na tatizo unakuta kampuni kwa miaka mitatu mapato yote hayazidi 1b, inaletwa kodi zaidi ya 1.2b, ambayo ikija kuhakikiwa atatakiwa kulipa si zaidi ya 50m . hii ni nini!

kuna madhara mengi wanayoyaleta kwenye uchumi kwa kusumbua makampuni kufanya biashara kwa sababu ya kodi zisizo halisi na za kubambikiza, mfano

-- Hiyo kampuni inakodi jengo pengine la mashirika ya serikali kama Pensions funds n.k.
-- Ina wafanyakazi ambao wana familia na wakipata hela wanaziingiza kwenye mzunguko unaochangia makusanyo ya kodi za mbeleni
-- kampuni hizo zina mikopo kwenye taasisi za fedha ambazo ikitokea ikasimamisha biashara, mikopo hiyo hailipiki.
-- makampuni binafsi ndo yanachangia pakubwa kwenye kukuza ajira nchini, ukiyafanya yasifanye biashara unaongeza tatizo la ajira.

kuna mlolongo mwingi wa madhara yanayotokea. Hivyo ni vizuri hawa watu na wasimamizi wao wasiwe kikwazo. kila jambo lina mlango wa kutokea basi wajitadhimini na kuwa wawezeshaji si wakwamishaji.

itafutwe njia mbadala ambayo haitawafanya makampuni kufunga biashara au kusimamisha miamala yake ya mabenki wakati TRA wakiendelea na kazi nzuri ya kukusanya kodi ambazo zinasaidia kujenga taifa letu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom