Naomba kujulishwa mila, tamaduni na desturi za Wakaguru

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,483
5,797
Mimi ni Mtanzania chotara wa Kinyakyusa na Kisukuma ila nimetokea kumpenda binti wa Kikaguru na ningependa kujua kwa ndani mila, tamaduni na desturi zao ikiwemo namna wananvyo mama mjamzito, mama mzazi na malezi ya watoto, nafasi ya mqanaume katika jamii, mapishi na vyakula, shughuli zao za uchumi, matambiko, mazishi, ndoa na mahari nk
Asanteni sana wadau.
 
Wakaguru (au Wakagulu) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Morogoro, ambako wako zaidi katika wilaya za
Kilosa na Gairo . Ni mojawapo ya makabila makuu katika mkoa wa Morogoro.
Pia wako katika mkoa wa Dodoma ( Mpwapwa na Kongwa ), Kiteto na sasa wanatanuka zaidi maeneo ya Handeni . Mtawala wao hujulikana kwa jina la Mundewa.

Mila na desturi

Kufikia karne ya 18 mnamo mwaka 1776 kabila la Wakaguru lilikuwa linajulikana uwepo wake likiwa na mila na desturi zake ambazo ndizo miongozo na dira ya maisha ya kuelekeza jamii katika makuzi mazuri.
Vipengele vinavyohusisha mila na desturi za Wakaguru ni kama vile: jando na unyago ,
tambiko na uchawi , kumaliza misiba (mwidiki),
kuzikana , ujenzi wa nyumba , ngoma za jadi na
michezo , kusalimiana, elimu, ufundi, biashara na uchumi , kilimo na mazao , ndoa na mahari,
ulinzi na usalama, ufugaji , utawala n.k.
Kufikia sasa zipo mila na desturi ambazo zinaendelezwa, wakati nyingine zimeachwa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuingiliwa na tamaduni nyingine. Humu huchambuliwa kwa undani kidogo ili kufahamu utamaduni wa Wakaguru tokea mwanzo na kuona mila zipi zinatakiwa ziendelezwe na zipi zipigwe vita kwa maana zimepitwa na wakati.
 
Naomba kujulishwa watu maarufu kutoka kwenye kabila hili, ie wasomi, viongozi wa dini, Wanasiasa, wanamichezo, wafanyabiashara etc

Shabiby, rose muhando, Dr. Aaron Chiduo, watafute gairo huko ndugu zake na profesa palamagamba kabudi aliwataja nimewasahau...
 
Kwa ufupi mkuu nikusaidie,

Wakaguru ni watu wapole sana. Mara nyingi (asilimia kubwa) huwa ni wapole na wakimya. Hawana makuu kabisa.

Wakaguru wengi ni washika dini, wanapenda sana dini na wengi ni wakristu (Anglikana na Rutherani) japo maadhehebu mengine yapo ila hata wale waislam ni washika dini. Wamelelewa kwa misingi ya dini hasa.

Wakaguru wanamuamini sana mjomba! Mjomba ana nguvu sana ukaguruni.

Shughuli kuu ya kiuchumi ni kilimo. Wanalima mazao mbali mbali kama viazi vitamu, mahindi nk. Wafugaji wapo pia

Chakula kikuu cha wakaguru ni ugali na mboga za majani
 
mkuu asilimia kubwa ya wakaguru sio wakuishi maisha ya ndoa.. n kuzaa na kuishi ...
na kumbuka ni wachache kwa population ase, so usifananishe wakaguru hao ulioeleza hapo juu na hawa waliojaa pwani, dar..
hizo characteristics ulizoeleza ni za wa gairo, ukimtoa huko mlete jijin au mkoa mwingine, na akijanjaruka tu,, utaniambia
 
Hawana tofauti na wagogo na lugha zao zinaendana sana, wapo mpwapwa, kongwa, mlali. Supika jobu ni mkagulu
 
Kabila halijawahi isemea nafsi ya mtu. Usimchunguze sana bata, hutomla wewe furahia utamu wa nyama yake then over.
 
Hapo mke umepata,
ni kabila pekee Mkoani Morogoro lenye watoto wasio na Wenge. Wengi ni washamba kama wale wa Kigoma.
 
Back
Top Bottom