Naomba kujulishwa hatua za kumshtaki mtu aliekutapeli mtandaoni

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,224
3,491
Maada husika inajieleza...
Ndugu wakubwa na Wadogo habari zenu
Kwanza niombe tu samahani kwa ambao chapisho langu litawakwaza kwa namna moja au nyingine wasitoe lugha za kashfa katika chapisho hili!

Kuna mtu amenitapeli tuliewana nae anitumie Mzigo kwa makubaliano mengine ila ametuma Mzigo pungufu tofauti na makubaliano na katika kuulizia amedai nimpeleke popote ninapopajua.

Kwa kweli, ukweli wangu ni kwamba sina uhakika wa kufika dar es salaamu kwa ajili ya kumshtaki ila ushahidi wa sauti na Messege zake zote tangu mwanzo wa makubaliano hadi saizi ninazo.

Swali langu ni kwamba Je? Ninaweza kumshitaki vipi hata nikiwa nje ya Jiji la Dar es salaamu ili nipate haki yangu? Na kama utaratibu huo utakuwepo taratibu zake zipoje?
 
Kwa bahati mbaya siwezi kukusaidia lakini ninataka kukuambia kwamba una bahati nzuri kwa sababu huishi Zanzibar ambapo SMZ wanasaidia sana matapeli!😡
 
Unaweza kumshitaki ila jua utatumia muda na pesa nyingi kutopata unachokitafuta, next time kuwa smart unapofanya manunuzi ya mbali na ulipo, achana na habari za kukubaliana, wabongo uaminifu katika biashara bado ni zero, uongo na utapeli ni mwingi.
Kama upo mbali tafuta mtu unaemwamini kama rafiki au ndugu, akusaidie kukamilisha na kukagua unachotaka kununua ndipo utume pesa, nayeye hakikisha unampa ya kumlinda na kumpotezea muda kufatilia mambo yako.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom