Naomba kujua zaidi kuhusu Toyota Crown Majesta

LJ BLOG

Senior Member
Jul 24, 2011
194
151
Habari wanazengo wa JF kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuomba kupata ufafanuzi zaidi kuhusiana na Gari hii ya TOYOTA CROWN MAJESTA ambayo kiukweli nimetokea kuikubali na kuipenda na moja ya sababu ya kuipenda ni kuwa na injini ya mfumo wa V8 na mifumo mingine mingi tu kama SUPERCHARGE option yenye gia 6 ambayo inawezesha gari hili kuzalisha nguvu ya 253 kW (339 hp; 344 PS).

Kwahio Napenda kuchukua nafasi hii kupata kusikia maoni ya wadau wengine humu ndani wajuzi wa maswala ya Magari Wanaielezea Vipi hii Gari. Hii pichani ni ya mwaka 2004 yenye injini ya 3UZ-FE V8

Naombeni kusikia Kutoka kwenu Strength na Weakness zake
c1.jpg
c2.jpg
c3.jpg
c4.jpg
 
Vipi kuhusu subaru foresta? Inaweza kuchuana na crown athlete(my dream car)
Subaru ipi? Kama Forester ya mwaka 2009 na kuendelea yenye CC2500 hivi, ikiwa na 240kph, hiyo athlete yako itaachwa kama mtoto mdogo.

Na hawa Fuji Heavy Industry ni kiboko, magari yao hupata nguvu ukikanyaga kidogo mafuta, wakati wewe unaitafuta 80kph ndani ya sekunde 3 mwenzako anatafuta 100kph. Ndo utofauti unaanzia hapo. Kwamba Subaru ya cc 1990 inapata speed kubwa ndani ya muda mfupi(acceleration) kwa muda mfupi though the same Speed at maximum wote gari ina 180kph.
 
Juzi nimedrive hiyo foresta ya CC 1900 nakibaliana na wewe kabisa kwanza ile pipe inapuliza na inachanganya mapema kwa kifupi nilijifananisha na kigari changu nikaona kumbe naendesha gari la kawaida sana
 
Baada ya Kuendelea kuitafiti Toyota Crown Majesta hususani Uzao wa Nne toleo la Mwaka 2004 ambayo ina engine code 3UZS-FE V8 kiukweli nimetokea kuikubali kutokana na vitu vingi baada ya kuona ni gari yenye Airbags 9 nadhani inaweza kuwa moja kati ya gari chache za TOYOTA kuwa na AIRBAGS nyingi maana nyingi zina airbags mbili.

Lakini Seat zake nimezipenda kutokana na kuwa za umeme lakini pia na heater kupelekea Dereva na abiria kuwa more comfortable pale wanapohitaji heater kwenye seat zao. Lakini pia Kuwa na Air Purify nayo imekuwa kigezo kizuri sana kwenye gari hii, Lakini pia Kuwa na DUAL A/C dereva au abiria akitaka kipupwe kikali anajichagulia huku dereva akichagua kiwango chake cha kipupwe bila kuathiriana na abiria.

Lakini mfumo wa sunspension zake nimeupenda pia kutokana na Kuwa na Option za High, Height na Normal lakini pia sunspension zake ni za umeme ambapo zina option mbili za SPORT na Normal lakini Pia taa zake za mbele ni Directional ambapo zinamulika pale ambapo unaelekea pindi ukikata kona zinamulika upande unaokata kona. Pia ni Gari yenye Cooler Box kwenye Seat za nyuma za abiria

Kutokana na Kuwa na Nguvu, Speed na Comfortability Hii gari inazalisha nguvu ya 253 kW (339 hp; 344 PS). Hapa sasa nadhani Wale wapenda mbio, Basi hili linawafaa kwasababu hata ground clearance yake ni nzuri pia. Kibongo Bongo ukiamua kuiagiza inaweza kukugharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Mil 16

Kuhusu Mafuta sidhani kama inaweza kuwa tishio kihivyo kwasababu kwa mujibu wa taarifa zao wanasema kuwa Lita Moja inaenda mpaka KM 18 - 19 . Tukiogopa sana Mafuta Tutashindwa kumiliki Magari mazuri aisee

Kwenye mbio nadhani mnyama huyu anaweza kuchuana na Land Cruiser V8 na aina nyingine za SUV lakini hizi sedan nyingi tu zitakuwa zinasoma namba kwa huyu Mnyama Aisee
c10.jpg

c1.jpg

c7.jpg

c3.jpg
 
Back
Top Bottom