Naomba kujua watu humaanisha nini hasa wanapotamka maneno haya

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
2,952
5,872
Hii nimeisikia mara nyingi ila kiukweli huwa sielewi: kwa mfano unakuta mtu anasema,

"lazima na haya yanatuhusu bhana, Tanzania sio kisiwa" kwani kisiwa huwa hawaishi watu? Wametengwa? ... Kwanini jambo hilo linalobishaniwa litajwe kwa kulinganishwa na kisiwa?

Au utasikia mwingine akisema, "daa, aisee siku hizi umepotea, kama uchi wa mtoto!" Swali langu, Kwani uchi wa mtoto huwa umepotea, hauonekani? Mbona huwa tunawaona watoto kila siku wakiogeshwa na mama zao huku kwetu uswazi.

Jingine ni hili utasikia mtu aliyekosea jambo kubwa akisema "duu aisee leo nimeingia choo cha kike" au mtu aliyetapeliwa kitu anaambiwa "... umeingizwa choo cha kike". Sasa Mimi ninajiuliza kuwa kuna jinai gani kuingia choo cha kike ukajisaidia endapo kwa wakati huo hakuna mwanamke mwenye kuhitaji huduma hiyo. Kwa mfano mnasafiri mmetoka kucheza mpira wanaume watupu, mkafika kwenye huduma ya kujisaidia mkawa mko peke yenu wanaume, kuna ubaya gani ukaingia kwenye chumba cha kujisaidia kilichoandikwa "ladies" ukamaliza mambo yako ukaondoka zako. Kufanya hivyo kuna kosa gani???

...
 
Sasa ulichokiuliza Kwetu ni nini wakati tayari hata katika Maelezo yako tu tayari umeshajijibu Mwenyewe? Hebu acha Kutupotezea Muda muhimu.
 
ngoja niwashe tochi kukitafuta unachotaka kukijua maana japo nimetumbua macho bado sikioni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom