Naomba kujua viungo tofauti vya kuweka kwenye nyama au samaki

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,435
17,076
Habari ya wakati huu.

Wakuu, najifunza kupika baada ya kuamua kupunguza kula migahawani.

Naomba kujua viungo au namna tofauti tofauti za kupika nyama au samaki. Namaaniaha viungo vya kuweka kwenye mchuzi wa nyama iwe nzuri zaidi.

Najua kupika nyama ile kawaida, kuweka nyanya, karoti, pilipili hoho, kitunguu na chumvi. Ila hua nakula migahawani nyama inanukia vizuri na inaladha nzuri, naambiwa umewekewa viungo tofauti tofauti.

Naomba kufundishwa au kuelekezwa viungo vya kupikia nyama au samaki.

Ahsanteni sana.
 
Nunua Curry powder ile ya Zanzibar masala ukiweka na Birian masala (ya zanzibar) kidoogo weee mbona utang'ata vidole.

Aisee mchuzi bila curry powder na thom (vitunguu saum) hua haupandi kabisaaa nitajilazimisha tu.
 
Nunua Curry powder ile ya Zanzibar masala ukiwela na Birian masala (ya zanzibar) kidoogo weee mbona utang'ata vidole.

Aisee mchuzi bila curry powder na thom (vitunguu saum) hua haupandi kabisaaa nitajilazimisha tu.
Tangawiz kidogo pilipili mbuz ndogo kutia ladha tu
 
Nunua Curry powder ile ya Zanzibar masala ukiweka na Birian masala (ya zanzibar) kidoogo weee mbona utang'ata vidole.

Aisee mchuzi bila curry powder na thom (vitunguu saum) hua haupandi kabisaaa nitajilazimisha tu.
Nachanganya vipi au nawekaje kwenye mchuzi.
Je hiyo vitunguu saum imesagwa au nahitaji kuponda ponda kwenye kakinu kadogo?
 
Tangawiz kidogo pilipili mbuz ndogo kutia ladha tu
Hiyo tangawizi inahitaji kupondwa pondwa au kuna powder yake?

Je roiko(Royco) na hizo masala hua kuna tofauti gani, je naweza kuchanganya pamoja kwenye mchuzi?

Ahsante.
 
Nunua Curry powder ile ya Zanzibar masala ukiweka na Birian masala (ya zanzibar) kidoogo weee mbona utang'ata vidole.

Aisee mchuzi bila curry powder na thom (vitunguu saum) hua haupandi kabisaaa nitajilazimisha tu.
Weekend nakuja kuonja hayo mapishi
 
Nachanganya vipi au nawekaje kwenye mchuzi.
Je hiyo vitunguu saum imesagwa au nahitaji kuponda ponda kwenye kakinu kadogo?
Aisee kuandika itakua mtihani ila ngoja nijaribu,
Nyama yako ikiwa mbichi ioshe vizuri, weka chumvi, limao, Tangawizi au Thom au vyote (i prefer thom pekee)
weka jikoni ichemke hadi iive, wakati unasubiri nyama iive anza kuandaa viungo,
Kitunguu,
Nyanya, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Karoti, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Hoho,
Thom iliyopondwa kwa kinu(inakua fresh) ni bora kuliko ya unga.

Ninavyopika sasa hehehe culture gal akiwa jikoni kama najiona vile.... lol.

Nyama ikiwa haina mifupa wala huna haja ya kubadili sufuria, weka mafuta kidogo sana kama haina mafuta nyama,
Tupia kitungua maji kaanga kiasi hua sipendi ule utaratibu mpk kiwe cha brown,
tupia karot, hoho na thom.... endelea kukaanga nyama na viungo vyako kiasi kisha weka nyanya pmj na unga wa Curry powder kama kijiko kimoja cha chai au viwili kutegemea na upendavyo, tupia na unga wa birian masala kama nusu kijiko cha chai hivi kuongezea ladha.... endelea kukaanga mpk nyanya ziive, (nyanya ziache mpk zianze kushika chini maana ukiwahi kuongeza maji zitakua bado mbichi na kuharibu ladha ya mchuzi wako)

Tupia pilipili kama ni mpenzi kama sio waweza kuacha maana hata curry ina ladha ya pilipili kwa mbaali.

Utaweka maji kiasi ni vema kuacha mchuzi mzito kuliko chururu kama wa kipemba (lol am sorry wapemba).

kisha epua mchuzi wako tayari kwa kuliwa iwe chapati, wali, maandazi, tambi au ugali.

Same procedure na samaki.
 
Hiyo tangawizi inahitaji kupondwa pondwa au kuna powder yake?

Je roiko(Royco) na hizo masala hua kuna tofauti gani, je naweza kuchanganya pamoja kwenye mchuzi?

Ahsante.

Royco sijui simba mbili zote ni masala.... ndio maana nikasema me napenda masala ya zanzibar, kuna wengine wanapenda masala ya india, wengine kenya ndio hao kina royco kama sikosei....

Vyote unatumia kwa mchuzi haina shida.

Tangawizi ya unga ipo ila pendelea kutumia vitu fresh kwa afya na ladha nzuri.
 
nijuavyo mimi ukishaosha nyama yako vizuri weka
chumvi
tangawizi
garlic
kamulia na ndimu kidogo then koroga kidog
weka jikoni usiweke maji kwanza yake maji ya kwenye nyama ndo yatavipika ivyo viungo viingie kwenye nyama vizuri na ilainike then ikianza kukaukia weka maji yakuivisha nyama nyama ikishaiva epua
andaa kitunguu maji
karoti
hoho
nyanya
etc
weka sufuria jikoni na mafuta
vikipata moto weka kitunguu maji kisiive sana (kwa mimi)
weka nyama kavu kwenye ivyo kitunguu koroga nyama mpka ikauke vizuri na vitunguu then weka karoti koroga kidogo then hoho visiive sana then weka nyanya funika kama dakika4 then funua koroga ule mvuke ukitoka nyanya inakuwa haina maji maji then weka size ya maji unayopendelea mchuzi wako
au vikorombezo vingine kama unavyopendelea kama ni royco, cotmill, masala,,,,, kuleta test
nitumiage na hela ya pepsi
 
Kunywa hata togwa nakuja kulipa. Ahsante sana. Ubarikiwe sana.
 
Baada ya kuviandaa kwa usafi twanga kwa pamoja kitunguu swaumu ,tangawizi na giligilani kwa pamoja...tupia ktk mafuta wakati Wa kukaanga vitunguu ......
 
Back
Top Bottom