Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Nauliza kwa ufupi sana,

Je, ni kwanini alama ya chanjo ya Ndui ipo kwa waTz tu? Ina maana hii small pox inadhuru Watanzania tu?
 
Kenya wenyewe wanaambiwa nyoosha mkono waangalie hio alama ya ndui, Ethiopia wao wanachanjwa begani Kama sisi.
 
Ili ng'ombe wako asipotee ni lazima umuwekee alama ya muhuri wa moto....

Yaani ukizamia tu nchi jirani, wanaangalia mabega tu wanafahamu kwamba huyu katokea Tanzania.
Kuna dada mmoja aliwahi kuleta kisa humu kuwa alienda kambi ya JWTZ Lugalo lakini akasahau kitambulisho chake cha kazi kwa maana yupo private sector. Aliendelea kwa kusema mwanajeshi walimpa kash-kash nyingi ikiweo kuangaliwa kama ana alama ya ndui begani.

Pia msanii wa bongo flavor Professor Jay aliwahi kuimba kama wimbo wake wa "hapo vipi, hapo sawa" aliimba kuwa "begani nina alama ya ndui mtanzania namba moja majungu hayasumbui"

Kuna dada mmoja alisomea udaktari Cuba alikuwa sweetheart wangu mwaka 2017..........
 
Small pox tz tu? Kwqnza naambiwa sikuhizi watoto wanadumgwa mivhanjo lukuki zaidi ya tatu huko yaani kama kuku wa kisasa
😣😥😑😐😯😶😫😴😪😌
 
Kusema ukweli nachukia izo chanjo mbon mabibi na mababu zetu hawakuchoma ila mpk leo wapo wanaish vzr tu?
 
Mataifa karibu yote wanatoa chanjo ya Ndui kwa Raia wao, ila kila nchi sehemu ya kufanya hyo chanjo.

Niliwai kuona kovu la ndui kwa mhindi mmoja, ilikua mkononi(Kwenye jointshapo)

Hivyo kwa muktadha huo, wahindi unaweza kuwatambua kwa kuangalia alama ya ndui kwenye eneo hilo.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo chanjo ya Ndui( smallpox) ilishasitishwa katambo. Haipo kwenue kifurushi cha chanjo kwa watoto.
 
Back
Top Bottom