Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 11,774
- 9,965
Ukishakufa unakuwa huna cheo.Lakini mfu mmoja anacheo kikubwa
Ukishakufa unakuwa huna cheo.Lakini mfu mmoja anacheo kikubwa
Hayati hutumika kwa watu waliokuwa na nafasi kubwa katika taifa kwa mfano mwalimu Nyerere huwezi kusema tu marehemu mwl. JK Nyerere bali yeye huwa tunasema Hayati mwl. JK au Karume huwa tunasema Hayati Abeid Aman Karume. Lakini akifa hohe hahe kama Bwana Kaduga tutasema Marehemu Bwana Kaduga!!Kwa muda mrefu sana nilikua nikisikia toka kwa ndugu na watu wengine wakimuita merehemu mtu alie kufa siku nyingi zilizopita.
Hivo ilinijengea mimi pia mazoea ya kumuita marehemu, mtu alie kufa mda mrefu.
Pia nimekuwa nikisikia katika vyombo vya habari wakimuita hayati mtu ambae amekufa muda mrefu lakini akiwa na cheo fulani.
Kwa hivo katika fikra zangu zimeweza kufikiri kuwa huenda kuna makundi mawili ambalo kundi la kwanza ni la wale wasio na cheo chochote katika taifa ndio huitwa marehemu lakini pia kundi la pili ni la wale wenye vyeo katika taifa ndio huitwa hayati, sina uhakika na fikra zangu.
Kwahivo nimeona ni bora niilete huku mada ili niweze kupata uhakika wa tofauti kati ya marehemu na hayati.
JamiiForums great thinker.
Hilo neno hayati waswahili wa mwanzo walilielewa vibaya,ni neno la kiarabu lenye maana hai milele,sasa mtu kafa anakuwaje hayati!?Mimi ni Kapuku flani tu, ila naomba nikifa mnipe cheo cha hayati kama hayati Bob Marley na hayati Tupac...
Ina maana wewe hujui kwamba kuna watu wamekufa lakini wanaishi?Hilo neno hayati waswahili wa mwanzo walilielewa vibaya,ni neno la kiarabu lenye maana hai milele,sasa mtu kafa anakuwaje hayati!?
We mngoni VP? upoo? umerefuka? uko kino?Hayati na marehemu ni sawa tu. Inategemeana anayeitwa ana nyazifa gani
Hayati sokoine,hayati kolimbaIna maana wewe hujui kwamba kuna watu wamekufa lakini wanaishi?
Ni kwa nini kila siku kwenye tv zenu mnaweka nukuu za Nyerere?
Bob Marley muziki wake kuna mtu ameweza kumpiku mpaka leo? Jiulize mwenyewe marehemu kwa miaka karibu 30 waluo hai wanashindwa kumbeat.
Hayati ni neno sahihi kwa watu hao.
Aliyefariki anaweza kuitwa hayati kama alikua kiongozi wa juu kabisa wa serikali
Aliyekufa hawezi kuitwa hayati huyu ni marehemu tu..
Kuna ku-dead na ku-pass away
mfano hayati ni kiarabu, marehemu imetokana na kngereza neno late
Marehemu ni maiti. Na maiti ni mwili wa mfu. Ule mwili unaoubeba kwenda kuuzika ndio marehemu. Hayati pengine kwa makusudio ya kiswahili ni mtu aliyewahi kuishi. Kwasababu muda ukishapita mwili hupotea hubakia sifa tu kwamba fulani aliishi. Na pengine pia hutumika neno hayati kama kwamba mtu huyo bado yuko pamoja nanyiNi nani anatakiwa aitwe Marehemu na ni nani anatakiwa aitwe Hayati na ni wakati gani haya Maneno mawili yanatakiwa Kutumika hasa 'Kiuwasilishaji' pale linapotakiwa Kuelekezwa kwa Mhusika ( aliyeaga ) dunia?
Ni maneno ambayo kwa muda mrefu yananichanganya na Kunifikiisha mno hivyo ni matumaini yangu leo hii wana JamiiForums ( Great Thinkers ) na Wabobezi Waandamizi wa Lugha adhimu ya Kiswahili mtanielimisha.
Ahsanteni.
Marehemu ni maiti. Na maiti ni mwili wa mfu. Ule mwili unaoubeba kwenda kuuzika ndio marehemu. Hayati pengine kwa makusudio ya kiswahili ni mtu aliyewahi kuishi. Kwasababu muda ukishapita mwili hupotea hubakia sifa tu kwamba fulani aliishi. Na pengine pia hutumika neno hayati kama kwamba mtu huyo bado yuko pamoja nanyi