Naomba kujua tofauti ya Kimatumizi ya haya maneno mawili ya Marehemu na Hayati kwani huwa yananichanganya mno

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,558
Points
2,000

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,558 2,000
Ni nani anatakiwa aitwe Marehemu na ni nani anatakiwa aitwe Hayati na ni wakati gani haya Maneno mawili yanatakiwa Kutumika hasa 'Kiuwasilishaji' pale linapotakiwa Kuelekezwa kwa Mhusika ( aliyeaga ) dunia?

Ni maneno ambayo kwa muda mrefu yananichanganya na Kunifikiisha mno hivyo ni matumaini yangu leo hii wana JamiiForums ( Great Thinkers ) na Wabobezi Waandamizi wa Lugha adhimu ya Kiswahili mtanielimisha.

Ahsanteni.
 

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,558
Points
2,000

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,558 2,000
Aliyefariki anaweza kuitwa hayati kama alikua kiongozi wa juu kabisa wa serikali
Aliyekufa hawezi kuitwa hayati huyu ni marehemu tu..

Kuna ku-dead na ku-pass away
Shukran kwa Elimu yako ya Awali na ngoja niwasubiri wengine ili niweze Kuelimika zaidi juu ya haya maneno mawili ' sumbufu ' Kwangu ya Marehemu na Hayati.
 

Vitalis Msungwite

Verified Member
Joined
May 11, 2014
Messages
1,711
Points
2,000

Vitalis Msungwite

Verified Member
Joined May 11, 2014
1,711 2,000
Kufa hutumika kwa wanyama wasio binadamu na kufariki kwa binadamu.

Hayati hutumika kwa waliokuwa au viongozi wajuu kisiasa waliofariki. Nijuavyo mimi hayati laweza kutumiwa kwa Waziri mkuu na Rais.

Marehemu ni kwa wengine wote,mfano wafanya biashara wakubwa, watu mashuhuri na cheap labour wengine.

Kwamujibu wa kamusi ya TUKI

Marehemu - mtu aliyefariki

Hayati - si mfu si mzima

Yaani mtu ambaye amefariki lakini anaishi katika ulimwengu uliopo kwa mchango wake katika nchi. Wakimaanisha kuwa yale aliyoyafanya marehemu yanaishi.
 

Forum statistics

Threads 1,344,274
Members 515,388
Posts 32,813,827
Top