Naomba kujua tofauti ya kimajukumu kati ya TANROADS na TARURA

sawee225

JF-Expert Member
Jun 14, 2017
3,220
12,089
Wakuu wasalaam

Naomba kujua tofauti ya kimajukumu kati ya TANROADS na TARURA

Nawasilisha
 
TANROADS Majukumu yao ni usimamizi, ukarabati na ujenzi wa barabara za mijini .
TARURA Majukumu yao ni usimamizi,ukarabati,na ujenzi wa barabara za vijijini. OVER
 
TANROADS Majukumu yake ni usimamizi ,ukarabati na ujenzi wa barabara zinazounganisha
1.Nchi moja kwenda Nyingine
2.Mikoa miwili au zaidi
3.Wilaya mbili au zaidi.

TARURA Majukumu yake Ni usimamizi, ukarabati na ujenzi wa Barabara zinazounganisha
1.Tarafa mbili au zaidi
2.Kata mbili au zaidi
3. Vijiji viwili au zaidi
4.Mitaa mbalimbali maeneo ya mjini.
 
Mbona Kuna road za mitaani zinasimamiwa na TANROAD.
 
Mbona Kuna road za mitaani zinasimamiwa na TANROAD.
Hii hutokea kwa baadhi ya miradi,
Maana katika mradi huwa Kuna msimamizi na mkandarasi, Kuna miradi hushindanisha wasimamizi (Consultants) wengi ili kupata msimamizi atakaekidhi vigezo vya usimamizi mfano ndani ya TANROADS Kuna kitengo Cha TECU kitengo hiki kinaweza kushida zabuni za usimamizi wa mradi wowote ule.
Usishangae hata bwawa la kufua umeme kule Rufiji pia linasimamiwa na TANROADS kupitia kitengo Chao Cha TECU.
 
Okey
 
Ukitaka kutumia hifadhi ya barabara kwa biashara inabidi uwalipe wote wawili kila mtu kivyake, hapo bado manispaa, tra na wengine
 
TANROADS Majukumu yake ni usimamizi ,ukarabati na ujenzi wa barabara zinazounganisha
1.Nchi moja kwenda Nyingine
2.Mikoa miwili au zaidi
3.Wilaya mbili au zaidi.

TARURA Majukumu yake Ni usimamizi, ukarabati na ujenzi wa Barabara zinazounganisha
1.Tarafa mbili au zaidi
2.Kata mbili au zaidi
3. Vijiji viwili au zaidi
4.Mitaa mbalimbali maeneo ya mjini.
Na kwa jiji kama Dar es Salaam ambako kuna Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP) hao TARURA wanasimamia barabara zipi na DMDP barabara zipi?
 
DM
Na kwa jiji kama Dar es Salaam ambako kuna Dar es Salaam Metropolitan Development Project (DMDP) hao TARURA wanasimamia barabara zipi na DMDP barabara zipi?
DMDP Ni moja ya miradi ya mikakati inaboresha barabara za miji lakini zipo chini ya uangalizi wa TARURA. Kama sijakosea miradi hii inafadhiliwa World bank,hawa DMDP wakimaliza kujenga atakabidhiwa TARURA kuendeleza shughuli zingine Kama vile ukarabati na masuala ya parking.
 
Ninachokijua, Tanroad wanadeal na Barbara juu za kitaifa zinazounganisha mikoa na wilaya mbalombali, Tarura manadeal na barabara za mitaani katika miji na vijiji husika!
Your right ndioaamana kuna Barbara za vumbi tanroads wanadeal nazo!only to connect regions and district
 
ni swala la mda tu, zitaungwa izi kuepusha utitiri wa taasisi zinazofanya kazi zinazofanana
 
Ukitaka kutumia hifadhi ya barabara kwa biashara inabidi uwalipe wote wawili kila mtu kivyake, hapo bado manispaa, tra na wengine
Katika hizo mbili, Tarura na Tanroads moja wapo imepewa mandate ya kukusanya mapato ya ma bango, na biashara kwenye hifadhi za barabara. Tra haikusanyi tena hizo tozo. Nafkiri ni Tarura.
 
Na wao wakaweka hifadhi ya barabara kwenye eneo la mtu wanalipa?kuna eneo wameweka bikon ndani ya kiwanja cha jamaa,hapo inakuwaje? Au jamaa anaweza kuendelea na miradi yake bila kujali hizo
bikon? ( jamaa alikuwa anajenga)
Ukitaka kutumia hifadhi ya barabara kwa biashara inabidi uwalipe wote wawili kila mtu kivyake, hapo bado manispaa, tra na wengl
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom