Africa Tanzania
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 1,504
- 2,261
Habari za muda huu madaktari,
Napenda kupokea ushauri wa kitabibu kutoka kwenu maana kuna mtoto wa Dada yangu alipitia yafuatayo wakati wa kuzaliwa:-
1.UJAUZITO zile tarehe za makadirio zilivuka, mtoto alizaliwa baada ya wiki mbili mbele zaidi. (zaidi ya wiki halali)
2.KUTOKULIA alipozaliwa hakulia, na madaktari walimuwekea oxygen kupumua baada ya muda wakaitoa na akawa vizuri.
3.KUMEZA MAJI wakati wa kuzaliwa kuna maji alikunywa(yale ya uzazi) na madaktari waliyanyonya kwa awamu kisha yakaisha..
Baada ya kutokea hayo, Madaktari walisema ukuaji wake utachelewa sana, pia anaweza kupata degedege au kifafa kutokana na kukosa hewa kwenye ubongo.
~mtoto alikuwa anashtuka mara kwa mara na kulia sana, alivyopelekwa tena hospital madaktari walisema ni degedege na wakampa dawa ya phenobarbital,
Hiyo dawa mpaka sasa anaitumia na usipo mpa mtoto analia sana,
Mpaka sasa mtoto anamiezi 9, hawezi kukaa. Shingo haijakaza na ukimuangalia hatofautiani na mtoto wa miezi mitatu.
Je...Tufanyaje mtoto huyu apate awe vizuri?
Ni tiba gani mwarobaini kwa case kama hii?
Hospital gani hapa Tz wanaweza kumsaidia mtoto huyu?
Nb: mtoto anahudhuria mazoezi kwrnye Center maalum, huu ni ushauri wa baadhi ya madaktari.
Tunaomba msaaada wa mawazo, ushauri au lolote neno hapo.
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app