Naomba kujua njia za kufuata kuanzisha shule ya mafunzo ya udereva

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
410
705
Wana JF naomba kufahamishwa taratibu za kufuata kuanzisha shule ya kufundisha madereva(Driving School) hapa nchi. Kama ifuatavyo.

1. Ni mamlaka gani inatoa usajiri
2. Idadi ya chini ya magari yanayohitajika kuanzisha shule.
3. Gharama za malipo ili kupata usajiri
4. Mengineyo muhimu ili kupata usajiri wa driving school.

Natanguliza shukrani zangu kwenu wana JF watukuka.
 
ila ungeweka na Lorry ungewakamata kweli kweli. Tanzania ya viwanda inakuja kwa hiyo sekta ya usafirishaji itakuwa dili baadae(ndoto)

Wenye utaalamu watakueleza
 
ila ungeweka na Lorry ungewakamata kweli kweli. Tanzania ya viwanda inakuja kwa hiyo sekta ya usafirishaji itakuwa dili baadae(ndoto)

Wenye utaalamu watakueleza
Shukrani kaka, ushuri wako ni wamaana sana kwangu. Ahsante nitalizingatia hilo.
 
Lazima uwe umepitia NIT uwe na leseni ya udereva ya class............ (kubwa) uchukue kibali trafick na uwe dereva ulie sajiliwa kwenye Chama cha Walimu wa madereva
 
Wana JF naomba kufahamishwa taratibu za kufuata kuanzisha shule ya kufundisha madereva(Driving School) hapa nchi. Kama ifuatavyo.
1. Ni mamlaka gani inatoa usajiri
2. Idadi ya chini ya magari yanayohitajika kuanzisha shule.
3. Gharama za malipo ili kupata usajiri
4. Mengineyo muhimu ili kupata usajiri wa driving school.

Natanguliza shukrani zangu kwenu wana JF watukuka.
Nenda kwa wafuatao;

1.National Institute of Transport (NIT)
2. Jeshi la polisi: kitengo cha usalama barabarani
3.Tanzania Revenue Authority (TRA)
4. Business Registration and Licensing Agency (BRELA)
5. Tanzania Roads Agency (TANROADS)
6. Surface,Marine Transport Regulatory Authority (SUMATRA)
7.Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi

Ukienda kwa hao wahusika utapata miongozo yote ya jinsi ya kuanzisha shule ya udereva,usajili, wafanyakazi,idadi ya magari,mapato na kodi, sheria, usalama,kanuni na vinginevyo vingi kwa hiyo ni wewe tu na muda wako....JIPANGE VYEMA
 
Kama kuna mdau mwenye practical experience juu ya uanzishwaji wa shule ya udereva (Driving school), tutashukuru sana endapo ata-share experience yake. Bila kusahau changamoto na faida zake.
 
Back
Top Bottom