Naomba kujua namna Islamic Banking inavyopata faida

naomba kujua taratibu zao za mkopo mfano wa kujenga nyumba na vigezo kwa wanaojua
 
Kiufupi wanatoza riba (tena kubwa tu) ila kwa mtindo tofauti ikiwemo kuweka kona kona, ujanja ujanja wa maneno na kujitahidi kuipa jina tofauti hiyo riba.

Kama hujaelewa, embu jaribu kutafakari tofauti ya Nguruwe, Kitimoto, Mdudu na Mbuzi katoliki.
 
Hujui maana ya riba. Unyamaze tu.

Kwa mleta mada:

Benki hizo kama alivyosema mdau mmoja hapo juu, wao wanakupa wewe materials. Yaani kwa mfano wewe unataka biashara ya kuuza magari, basi wao watanunua gari mfano IST inauzwa $1000, wao watakuuzia wewe $1100. Kwahiyo wakikupa hio gari uuze, wao uwarudishie dola 1100 yao. Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba wao wanakuuzia kwa bei nyingine ila ndiyo utalipa kwa awamu mlizokubaliana.
 
naomba kujua taratibu zao za mkopo mfano wa kujenga nyumba na vigezo kwa wanaojua

Watakwambia mambo haya:

Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.

Kwa mfano:

Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.

Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonesha (kukuzuga) kuwa riba na faida ni kitu tofauti kwa kuwa Uislamu hauruhusu riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'Kswahili kiswahili'.
 
Watakwambia mambo haya.
Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.

Kwa mfano.
Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.

Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonyesha(kukuzuga!) kuwa Riba na Faida ni kitu tofauti kwa kuwa uislamu hauruhusu Riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'kiswahili kiswahili'.

Asante nimekuelewa sana mkuuu
 
Hujui maana ya Riba. Unyamaze tu.

Kwa mleta mada:
Benki hizo kama alivosema mdau mmoja hapo juu, wao wanakupa wewe materials. Yaani kwa mfano wewe unataka biashara ya kuuza magari, basi wao watanunua gari mfano IST inauzwa $1000, wao watakuuzia wewe $1100. Kwaio wakikupa hio gari uuze, wao uwarudishie dola 1100 yao. Kwaio kwa ufupi, ni kwamba wao wanakuuzia kwa bei nyengine ila ndio utalipa kwa awamu mlizokubaliana
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?

Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?
 
Wataalam wa hi kitu naamini wapo mje mtuongezee nyama hapa pia nawashukuru Sana walioshiriki katika uzi huu
 
Watakwambia mambo haya.
Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.

Kwa mfano.
Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.

Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonyesha(kukuzuga!) kuwa Riba na Faida ni kitu tofauti kwa kuwa uislamu hauruhusu Riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'kiswahili kiswahili'.
Hii kitu ni vema ikatolewa ufafanuzi na wenyewe wenye Imani ya Kiislam ili tupate maelezo sahihi

Watueleze kama hivi ndivyo na kama hivi ndivyo kuna tofauti gani na benki nyingine au wale wanaokopesha mitaani?

Maana mwisho wa siku wote wanalenga kupata faida
 
Kiufupi wanatoza riba (tena kubwa tu) ila kwa mtindo tofauti ikiwemo kuweka kona kona, ujanja ujanja wa maneno na kujitahidi kuipa jina tofauti hiyo riba.

Kama hujaelewa, embu jaribu kutafakari tofauti ya Nguruwe, Kitimoto, Mdudu na Mbuzi katoliki.
Watz bana, ulitakiwa kueleza kama wanatoza riba wanatoza kwa namna gani na sio kubwabwaja.

Mimi niliwafuatilia wakanieleza kuwa masharti yao ya kunikopesha ni kuwa hawanipi pesa bali wananipa bidhaa za duka then tuta share faida/hasara itayopatikana
 
Kiufupi wanatoza riba (tena kubwa tu) ila kwa mtindo tofauti ikiwemo kuweka kona kona, ujanja ujanja wa maneno na kujitahidi kuipa jina tofauti hiyo riba.

Kama hujaelewa, embu jaribu kutafakari tofauti ya Nguruwe, Kitimoto, Mdudu na Mbuzi katoliki.
Au Atafakari Maana Ya "Ada, Nauli, Sadaka, Mshahara" Au Wanafunzi, Abiria, Askari,)
 
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?

Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?
cc FaizaFoxy Gavana
 
Watakwambia mambo haya.
Leta mchanganuo wa gharama za ujenzi wako, sema wapi wapi zinapaswa kulipiwa, kisha wataweka faida yao ikiwa watazilipa hizo gharama. Sasa ukikubaliana nao wanakuja kulipa au kukununulia hicho unachokihitaji, mwisho wa siku wewe utakuja kuwalipa hizo gharama pamoja na faida yao.

Kwa mfano.
Wewe unataka kujenga nyumba, kiwanja unachotaka kununua kinauzwa Milioni 5, basi ukienda kwao kutaka kukopa milioni 5 ili kununua kiwanja, watakwambia tuonyeshe kiwanja na muuzaji, wao watakwenda kukinunua kwa niaba yako kwa hiyo milioni 5, na wewe utapaswa kuja kuwalipa benki Milioni 5 yao pamoja na FAIDA yao baada ya muda fulani mtakaopata. Sasa hiyo faida itakuwa kiasi gani? Hayo ni mapatano ya wewe na wao kutegemea Muda utakaotumia kulipa na kiasi utakachotaka kukopa.

Wao wanakwepa neno RIBA lakini wanataka neno FAIDA. Na ili kutaka kukuonyesha(kukuzuga!) kuwa Riba na Faida ni kitu tofauti kwa kuwa uislamu hauruhusu Riba, basi wanaweka hizo kona kona za 'kiswahili kiswahili'.
cc wafia dini FaizaFoxy Gavana
 
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?

Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?
Kukopeshwa nyumba ya milioni 100 halafu ukaambiwa ulipe milioni 150 NA Kuuziwa nyumba kwa milioni 150 na ukaambiwa ulipe kwa awamu, wewe unaona ni sawa?

Hivi wewe umewahi kuona wapi kuwa mimi nikinunua kiwanja kwa mtu kwa milioni 5, halafu nikaja kukuuzia wewe milioni 7 ikaitwa riba? :D

Halafu sasa, kwenye kufanya biashara, hasara itakayopatikana kwenye hio biashara ni hasara ya mkopeshaji na mkopeshwaji, kwa sababu mkopeshaji anahesabika kama mbia kwenye biashara na yule aliemkopesha. Sasa wewe na hio NMB yako, ukipata hasara bank inafanya nini? inapata hasara au inakuja kuchukua bondi ulioweka?

Tatizo vichuki vyenu vinawafanya akili zilale
 
Sasa nini tofauti ya benki yao inayosema haitozi Riba na benki zingine zinatoza Riba kwa mteja?

Kama mimi nikienda NMB kukopa dola 1000 halafu baada miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200, na nikienda Islamic bank(ambapo wanasema hawatozi Riba) kukopa dola 1000 na baada ya miezi sita nitapaswa kulipa dola 1200. Nini tofauti ya kimantiki?
Kuna tofauti kubwa, unapokopa benki yenye riba , riba inahesabiwa Kila mwezi au mwaka. Kwa hio kama itatokezea kwa mwezi au mwaka mmoja ulishindwa kulipa hutolipadola 1200 penine zitakuwa 2000 kwa kuchelewesha kwako. Hapo ndipo unapoingia uharamu kwenye uislamu kwa sababu unatumia matatizo ya huyo uliemkopesha ili kujiongezea wewe faida. Lakini kwenye Benki ya kiislamu ni Faida, kata kama utashindwa kurudisha kwa wakati hawaruhusiwa kukuongezea ili ulipe faida kubwa. Muhimu utoe taarifa tu mapema muwelewane muda muafaka kurudisha. Mara nyingi katika benki ya Kiislamu wanaangalia ile Faida utakayopata na ndio inayogaiwa baina yako na Wao. Kwa mfa una Duka na umeagiza Vitu China, watakuuliza faida yake ni kiasi gani? sasa ile faida utakayopata ndio inayogawanywa
 
Ukiacha kulipa deni unafanywaje?
 
Ukiacha kulipa deni unafanywaje?
Kuacha kulipa deni bila sababu haikubaliki popote. Ni hivi kuna wenzako kama wewe au mimi tunaweka Pesa kwao. Masharti yao ni kuwa wanakwambia hakuna Riba. Sasa unatokea wewe unakopa kwa masharti utarejesha na faida . Sasa hii faida unayorejeshwa ndio Islamic Bank wanaigawa Baina ya Mteja na wao. Sasa kama hukurejesha mkopo , maana yake umentia hasara mteja aliyeka zile ukapata wewe kukopa
 
Back
Top Bottom