Naomba kujua mimi ni kundi gani /mtu wa aina gani

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,562
2,000
Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;

- Mimi ni mkorofi (tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari)

- Mimi ni mkimya (yaani sipendi kuongea na pia sipendi mtu aniongeleshe kwa muda mrefu nachukia sana yaani natak nikiwa na wewe ukae kimya usiniulze maswali mengi)

- Ninapenda kampani au watu wasio wapole wapole yaani napenda watu waliochangamka(wahuni wahuni)

- Nayachukia mahusiano(ya kimapenzi) naweza kumtongoza msichana ila baada ya kukubali nkikaa nae kidogo nachoka na naachana nao.

- Mara nyingne Ni muongeaji Sana kwa watu nisiowajua ama ninaowajua ila wakati mwingne nakuwa mkimya Sana naweza maliza muda sijaongea na mtu

- Sinaga aibu.

- Napenda Sana kuishi/kukaa pekeangu pekeangu muda mwingne natamani dunia nzima ningebaki mwenyewe.

- Nina huruma Sana.

- Sipendi sehemu zenye starehe starehe (hii sjui kutokana na malezi) mf birthday party izi ama sehemu za kuchanganyika na watu, napenda Mambo ya fujofujo.

- Nikimbembeleza mtu au mpenzi wangu roho inaniuma Sana najiona Kama sjui Nini yaani kiufupi sipendi maswala ya kubembelezana (ata Mimi sipendi kubembelezwa.

- Napenda Sana uadui na pia kuwa kwenye mazingira magumu(waga ninakuwaga na mawazo Sana ) na bila kuwa na mawazo sifanyagi vitu vizuri(malezi nilokulia).

- Sipendi kufatilia mtu na Mimi sipendi kufatiliwa Mambo yangu.

- Story zangu waga haziko romantic napenda story za matukio matukio ya ajabu na ya kiume sinaga story za kuvutia za mapenzi

Hayo ni machache tu, je me ni mtu wa aina gani maana yake nashindwa kuelewa! Msaada tafadhali🙏
Dalili zote unaonyesha upo katika Kundi la Wagonjwa wa Akili na unahitaji Tiba ya haraka sana.
 
Diazepam

Senior Member
Dec 3, 2020
145
500
Bro, pole sana
Kwa maelezo yako unashida ya akili yaani mental illness,

Kama hutojali tutajie tatizo lilianza lini , sasa hivi una umri gani?
Uliwahi kuwa na tabia ya kubishana na mzazi,walimu au wakubwa zako? Wakati wa utoto ulikuwa ukipigana na wenzio mara kwa mara shuleni?
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
7,037
2,000
Kwa maelezo yako,wewe utakuwa
1. Kijana wa kiume
2. Umri wako ni kati ya miaka 22-32
3. Kuna matatizo ya kisaikolojia unayo baada ya aidha kunyanyaswa utotoni kwa kuonewa, kunajisiwa, kupigwa au kuteswa. Hivyo una hasira ya ndani kwa ndani kwa uliyotendewa
4. Kiasili wewe ni mtu mpole, lakin kutokana na uliyotendewa utotoni unaona kama kuwa 'mpole' ni unyonge, au kutulia ni uoga. Hivyo unapenda 'ujipapatue' kuwa wewe si mnyonge tena na ni 'mpambanaji' hiyo inapelekea wewe kuwa mkorofi.
5. Una restlessness na upweke ndani yako ambayo inakufanya upende uwe kwenye mikusanyiko ya watu na kwenye kelele. Ili kukufanya usiyawaze yaliyokupata huko siku za nyuma.
Kwa kuhitimisha you are troubled person deep inside. Una matatizo ya kisaikolojia. Inawezekana ulikuwaga bullied ulipokuwa mdogo. Ndo maana unashindwa kujitambua wewe ni nani. Maana wewe deep inside ni mtu mzuri, lakin uliyopitia yamekufanya uwe mkorofi ili usiwe mnyonge tena.
 
Wanama

Senior Member
Jun 12, 2021
138
250

Tatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida gani na mamangu lakini hawakunionyesha uungwana ata kidogo walinitenga Sana ata kuingia majumbani mwao ilikuwa shida walinizuia ama wakiniruhusu waliniweka pekeangu chini Apo ndo mwanzo wangu wa kuanza kujitenga ila nilitamani kukaa na watu

Tabia ya kubishana na wazazi na wakubwa ilianza miaka ya baadae kidogo na sikuishia kubishana nao ata kupigana nao ingali nilikuwa mdogo hii ilitokana na tabia ya wao kupenda kunipiga piga ovyo

Mashuleni na mtaani Hali ilikuwa ivo ivo(siyo walimu Wala wanafunzi nilipigana nao) ile Hali ya kutengwa tengwa ilikaa akilini na nilikuwa najihisi Mimi sina faida yoyote kwa mtu yyte na ata mtu akinialika kwenda kwao au kwenye sherehe yoyote sikwenda niliona Hawa wanaenda kunitenga

Yapo mengi Sana ila ayo Ni machache zaidi ukitaka mengine ntaongeza.
 
Umri Ni 20,s, wewe umeweza kunijua zamani nilinyanyaswa Sana kuanzia level ya familia mpk mtaani kwaivyo niliona Mimi si kitu make mtu akinifanya kitu Sina pa kwenda kushtaki ivyo nilijitahidi kupambna mwenyewe ata watu wazima waliponionea nilijaribu kulipiza kisasi na Kama akinikamata kwa Mara ya pili na Mimi nililipiza kwa kuharibu kitu chake Cha maana nayeye haumie kama Mimi.

Nishawai pia kuishi mtaani & kulala kwenye majengo mabovu na vibanda

Siku za nyuma pia nilishajaribu kujiua

Ayo machache mengine ukitaka pia ntaeleza naomba msaada wa mawazo ya Nini Cha kufanya
 
Diazepam

Senior Member
Dec 3, 2020
145
500
Tatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida
Pole sana mkuu, tafuta muda uende hospital yoyote ya magonjwa ya akili.

Kwa maelezo yako machache ulipokuwa utotoni ulikuwa unaelekea kupata(au ulipata) baadhi ya mgonjwa ya disruptive impulse-control and conduct disorders. Ambayo baadhi yake huwa yanaishia kumfanya mtu awe psychopathy ukubwani.

Nenda hospital utafanikiwa kwa sababu tayari ushajua tatizo lako
 
Shukrani mkuu nitafanyia kazi ushauri wako
 
Buti la mkoloni

Senior Member
Oct 20, 2019
167
500
Wewe ni kichaa ni vema ukawai kwenda hospitalini mapema angali bado unajitambua ukichelewa sana utaokota makopo. Hakuna binadam timamu mwenye characteristics za hvyo
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
7,037
2,000
Umri Ni 20,s, wewe umeweza kunijua zamani nilinyanyaswa Sana kuanzia level ya familia mpk mtaani kwaivyo niliona Mimi si kitu make mtu akinifanya kitu Sina pa kwenda kushtaki ivyo nilijitahidi kupambna mwenyewe ata watu wazima waliponionea nilijaribu kulipiza kisasi na Kama akinikamata kwa Mara ya pili na Mimi nililipiza kwa kuharibu kitu chake Cha maana nayeye haumie kama Mimi.

Nishawai pia kuishi mtaani & kulala kwenye majengo mabovu na vibanda

Siku za nyuma pia nilishajaribu kujiua

Ayo machache mengine ukitaka pia ntaeleza naomba msaada wa mawazo ya Nini Cha kufanya
Sasa hapo Mwamba tulia..ya zamani yamepita. Sasa hivi wewe ni dume,na kwa uliyoyapitia umeshakomaa kwelikweli. Hakuna mtu anaweza kukufanya kitu chochote.

Sasa jambo la kufanya hapo kwanza anza kufikiria zaidi maisha ya kesho na sio yaliyopita. Waza kutafuta hela zaidi, kama hujaenda shule angalia namna ya kuingia kwenye biashara za mitumba nk, au kama huna mtaji nenda kajitose kwenye migodi ya dhahabu nk.

Achana na mawazo ya kujiua. Miaka hii mitano iliyopita ilikuwa migumu sana kwasababu ya aina ya kiongozi tuliekuwa nae, alikuwa hovyo, alikuwa hajali kuhusu maendeleo ya watu,yeye alijali maendeleo ya vitu. Ndo maana maisha yalikuwa magumu kwa kila mtu,hasa kwa vijana wanaoanza maisha. Waliona kama maisha yenyewe ndo hivi hakuna kutoboa Bora nife tu.

Lakin kwasisi ambao tumeishapitia maisha tofauti,ninakuhakikishia baada ya mwaka mzunguko wa hela utarudi vizuri tu na utaona unaanza kuishi maisha mazuri tu ya kawaida. Kitu unatakiwa ujue kuwa hii hali ngumu iliyopo sasaiv haikusababishwa na wewe " kwa ujinga wako" au "kutokuwa na bahati kwako" Bali sera mbovu za kiongozi wa nchi. Mambo yanaenda kubadilika soon. Kaza mwanangu
 
Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
7,037
2,000
Shukrani mkuu nitafanyia kazi ushauri wako
Pia puuzia humu wengine wanaokuita majina ya ajabu kama kichaa, mwehu, mwendawazimu nk. Wengi wao wanaokuita hivyo wao ndo vichaa. Tena kama humu JF yamejaa machizi. Unaweza shangaa mtu anakutukana bila sababu. Achana nao. Ukiweza pata muda unaweza kwenda kumtafuta mtaalamu wa mambo ya saikolojia mkae nae mzungumze
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
24,245
2,000
Tatizo lilianza miaka mingi iliyopita baada ya wazazi kutengana Sasa mimi sikujua majirani walikuwa na shida gani na mamangu lakini hawakunionyesha uungwana ata kidogo walinitenga Sana ata kuingia majumbani mwao ilikuwa shida walinizuia ama wakiniruhusu waliniweka pekeangu chini Apo ndo mwanzo wangu wa kuanza kujitenga ila nilitamani kukaa na watu

Tabia ya kubishana na wazazi na wakubwa ilianza miaka ya baadae kidogo na sikuishia kubishana nao ata kupigana nao ingali nilikuwa mdogo hii ilitokana na tabia ya wao kupenda kunipiga piga ovyo

Mashuleni na mtaani Hali ilikuwa ivo ivo(siyo walimu Wala wanafunzi nilipigana nao) ile Hali ya kutengwa tengwa ilikaa akilini na nilikuwa najihisi Mimi sina faida yoyote kwa mtu yyte na ata mtu akinialika kwenda kwao au kwenye sherehe yoyote sikwenda niliona Hawa wanaenda kunitenga

Yapo mengi Sana ila ayo Ni machache zaidi ukitaka mengine ntaongeza.
Duuuh hii hali imewakumba wengi sana abusive....usijione uko peke yako

Kikubwa piga chini past..deal na present na future, badilisha fikra hii itakusaidia sana mkuu, pole
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
11,910
2,000
Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;

- Mimi ni mkorofi (tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari)

- Mimi ni mkimya (yaani sipendi kuongea na pia sipendi mtu aniongeleshe kwa muda mrefu nachukia sana yaani natak nikiwa na wewe ukae kimya usiniulze maswali mengi)

- Ninapenda kampani au watu wasio wapole wapole yaani napenda watu waliochangamka(wahuni wahuni)

- Nayachukia mahusiano(ya kimapenzi) naweza kumtongoza msichana ila baada ya kukubali nkikaa nae kidogo nachoka na naachana nao.

- Mara nyingne Ni muongeaji Sana kwa watu nisiowajua ama ninaowajua ila wakati mwingne nakuwa mkimya Sana naweza maliza muda sijaongea na mtu

- Sinaga aibu.

- Napenda Sana kuishi/kukaa pekeangu pekeangu muda mwingne natamani dunia nzima ningebaki mwenyewe.

- Nina huruma Sana.

- Sipendi sehemu zenye starehe starehe (hii sjui kutokana na malezi) mf birthday party izi ama sehemu za kuchanganyika na watu, napenda Mambo ya fujofujo.

- Nikimbembeleza mtu au mpenzi wangu roho inaniuma Sana najiona Kama sjui Nini yaani kiufupi sipendi maswala ya kubembelezana (ata Mimi sipendi kubembelezwa.

- Napenda Sana uadui na pia kuwa kwenye mazingira magumu(waga ninakuwaga na mawazo Sana ) na bila kuwa na mawazo sifanyagi vitu vizuri(malezi nilokulia).

- Sipendi kufatilia mtu na Mimi sipendi kufatiliwa Mambo yangu.

- Story zangu waga haziko romantic napenda story za matukio matukio ya ajabu na ya kiume sinaga story za kuvutia za mapenzi

Hayo ni machache tu, je me ni mtu wa aina gani maana yake nashindwa kuelewa! Msaada tafadhali🙏
Contradictions mwanzo mwisho

Wewe ni not either of all those mentioned
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
11,910
2,000
Duuuh hii hali imewakumba wengi sana abusive....usijione uko peke yangu

Kikubwa piga chini past..deal na present na future, badilisha fikra hii itakusaidia sana mkuu, pole
Screenshot 2021-04-20 at 18.44.16.png
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom