Naomba kujua mimi ni kundi gani /mtu wa aina gani

Wanama

JF-Expert Member
Jun 12, 2021
277
315
Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;

- Mimi ni mkorofi (tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari)

- Mimi ni mkimya (yaani sipendi kuongea na pia sipendi mtu aniongeleshe kwa muda mrefu nachukia sana yaani natak nikiwa na wewe ukae kimya usiniulze maswali mengi)

- Ninapenda kampani au watu wasio wapole wapole yaani napenda watu waliochangamka(wahuni wahuni)

- Nayachukia mahusiano(ya kimapenzi) naweza kumtongoza msichana ila baada ya kukubali nkikaa nae kidogo nachoka na naachana nao.

- Mara nyingne Ni muongeaji Sana kwa watu nisiowajua ama ninaowajua ila wakati mwingne nakuwa mkimya Sana naweza maliza muda sijaongea na mtu

- Sinaga aibu.

- Napenda Sana kuishi/kukaa pekeangu pekeangu muda mwingne natamani dunia nzima ningebaki mwenyewe.

- Nina huruma Sana.

- Sipendi sehemu zenye starehe starehe (hii sjui kutokana na malezi) mf birthday party izi ama sehemu za kuchanganyika na watu, napenda Mambo ya fujofujo.

- Nikimbembeleza mtu au mpenzi wangu roho inaniuma Sana najiona Kama sjui Nini yaani kiufupi sipendi maswala ya kubembelezana (ata Mimi sipendi kubembelezwa.

- Napenda Sana uadui na pia kuwa kwenye mazingira magumu(waga ninakuwaga na mawazo Sana ) na bila kuwa na mawazo sifanyagi vitu vizuri(malezi nilokulia).

- Sipendi kufatilia mtu na Mimi sipendi kufatiliwa Mambo yangu.

- Story zangu waga haziko romantic napenda story za matukio matukio ya ajabu na ya kiume sinaga story za kuvutia za mapenzi

Hayo ni machache tu, je me ni mtu wa aina gani maana yake nashindwa kuelewa! Msaada tafadhali🙏
 
Naomba kwa wataalamu humu mniambie Mimi ni mtu wa Aina gani kwa izi sifa zangu;

- Mimi ni mkorofi(tokea utotoni napenda Sana ugomvi na sehemu zenye ugomvi na shari).

- Mimi ni mkimya (yaani sipendi kuongea na pia sipendi mtu aniongeleshe kwa muda mrefu nachukia Sana yaani natak nikiwa
Wewe ni mhaya kama sio basi ni mmasai.
 
Wewe ni mtu tu unayetakiwa kuwa shule muda wote. Kama mimi muongo, utakuja kuona matokeo yakitoka.

Kinyume na hapo, basi wewe ni mtu unayetakiwa kuishi jela! Na siyo huku uraiani tuliko sisi. Wewe unatakiwa maisha yako yote kuishi chini ya amri.
 
Swali zuri sana, kiwiliwili cha kuimbe chochote huongozwa na uwepo wa roho ndani yake! Maana yake ni kuwa, bila roho, mwili si chochote! Sasa iko hivi, kuna wakati mwili huongozwa na roho zaidi ya mmoja ndani yake, matokeo yake mtu huyo au kiumbe huyo matendo yake hayatabiriki!

Kuna watu wengi sana waishio kwa kuongozwa na roho wengi ndani yao, roho hao wengi huwa kama jeshi! Roho wanapokuwa wengi zaidi ya kawaida, mtu huyo tunamtaja kama chizi au kichaa maana waongoza mwili ni wengi ndani yake! Ukichunguza utabaini kuwa, kadri ya wingi wa roho ndani yako, mwili wako pia unakuwa thabiti kiafya hata kama utakuwa visivyoeleweka! Vichaa wengi huwezi kuwaona wanaathirika kutokana na vyakula wakulavyo hovyo honyo maana ndani yao ni makazi ya jeshi la Roho wautumiao mwili huo kwa maslahi yao!

Ukubali usikubali, kwangu wewe nakutaja kama mtu unayeongozwa na zaidi ya Roho mmoja! Hii ni kutokana na maelezo yako hapo juu! ukitaka msaada ili ufanye nini, nitakuelekeza cha kufanya nikijua umri wako maana kuna wakati umri ukiwa umekwenda sana, hiyo tunaita tumechelewa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom