Naomba kujua mchango wa Wamisionari katika maendeleo ya elimu Afrika

I LOVE GIRLS

JF-Expert Member
Nov 17, 2020
857
1,320
Assalam allaykum wakuu,

Naomba kujua mchango wa wa-missionary katika maendeleo ya elimu Afrika.
 
I Love Girls,
Nakuwekea hapo chini niliyoandika kuhusu Wamishionari na Elimu kama nilivyoeleza katika kitabu changu, ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'' (1989).

Nimehariri hapa na pale kidogo ili msomaji aelewe somo tunalojadili:

''
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini. Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ''Washenzi' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake za ndani ya madrasa.

Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.

Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888 - 1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya iliyokuwa inatolewa na Wamishionaro katika kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza.

Wengi wanaamini kuwa kanisa kuwa lenyewe ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madrasa na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madrasa.''

Ok...kama kweli ilikomeshwa, elimu ya kiarabu ilirudi lini na kwa njia ipi maana madrasa mpaka leo waislam wanasoma
 
Nashukuru sana Mr Mohamed
 
Ok...kama kweli ilikomeshwa, elimu ya kiarabu ilirudi lini na kwa njia ipi maana madrasa mpaka leo waislam wanasoma
Kilambi...
Madrasa kama taasisi ya elimu hapo ikawa ndiyo mwisho wake kufundisha zilr zinaitwa 3Rs yaani, Writing, Reading and Arithmetic.

Hizi zikawa sasa zinahodhiwa na shule zilizokuwa zinajengwa na Wamishionari.

Madrasa ikabaki kusomesha Islamics.
Ndiyo hizi madrasa unazoziona leo.
 
Wakuu,
Bila ya kukwaza, Kwanini msiseme tu Kati ya dini ya kikristo na ya kiislamu nani alichangia elimu Afrika? badala yake mnaanza na kuchonganisha, mkumbuke pia kuwa sio kweli kuwa Waafrika hawakuwa na elimu na hilo nitakubaliana, lakini pia ikumbukwe kuwa Waafrika nao walitoa elimu ya juu ambayo waislamu na wamishionari walichoma moto egypt?
Tuepushe upotoshi, tuepushe unyanyapaa, tuepushe...
 
Syllo...
Afrika ilikuwa chini ya ukoloni kwa hiyo Waafrika hawakuwa na uwezo wa kujenga taasisi zao za elimu zilizokuwa nje ya mfumo wa wakoloni na wamishionari.

Elimu ikahodhiwa na wakoloni wakishirikiana na wamishionari na ili Mwafrika aweze kupata elimu kwanza lazima akubali kubatizwa awe Mkristo ndipo asome.

Huu ulikuwa mtihani mkubwa kwa Waislamu.

Waislam wa Tanganyika wakaamua kujenga shule zao zikiitwa Muslim Schools.

Moja ambayo mimi najua historia yake ni shule ya Al Jamiatul Islamiyya ambayo ilijengwa mwaka wa 1933 na viongozi Waislam waliounda African Association mwaka wa 1929 Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Jumbe Kiro kwa kuwataja wachache.

Hii ndiyo shule aliyosoma baba yangu pamoja na Abdul na Ally Sykes na watoto wengine wa Dar es Salaam.

Hii African Association ndiyo iliyokuja kuunda TANU mwaka wa 1954 chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.
 
..kwa kiwango kikubwa mkoloni aliwaachia Wamisionari jukumu la kutoa elimu.

..kwa hiyo it is obvious kwamba ili Mwafrika apate elimu ya Mmisionari ilikuwa ni lazima abatizwe.

..naamini ilikuwa hivyohivyo kwa shule za Waislamu kwamba ili wakupe elimu lazima uwe Usilimu.

..au nasema uongo ndugu zangu?
 
JK,
Wakristo hawakuwa na shida ya kwenda kusoma shule ya Waislam na kwa sababu nyingi.

Shule za Wamishionari zikipata Grant in Aid, yaani fedha za kuendesha na kujenga shule wakati shule za Waislam zilinyimwa msaada huu.

Shule za Wamishionari zilikuwa shule bora sana ukilinganisha na shule za Waislam.
 
..tuwe wakweli.

..hizi dini mbili zina upinzani wa jadi.

..Mkristo anaona raha sana kumbadilisha dini Muislamu kuliko Mpagani.

..Na Muislamu anaona fahari kwelikweli Mkristo anaposilimu kuliko Mpagani anaposilimu.

..Kwa hiyo mimi siamini kabisa kwamba shule za Kidini [ Kiislamu / Kikristo ] hazikuwa na ubaguzi wa aina yoyote ktk kutoa elimu.

..Ni kweli mkoloni alikuwa akitoa grant kwa shule za makanisa, lakini pia hakutoa kwa makanisa yote. Kwa mfano, kuna maeneo ambayo kulikuwa na wamisionari wa Kijerumani na walianzisha shule lakini alipoingia Muingereza alikamata Wamisionari hao na shule zao zikasambaratika.
 
Kutumia neno "upinzani," ni tatizo kidogo katika Uislam hali kadhalika "ubaguzi."

Lakini ili uyajue haya utahitaji ufahamishwe nini Qur'an inasema na mimi sipendi mjadala wa namna hii.
 
Mzee usichoke kuzishauri shule za kiislamu na madrasa, zisipuuzie elimu dunia, Dunia ya sasa imebadilika sana, Teknolojia inatawala, kama hutakua na elimu dunia basi kila siku utabaki kulaumu kuwa unaonewa, utabaki kulaumu maisha ya zamani wakati hata hivi sasa una-nafasi ya kubadilisha maisha yako.
Elimu ya quran haina tija kwa ulimwengu wa telnolojia kwa sasa..Ova.
 
Bhachu,
Sijui ni kipi kimekufanya wewe udhani kuwa Waislam wanapuuza elimu.
Msingi wa elimu katika Pwani ya Afrika Mashariki uliwekwa na Waislam.

Wamishionari mfano wa Johann Krapf amefika kwa Chief Kimweri miaka ya katikati 1800 amemkuta Kimweri anajua kusoma kuandika na hesabu na herufi zilizokuwa zikitumika ni za Kiarabu.

Ukoloni ukapiga marufuku herufi za Kiarabu na kulazimisha ziktumika za Kirumi.
Wakoloni wakishirikiana na Wamishionari wakajenga shule na kuweka sharti la kubatizwa kwa kupata elimu.

Waislam wakajenga shule zao wakiziita Muslim School ili waelimike.

Harakati za kupigania uhuru zikaongozwa na Waislam kwa kutaka kuondoa kila aina ya dhulma zilizokuwapo Tanganyika.

Uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 mwaka wa 1962 Waislam wakaitisha Muslim Congress agenda ikiwa Elimu.

Azimio lililopitishwa ni kuwa Waislam wajenge shule kika mkoa na pia wajenga Chuo Kikuu.
Jiwe la msingi likawekwa na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1968.

Juhudi hizi za Waislam katika elimu hazikuwapendeza walioshika serikali na hujuma ikafanyika na East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa inajenga Chuo Kikuu ikapigwa marufuku na serikali ikaunda BAKWATA.

Yapo mengi.

Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (IOC) ilitaka kujenga Chuo Kikuu Cha Kiislam Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali na chuo hicho kikajengwa Mbale Uganda.

Kumekuwa na malalamiko kuwa kuna hujuma kubwa dhidi ya Waislam NECTA na Wizara ya Elimu.

Mwaka wa 2012 palifanyika maandamano ya kulaani hujuma ya NECTA dhidi ya shule za Waislam.

Waislam hatujapuuza elimu.
 
Syllo...
Afrika ilikuwa chini ya ukoloni kwa hiyo Waafrika hawakuwa na uwezo wa kujenga taasisi zao za elimu zilizokuwa nje ya mfumo wa wakoloni na wamishionari.

Elimu ikahodhiwa na wakoloni wakishirikiana na wamishionari na ili Mwafrika aweze kupata elimu kwanza lazima akubali kubatizwa awe Mkristo ndipo asome.

Huu ulikuwa mtihani mkubwa kwa Waislamu.

Waislam wa Tanganyika wakaamua kujenga shule zao zikiitwa Muslim Schools.

Moja ambayo mimi najua historia yake ni shule ya Al Jamiatul Islamiyya ambayo ilijengwa mwaka wa 1933 na viongozi Waislam waliounda African Association mwaka wa 1929 Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ali Jumbe Kiro kwa kuwataja wachache.

Hii ndiyo shule aliyosoma baba yangu pamoja na Abdul na Ally Sykes na watoto wengine wa Dar es Salaam.

Hii African Association ndiyo iliyokuja kuunda TANU mwaka wa 1954 chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.
Mkuu,
Kuna nadharia inayojengeka kwa makusudi, ya kuwa Mwafrika hakuwa na elimu yeyote ile! Yaani ni mbumbumbu na hata u bin adam hana.

Vile vile, kumekuwa na upotoshaji wa kina katika dini kuu mbili, yaani wakristo na waislam kuhusu jinsi ya walivyowakuta wazawa na watu wa maeneo ya mwaafrika.

Mkuu, tukubaliane kwa hayo, tukubaliane pia walitukuta tukiwa na elimu, ujuzi uliotukuta, na uwezo wa kufanya biashara, kupigana vita;unahitaji hisabati fulani, pamoja na utengenezaji wa silaha pia
...Mkuu sipingi utumiaji wa herufi na maendeleo ya kisayansi yaliyowezeshwa na uislamu, vile vile sipingi maendeleo ya bin adam kwa dini zote mbili, yote yana mafundisho mazuri tu lakini watu ambao walitumia na bado wanatumia kulete mfarakanyo na hisia mbaya kati wale ambao siyo wafuasi wa dini hizi sitokubalina nao na wanajulikana

Najaribu kutojihusisha na siasa za "wale" "nyinyi watu"
wakati naona unataka kuhusisha jamii nzima ya waafrika walikuwa waislamu.

Mkuu, tukiweka dini pembeni Jibu kwa aliyeuliza swali litakuwa rahisi
 
Syll...
Sina tatizo na fikra zako nimesoma na nimekuelewa na mimi nimekueleza elimu kama ilivyo katika jamii moja na kubwa Tanganyika.

Nimekueleza historia ya jamii hii kwa miaka mingi hadi kufika kwa Wamishionari na Ukoloni.

Ningeweza nikakueleza baada ya uhuru nini kilitokea.

Naamini huna historia ya Muslim Congress mbili ya 1962 na 1963 mikutano iliyojadili elimu kwa Waislam ili kujiondoa katika ile hali iliyotamalaki Tanganyika wakati wa ukoloni.

Naamini huna historia ya mapambano ya chini kwa chini yaliyozuka baada ya Congress ya 1963.

Naamini hujui mgogoro mkubwa uliozuka 1968 Waislam walipoweka jiwe la msingi kujenga Chuo Kikuu pale Chang'ombe.

Mgogoro huu ukadababisha EAMWS wajenzi wa Chuo Kikuu kuvunjwa na kuundwa BAKWATA.

Hapa.kuna historia ya kusisimua.

Naamini huelewi mengi katika Wizara ya Elimu, Baraza la Mitihani nk. nk. kuhusu Waislam wala huna taarifa ya Kitwana Kondo Bungeni Dodoma 1999 alipotahadharisha serikali kuhusu uchaguzi wa wanafunzi kuingia sekondari uchaguzi ulioelemea waumini wa dini moja.

Lakini naamini ulisoma katika magazeti na kusikia katika tv na radio kuwa Waislam walifanya maandamano bila kibali dhidi ya Baraza la Mitihani.

Hii ilikuwa mwaka wa 2012.

Uzuri wa mijadala kama hii ni hii fursa ya kuelimishana.

Ndugu yangu kwa kutojua historia ya Waislam na elimu kaandika hapa akituhimiza Waislam tutie bidii katika suala la elimu tuache Qur'an kwani haina nafasi katika dunia ya leo.

Huwa sikasiriki na kejeli kama hizi.

Kwangu mimi huwa nimepewa fursa kuelimisha jamii kama hivi.

Jambo la kusikitisha ni kuwa wanaostahili kutoa majibu huwa kimya kwa kuhofia kuwa suala hili ni nyeti mno.

Wanaotoa majibu ni watu ambao tatizo hili wao linawanufaisha.

Hawa wao ni raia hawana dhima ya kuwajibu Waislam.
 
Bhachu,
Sijui ni kipi kimekufanya wewe udhani kuwa Waislam wanapuuza elimu.
Msingi wa elimu katika Pwani ya Afrika Mashariki uliwekwa na Waislam.

Wamishionari mfano wa Johann Krapf amefika kwa Chief Kimweri miaka ya katikati 1800 amemkuta Kimweri anajua kusoma kuandika na hesabu na herufi zilizokuwa zikitumika ni za Kiarabu.

Ukoloni ukapiga marufuku herufi za Kiarabu na kulazimisha ziktumika za Kirumi.
Wakoloni wakishirikiana na Wamishionari wakajenga shule na kuweka sharti la kubatizwa kwa kupata elimu.

Waislam wakajenga shule zao wakiziita Muslim School ili waelimike.

Harakati za kupigania uhuru zikaongozwa na Waislam kwa kutaka kuondoa kila aina ya dhulma zilizokuwapo Tanganyika.

Uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 mwaka wa 1962 Waislam wakaitisha Muslim Congress agenda ikiwa Elimu.

Azimio lililopitishwa ni kuwa Waislam wajenge shule kika mkoa na pia wajenga Chuo Kikuu.
Jiwe la msingi likawekwa na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1968.

Juhudi hizi za Waislam katika elimu hazikuwapendeza walioshika serikali na hujuma ikafanyika na East African Muslim Welfare Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa inajenga Chuo Kikuu ikapigwa marufuku na serikali ikaunda BAKWATA.

Yapo mengi.

Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (IOC) ilitaka kujenga Chuo Kikuu Cha Kiislam Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali na chuo hicho kikajengwa Mbale Uganda.

Kumekuwa na malalamiko kuwa kuna hujuma kubwa dhidi ya Waislam NECTA na Wizara ya Elimu.

Mwaka wa 2012 palifanyika maandamano ya kulaani hujuma ya NECTA dhidi ya shule za Waislam.

Waislam hatujapuuza elimu.
Waislamu hawajapuuza elimu, hili ni kweli. Kinachogombewa ni sawa tu nz maongezi ya siku hizi kuwa haiwatayarishi vijana kujitegemea, inawadumiza kusubiri wapewe kazi, walishwe na kuhudumiwa. Wamisionari wameleta shule zao watu wamesoma bila ubaguzi (soma kwanza, batizwa baadaye, shule za waislami ni za waislam zilifundisha uislamu).

Kumbuka kuwa Tanganyika haijawahi kuwa nchi ya Waislamu, wala ya Wakristo, hii ilikuwa nchi ya Wapagani. Sensa 1965 ilikuta Wapagani 35% Wauslamu 33% Wakristu 31%. Ukihesabu leo (Nyerere alifuta) utakuta Waislamu bado ni 33% lskini Wapagani wamebaki 20% (sanasana Serengeti, Usukunani na Wakinga).

Nitajie shule za Waislamu zilizoelimisha Watanganyika? Hakuna, labda utaje za Aga Khan (Usagara, Tambaza, Kisutu, lakini hizi zilikuwa hazifundishi uislam). Na Wamisionari? St Francis (Pugu), St Michael & St George (Mkwawa), Rosary College (Ngaza), Marian College (Kilakala) hizi zinewasonesha "wapagani".

Kusifia Wamisionari si kudogosha Waislam, kila mmoja alifanya alichoweza Inshaallah.

Umemtaja Aga Khan na EAMWS hapo ni manati yenyewe. Soma kitabu cha Abdulwaheed Sykes mtunzi Mohamed Said. Soma kile cha Kiingereza kimeelezea vizuri (cha Kiswahili kilichakachuliwa kwenye translation baada ya mwandishi kuwa siasa kali ). Itoshe tu kuwa makao makuu ya EAMWS yalikuwa Nairobi, (kusiko na Waislamu) na CEO wake alikuwa Mhasibu (CPA, si Imam). Kazi yake kuu ilikuwa ni kutunza biashara za Aga Khan (Riddoch Motors, Motor Mart, Landrover, Sugar Plantations).

EAMWS kilikataliwa na wazee wetu Waislam masheikh, kupitia baraza la Ulamaa na Viongozi wetu naarufu wakiwamo Rashidi Kawawa, Abedi Karume, Adam Naseeb, Hamis Masasi, Ali Bawazir, na wengineo wengi. Wakaanzisha BAKWATA, kwani ulishwahi kusikua BAKWAKE hadi leo? Kwa nini walimkataa Aga Khan? Alitaka kuivunja Tanganyika kwa udini kama alivyoibomoa India na Pakistan akaanzisha chama kinaitwa AMNUT (All Muslim National Union of Tanganyika) kuipinga TANU (Tanganyika African National Union).

Haya yote soma kitabu cha Mohamed Said, kipo wanauza pale Faya.

Nikutakie Mwaka Mpya lakini umechagua ajenda dhaifu.
 
LGF,
Unazungumza jambo usilolijua.

EAMWS leo tena si muhimu kwa Waislam ila kueleza ule ukweli kuwa ilikuwa inajenga Chuo Kikuu na hili halikutakiwa ndiyo yakapitishwa yaligopita.
 
Back
Top Bottom