JK
BAKWATA ni katika matatizo makubwa waliyopata kukutananayo Waislam wa Tanzania.
Kwa zaidi ya nusu karne Waislam wamekataa kuikubali BAKWATA kama taasisi yao.
Naamini hili si jambo geni kwako lazima utakuwa unalijua na kwa nini wameikataa naamini sababu unazijua.
Kwa ajili hii basi Waislam wamejiweka mbai sana na BAKWATA.
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 vijana wa Kiislam kupitia taasisi ya Warsha waliweza kujipenyeza katika uongozi wa BAKWATA kwa nia ya kuboresha shule zake, Kinondoni, Kibohehe na Jumuiya kwa kuzigeuza kuwa Seminari za Kiislam.
Shule hizi zilibadilika na kwa mara ya kwanza matokeo ya mitihani ilitia fora.
Pamoja na mabadiliko haya Warsha iliandika waraka kwa Waislam wa Tanzania kuonyesha hali yao ya elimu toka uhuru mwaka wa 1961.
Serikali ilikuwa inashutumiwa kwa kukosa uadilifu.
Waraka huu ulishtua si serikali peke yake bali hata Waislam wenyewe.
Hii ilikuwa mwaka wa 1981.
BAKWATA ikajikuta inagongana na serikali iliyounda taasisi hiyo.
Vijana wa WARSHA waliokuwa BAKWATA wakafukuzwa BAKWATA pamoja na Katibu Mkuu wa wakati ule Sheikh Mohamed Ali.
Kosa lao likiwa kuliweka jambo nyeti hadharani.
Ninakuandikia kwa kifupi kwani ni kisa kirefu.
Kuanzia wakati huo hadi hivi sasa Waislam wanajitahidi kujenga shule zao nje ya BAKWATA na kujiletea maendeleo yao hawajishughulishi na BAKWATA kwa jambo lolote sababu kubwa ni kuwa taasisi hiyo haikuasisiwa na wao wenyewe Waislam bali na serikali mwaka wa 1968.
..nimesoma historia uliyoandika kuhusu kuanzishwa kwa Bakwata.
..hata nikikubaliana na wewe 100% bado inaniumiza kuona sekondari za Bakwata zikifanya vibaya.
..na waathirika wa sekondari za Bakwata ni watoto wa imani mbalimbali, lakini mostly ni watoto wa Kiislamu.
..kwanini Waislamu msiungane ktk suala hili la ELIMU na hayo mengine mkayashughulikia baadae?
..Na ukichunguza Waislamu ni matajiri wakubwa hapa nchini, sasa inakuwaje shule za taasisi ya Kiislamu iliyopo nchi nzima kama Bakwata zikatelekezwa kiasi hiki?
..Mimi nawashauri muungane mrekebishe madhaifu yaliyoko ktk sekondari za Bakwata.