Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,857
- 30,205
Kinyungu,Endelea naye. Ni kwa faida yetu sote.
Hujanijibu swali shule ya Kiislam uliyoitaja iko wapi? Hakuna hata masalia ya majengo yake?
Shule ipi?
Kinyungu,Endelea naye. Ni kwa faida yetu sote.
Hujanijibu swali shule ya Kiislam uliyoitaja iko wapi? Hakuna hata masalia ya majengo yake?
Kinyungu,Hiyo shule iko wapo kwa sasa? Au ilikuwa eneo gani?
Tutajie jina la hilo jengo.Kinyungu,
Shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilijengwa kuanzia mwaka wa 1933 ilipoasisiwa taasisi yenyenyewe.
Waasisi wakiwa Mzee bin Sudi President, Kleist Sykes Secretary pamoja Ali Jumbe Kiro na wazee wengine wa Dar es Salaam.
Hawa wote walikuwa viongozi pia katika African Association.
Mwaka wa 1936 Aga Khan alitembelea Tanganyika na akakaribishwa kuitembelea shule hii.
Mwanafunzi aliyesoma risala ya kumkaribisha Aga Khan alikuwa Abdul Sykes.
Baba yangu na watoto wengi wa miaka ile walisoma shule hii.
Aga Khan akachangia fedha shule ikamilishwe na likajengwa jengo ambalo lipo hadi leo Mtaa wa Makisi Mbwana na Lumumba Avenue.
Serikali ilipovunja EAMWS na kuunda BAKWATA mwaka wa 1968 shule hii ikaangukia mikononi kwa BAKWATA na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mali zote za Waislam.
Hii shule imebadilishwa jina inaitwa Lumumba.
Waislam wameomba warudishiwe jengo lao na shule lakini hadi leo hawajafanikiwa.
Naingia Maktaba kukutafutia picha.
Sorry sijaelewa ni wapi? Au unamanaisha hii hapa kwenye makutano ya Mkunguni na Lumumba ave? Mbele yake kidogo penye Shopping Mall kubwa ambayo nasikia majengo ni ya Bakwata?Kinyungu,
Shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilijengwa kuanzia mwaka wa 1933 ilipoasisiwa taasisi yenyenyewe.
Waasisi wakiwa Mzee bin Sudi President, Kleist Sykes Secretary pamoja Ali Jumbe Kiro na wazee wengine wa Dar es Salaam.
Hawa wote walikuwa viongozi pia katika African Association.
Mwaka wa 1936 Aga Khan alitembelea Tanganyika na akakaribishwa kuitembelea shule hii.
Mwanafunzi aliyesoma risala ya kumkaribisha Aga Khan alikuwa Abdul Sykes.
Baba yangu na watoto wengi wa miaka ile walisoma shule hii.
Aga Khan akachangia fedha shule ikamilishwe na likajengwa jengo ambalo lipo hadi leo Mtaa wa Makisi Mbwana na Lumumba Avenue.
Serikali ilipovunja EAMWS na kuunda BAKWATA mwaka wa 1968 shule hii ikaangukia mikononi kwa BAKWATA na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mali zote za Waislam.
Hii shule imebadilishwa jina inaitwa Lumumba.
Waislam wameomba warudishiwe jengo lao na shule lakini hadi leo hawajafanikiwa.
Naingia Maktaba kukutafutia picha.
Kinyungu,Sorry sijaelewa ni wapi? Au unamanaisha hii hapa kwenye makutano ya Mkunguni na Lumumba ave? Mbele yake kidogo penye Shopping Mall kubwa ambayo nasikia majengo ni ya Bakwata?
Don't be daft. Chuo Kikuu cha Waislamu kimejengwa na Benjamin William Mkapa, Mkiristo, kawanyanganyaTANESCO shule ymao ya Engineering pale Msanvu Morogoto. Naona wewe ni mbux3 hujui mambo. Njoo ofisini pale Faya nitakupa kitabu cha Mohamed Said. Unajua Kiingrezq? Kinaitwa THE LIFE AND TIMES OF ABDUKWZHEED SYKES. Kinaeleza jinsi gani Agha Khan alitaka kutuuzia mbuzi guniani kama alivyovunja India na Pakistan ila Wazee wetu Waislamu wakakataa. Hujui historia, kama kimya.
Nipe Dunihaji.
Mkuu,Syll...
Takriban nusu ya umri wangu wa miaka 68 naingia 69 In Shaa Allah Februari nimekuwa nikiandika vitabu, ''academic papers,'' na makala nyingi zisizo na hesabu kuhusu Uislam Tanzania na nimehudhuria mikutano mingi ndani na nje ya Tanzania pamoja na kuzungumza katika vyuo mbalimbali Afrika, Ulaya na Marekani.
Naweza kujidai kuwa suala hili nalijua kwa kiasi changu.
Katika ujuzi huu kuna namna ya ''pattern,'' nimejenga na kwa sasa naweza kusema imekuwa sawasawa na sheria au kanuni ya aina fulani mfano wa ''Archimedes Principle.''
Mfano ni kama huu wako.
Unapoona mtu anaandika kwa staili yako kuwa liko tatizo na linajadiliwa na mtu anaandika kwa kusema kama unavyosema wewe kuwa huwajuia Waislam, Waarabu, Wakristo, Waafrika, Wamishionari nk; huyu tafuta imani yake utakuta si Muislam.
Sasa utafiti wangu haukuishia hapa ili niweze kuitengeneza hii sheria yangu au kanuni iweze kuwa na mashiko ni lazima nijue kiwango cha elimu yake.
Nitakijuaje?
Huwa namtia hamu ya kufanya majadala na mimi na kila anapoandika najaribu kupima kiwango cha elimu yake na si kazi kubwa mara moja naweza kukisia kama ni elimu ya chini, kati au juu.
Hapa nitaeleza jambo.
Uzoefu wangu unaonesha kuwa baadhi katika mjadala huu wa dhulma huwa wanapandwa na hamaki kwa kukosa hoja na huja na lugha kali na pengine matusi na vitisho au kunishambulia binafsi badala ya kujibu hoja.
Lakini haya yote yamesaidia sana katika kuelewa uzito wa suala hili.
Suala linalofuatia ni kwa nini ghafla baada ya kujua uwezo wake kuwa kiwango chake cha elimu ni kizuri anaandika kama mtu asiyejua kitu?
Sasa ili kupata ''conclusion,'' au uhakika wa kile ninachotafuta ni lazima hii ''pattern'' yangu iwe na ''sampling,'' kubwa yaani nimejadiliana na watu wengi katika jamii katika tatizo hili.
Nilichogundua ni kuwa imani ina nafasi kubwa sana katika fikra kiasi anaona kukubali ukweli anaowekewa wazi ni kushindwa kwa imani yake.
Hiki ni kitu muhali mkubwa sana kwake hawezi kukiruhusu.
Sasa ukichukua ukweli huu ukauweka katika serikali ambayo watendaji wakuu wanaoshika nafasi za maamuzi ni wa imani moja kwa mathalan uwiano wa 20:80 utaelewa bila tabu yote kwa nini hali iko hivyo ilivyo kuwa Waislam wanajaribu kueleza matatizo yao lakini hakuna aliye tayari katika serikali kusikiliza au hata kuamini kuwa liko tatizo.
Hapa ndipo linapoingia lile suala linalotisha.
Ni akina nani waliotoa uamuzi wa kuvunjwa kwa EAMWS wakati wanajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 na kutekeleza mipango yao ya elimu?
Nini lilikuwa kusudio lao?
Hofu kuwa Waislam wataelimika na hivyo kushika madaraka katika serikali ya Tanganyika huru?
Ndiyo hapo ghafla unasoma mtu kama Edwayne anaandika kuwa Uislam na Ukristo zote ni dini za shetani na utumwa.
Tafuta imani yake utapata jibu.
Lakini ukiangalia mjadala si huo bali ni dhulma ambayo Waislam wanaeleza serikali kuwa wamekuwa wanafanyiwa toka uhuru upatikane mwaka wa 1961 na vielelezo vyote kama ushahidi wameweka.
Nachelea kumchosha msomaji lakini mifano ipo mingi.
Tatizo ni kuwa viongozi wetu hawako tayari kuliweka tatizo hili katika agenda lijadiiwe kwa wazi kwa hofu ambayo si tabu kuitambua.