Naomba kujua maana ya kukuwa kwa uchumi

NOT ENOUGH

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
596
307
Nina elimu ya certificate katika mambo ya Hoteli hivyo uwelewa wangu ni mdogo katika maswala ya uchumi. Nasikiaga mara kwa mara viongozi wakiongea kwenye hotuba zao kwamba uchumi umekuwa/umeshuka labda kwa asilimia kadha wa kadha.

Mara ya mwisho nilimsikia Mh Raisi akiongea kwenye hotuba yake ya salamu za mwaka mpya kwamba uchumi wetu umekua kwa 8% kama sikosei.

Sasa mimi sijui ni vigezo gani wanatumia kusema uchumi umekua au umeshuka. Kwa uwelewa wangu nisikia uchumi umekua mara moja naanza kufikiria maisha yanayo nizunguka hivyo naangalia unga sasa bei gani, sukari, petrol, mkate, nauli, ada za shule na kadhalika.

Je vigezo nitumiavyo mimi ni sahihi au si sahihi? Naombeni nifahamu itanisaidia.
 
Ni kuongezeka kwa uwekezaji kama dowans,ongezeko la taasisi za fedha ,ongezeko la pengo kati ya wakesha hoi na mafisadi,kukua kwa wafisadi!...jk
 
Back
Top Bottom