Naomba kujua kwanini toka rais wa marekani achaguliwe mpaka kuapishwa inachukua zaidi ya miezi 3?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Wadau naomba kujua kwani nini inachukuwa karibu miezi 3 kwa Rais wa Marekani toka achaguliwe mpaka kuapishwa kwake? Je kuna taratibu gani zinazofanyika mpaka zinapelekea kuchukuwa muda huo?
 
Kwan wa Tz anachukua muda gan kuapishwa?.
Kama hapa bongo nchi inachukua mwezi na siku kadhaa ajabu nini kwa marekani kuchukua miezi 3?
 
Wadau naomba kujua kwani nini inachukuwa karibu miezi 3 kwa Rais wa Marekani toka achaguliwe mpaka kuapishwa kwake? Je kuna taratibu gani zinazofanyika mpaka zinapelekea kuchukuwa muda huo?
Katiba ya The United States of America ndivyo inavyosema. Sababu ni kuwapa muda wa kutosha kwa Rais anayemaliza muda wake kukamilisha kazi na kuweza kukabidhi kazi kwa Rais anayefuata.
Pia ningependa kukusahihisha kuwa si kweli kuwa ni miezi mitatu. Ni takriban miezi miwili kuanzia mwezi November wanapopiga kura mpaka tarehe 21 Januari Rais mpya anapoapishwa.
 
Yaan nadhani huwa huo muda wanawapa cancelling maana trump hapo tu amefanyiwa cancelling hivi kama angekuwa hajafanyiwa angemuovertake hata yule kichaa aliyejitangaza
 
Wakati huo hukumika kukabidhiana ofisi kama katiba yao inavosema, pia kuna waraka ambao Raisi aliyemaliza muda wake huainisha matatizo, changamoto, fursa na maswala mbalimbali kwa mtazamo wake na kumkabidhi hyo Raisi aliyechaguliwa. Kwa ujumla Marekani wanaamini kua Uraisi ni cheo kikubwa sana hvyo huwezi kukabidhi Ofice hyo kwa muda mfupi na pia lazima upikwe kisaikolojia na uelezwe namna mbalimbali ya kupata msaada kwa mambo ambayo huyafahamu. Mengine wadau wanaendelea kutiririka
 
Pia wanatoa room ya muda wa kukata rufaa kwa yule ambaye hajarizika na matokeo, hapa kwetu uchaguzi wa rais haupingwi mahakamani na akishatangazwa basi imetoka hiyo, huku kwetu kuna utapeli furani wawazi kabisa, na ndio wako faster kumuapisha ili yeye mwenyewe aulinde urais wake iwe hata kwa kumwaga damu.
 
Huwa tunampeleka kozi fupi ya urais. Anapata intelligence briefings za rais, anajipanga kuteua timu yake, anakamilisha miamala kwa michepuko na kadhalika.
Kiranga, hivi lakini huyu Rais wenu wa sasa ni yeye ndio anamatatizo au ni haw wanasiasa wengine? sijwahi ona Rais anasumbuliwa kama huyu toka nizaliwe
 
Kuna tatizo la kufikiri mtu mmoja ndiye ana matatizo.

Nitatoa mfano. Nilikuwa nashangaa sana imekuwaje nchi iliyokuwa na wasomi wengi na maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia kama Ujerumani ( wasomi wengi walioendeleza sayansi Marekani, kina Einstein, walitoka Ujerumani) iliweza kupumbazwa na kushikiwa akili na mtu mmoja aliyeitwa Adolf Hitler.

Baada ya kusoma vitabu kama "The Rise and Fall of The Third Reich: A History of Nazi Germany" cha William Shirer na "The Origins of the Final Solution: The Evolution of Nazi Jewish Policy, September 1939-March 1942"
cha Christopher Browning, nikagundua kwamba, Hitler hakuwahadaa Wajerumani, Wajerumani ndio waliomtengeneza Hitler. Kulikuwa na watu wabaguzi wengi tu katika jamii ya Ujerumani tangu kabla ya enzi za Chancellor Bismark.

Kwa nini natoa mfano huu?

Jamii ya Kimarekani imegawanyika.

Marekani imepunguza ushawishi wake kimataifa kwa sababu nchi nyingine zinaibuka kiuchumi na kutoitegemea sana Marekani. Ukisoma kitabu cha Fareed Zakaria, columnist wa Washington Post na mtangazaji wa a CNN weeekly show, kitabu kinaitwa "The Post American World" utaona kaandika vizuri hili. Ona wiki page hapa

Pia, ndani ya Marekani kwenyewe, "wazungu" wanapoteza nguvu yao kama majority, sasa hivi watu walioitwa "ethnic minorities" kama weusi na Hispanics wanatarajiwa kuzidi watu weupe katika miongo michache ijayo.

Masuala kama uhamiaji na trade tariffs, ambayo watu wengi hawayajui vizuri, yanamfanya Trump aonekane ndiye mtu sahihi. Kwa sababu anafikiri kizamani na anatoa sound bites ambazo watu wengi wanazifurahia.

Kuna mambo mengi sana, lakini, hii si vita ya Trump na wanasiasa wapinzani wake. Trump ana wafuasi wengi sana wanaomuunga mkono. Ndiyo maana anapata kichwa na kusema anaweza kumpiga mtu risasi katikati ya New York City, halafu wafuasi wake wakaendelea kumuunga mkono. Sasa rais gani anasema maneno kama hayo?

Kuna watu walikuwa wanafanya kazi kwenye viwanda, wamepoteza kazi zao, kwa sababu imekuwa rahisi kutengeneza vitu China. Wafanyakazi wa Marekani tuna gharama sana. Nilikuwa nasoma jana jinsi raia wa Uingereza walivyokuwa wanashangaa kuona gharama za huduma za afya Marekani. Zamani watu walikuwa wanaweza kusima mpaka sekindari tu, bika kwenda chuo, halafu wakapata kazi za "blue collar", kazi zisizohitaji usomi sana hususan za viwandani, halafu wakalipwa vizuri tu. Mfani ni viwanda vya magari vilivyokuwa Detroit. Siku hizi hakuna, moaka Detroit umekuwa ni mji wenye nyumba zisizo na watu. Kuna sehemu unaweza kununua nyumba kwa USD 1. Dola moja. Watu wamekimbia. Detroit Motown palitingusha dunia, no more.

Pia, kijamii kuna watu wa red states (majimbo ya wahafidhina) hawapendi nchi inavyoendeshwa na watu wa blue states (majimbo ya waliberali). Kwenye mambo kama kuruhusu ushoga, kujiingiza sana katika mambo ya nje, kuruhusu mashirika ya kimataifa kama UN kuingikia nguvu za Marekani etc. Haya mambo mengine yamekuwapi miaka mingi sana. Hili ka UN kwa mfano lipo tangu UN inaanzishwa. Rais Woodrow Wilson alipata upinzani sana kuhusu kuanzishwa kwa League if Nations, a predecessor of the UN.

Trump mwenyewe naye kichaa. Yani kabla hajamaliza scandal moja, anajianzishia nyingine. Wakati watu wanasoma Mueller Report, wanakuja kukuta kumbe alikuwa anamlazimisha rais mpya wa Ukraine amshurumu mtoto wa mpinzani wake, Makamu wa Rais aliyepita, Joe Biden.

Wakati watu wanagundua alitaka kutumia msaada wa dola za Kimarekani milioni 400 kwa Ukraine kumlazimisha rais wa Ukraine kumshutumu mtoto wa Biden, Trump anaenda kwenye TV na kuitaka China imchunguze Biden, kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya uongozi, kwa sababu anataka nchi ya nje iingikie uchaguzi wa Marekani.

Habebeki. Hata mtu angetaka kumezea mambo ya Mueller report, anakuja na scandal mpya kila siku. Na watetezi wake wanamtetea. Kwa sababu hawajali mambo kwa mantiki ya kupima kwa kina, wanakwenda kwa husia na kuona huyu ndiye mtu wetu wa kurmturudishia viwanda.

To "Make America Great Again".

Even as the cost of production of manufactured goods in America is ridiculously unrealistic.

Kwa hiyo, Trump ni kichaa na anastahili yote yanayompata. In fact hakustahili kuwa rais.

Lakini, anapewa kichwa na Wamarekani wengi sana wanaoona anachofanya ni sawa.
 
Mimi naona Trump kaja muda sahihi kusaidia baadhi ya mambo ya USA, na sioni kama kuna mtu wa Democrat wa kumshinda katika uchaguzi wa 2020, Waafidhina wanaona ndo mtu sahihi wa kupambana na China, lakini kinachomshinda katika mapambano na Uchina ni Matajiri wenzie na hata yeye kawekeza China kwahiyo vita inakuwa ngumu kuishinda, kwa upande wa Urusi naiona ikiimeza Ulaya haswa kwa kuizuia gesi na rasilimali zingine ambazo wanazihitaji EU. Trump alichoepuka ni vita ambayo ingeshusha hadhi ya uchumi wa USA pamoja na Saudia kujifanya atafadhili lakini Trump katumia busara sana kutopigana na Iran.

Sasa mtu sahihi wa kupambana na China halafu na yeye kawekeza China, hapo inakuwaje?

Trump anafanya vita kisiasa tu. Anajua kwamba, hawezi kurudisha manufacturing Marekani.

Marekani gharama za bima ya afya za mwezi mmoja tu zinaweza kulipa mshahara wa Mchina kwa mwaka mzima.

Sasa hapo utashindanaje na Mchina?
 
Nimekuelewa, kwa namna Marekani ilivyokuwa msingi wa elimu na ustaarabu duniani, Trump sio tatizo ni wamarekani wenyewe. they should have known him better.

sasa hili la gharama za bidhaa, huduma na uzalishaji kuwa kubwa sana marekani, ni nani analipia hizi gharama?
kuna namna yoyote mnatunyonya labda?
 
Mimi naona Trump kaja muda sahihi kusaidia baadhi ya mambo ya USA, na sioni kama kuna mtu wa Democrat wa kumshinda katika uchaguzi wa 2020, Waafidhina wanaona ndo mtu sahihi wa kupambana na China, lakini kinachomshinda katika mapambano na Uchina ni Matajiri wenzie na hata yeye kawekeza China kwahiyo vita inakuwa ngumu kuishinda, kwa upande wa Urusi naiona ikiimeza Ulaya haswa kwa kuizuia gesi na rasilimali zingine ambazo wanazihitaji EU. Trump alichoepuka ni vita ambayo ingeshusha hadhi ya uchumi wa USA pamoja na Saudia kujifanya atafadhili lakini Trump katumia busara sana kutopigana na Iran.

Ikitokea CHINA ikakubali kwa mfano ku implement mabadiriko anayoyataka trump kwenye mambo yafuatayo.
1. Intellectual property
2. Kuruhusu makampuni ya marekani kuwekeza China bila kulazimishwa kushirikiana na makapuni ya kichina.

Trump na Marekani wanakuwa wameshinda trade war.
 
Sasa mtu sahihi wa kupambana na China halafu na yeye kawekeza China, hapo inakuwaje?

Trump anafanya vita kisiasa tu. Anajua kwamba, hawezi kurudisha manufacturing Marekani.

Marekani gharama za bima ya afya za mwezi mmoja tu zinaweza kulipa mshahara wa Mchina kwa mwaka mzima.

Sasa hapo utashindanaje na Mchina?
Nyie wenyewe mnaomshangalia mko tayari kufanya kazi za shuruba kama wachina?
 
Back
Top Bottom