Naomba kujua kuhusu safari ya Dar kwenda Dodoma kwa pikipiki

Kaluluma

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
454
584
Habari za leo wakuu,

Ninafikiria kati ya njia mbili za kusafiri, aidha kwa pikipiki au kuisafirisha chombo yangu used kwa malori ya mizigo. Kwa wale wenye uzoefu na route hii kwa pikipiki mnaweza kunipa muongozo wa sehemu za kupumzika, kufanya service nikiwa njiani, muda wa safari kwa makadirio na changamoto zilizopo barabara hiyo ya Dar - Dodoma.

Chombo ni mbili moja boxer cc125, na Tvs cc 150 madereva tupo wawili.

Natanguliza shukrani.
 
Safirisha kwa lori.

Au endesha kama una mtu wa kukuuguza KCMC / Muhimbili mwaka mzima. Kumbuka hii ni Tanzania, barabara nyembamba jumlisha jeuri na dharau za madereva wa magari.

Jirani yangu safari ya Dar-Dom iliishia pale Chalinze, tulizika bila hata kuaga.
 
cha kwanza angalia gharama ya mafuta kutoka dar dom utatumia shi ngap!!na ghrama ya kusafilisha halafu compair uone!!. ila safal dar dom karibu tu mkuu unafika fresh bila shaka kabisa,, cha mhimu ni kuwa na mavaz mazur kudhibit upepo!!mm mwenyewe usafili wang ni pikpik naenda mikoan bila shida kabisa huu mwaka wa nne sasa,

nakumbuka siku natoka tanga to musoma bila shaka nilifika fresh tu,, musoma to bukoba bila shida, mwanza kigoma bila shida na morogoro to chato na ninatumia tvs 150* ko usiogope cha mihimu hasa ni mavaz unayovaa,, kwanza ni usafili usiokuwa na vituo ving.
Nb; miaka 2 nyuma nilikuwa natumia honda sport cc 200, badae nilinunua tvs 150 ndo natumia toka 2020 january... mafuta kibaba.
 
cha kwanza angalia gharama ya mafuta kutoka dar dom utatumia shi ngap!!na ghrama ya kusafilisha halafu compair uone!!. ila safal dar dom karibu tu mkuu unafika fresh bila shaka kabisa,, cha mhimu ni kuwa na mavaz mazur kudhibit upepo!!mm mwenyewe usafili wang ni pikpik naenda mikoan bila shida kabisa huu mwaka wa nne sasa,,nakumbuka siku natoka tanga to musoma bila shaka nilifika fresh tu,, musoma to bukoba bila shida, mwanza kigoma bila shida na morogoro to chato na ninatumia tvs 150* ko usiogope cha mihimu hasa ni mavaz unayovaa,, kwanza ni usafili usiokuwa na vituo ving.
Morogoro to chato ulitumia siku ngapi
 
Kwanza tujue.

1. Dar dom km ngapi
2. Unaenda kwa km ngapi kwa saa
3. Lita inakupeleka km ngapi
4. Je una vifaa vya kujikinga, koti, helmet nk
5. Je una tool box
6. Una pesa ya dharura.

Inawezekana kabisa. Wanaokutisha hata pikipiki hawajui kuendesha. Jipange, inawezekana.
Asante mkuu kwa kunitia moyo
 
Back
Top Bottom