Naomba kujua kuhusu njia sahihi ya kutumia kufanya uamuzi juu ya uchaguzi wa hisa za kununua

The smartest

New Member
Sep 5, 2017
2
0
Habarini za kwenu wadau wa masuala ya stocks. Naomba kujua juu ya ukweli kuhusu method sahihi ya kutumia kufanya uamuzi juu ya uchaguzi wa hisa za kununua sokoni kati ya fundamental analysis method na technical analysis method hasa katika soko letu la hisa la DSE.
 
as a trader mi naona ujue zote tuu maana hamna namna sasa.
 
kimsingi nimefanya baadhi ya literature review juu ya hii issue na bado naendelea nayo, ila inaonekana ni methods mbili zilizo na mitazamo miwili tofauti na kila njia ikiwa na advocates wake. Ila pia wapo wanatetea kuwa investor anaweza kutumia njia zote mbili kwa wakati mmoja. Naomba kama kuna watu ambao watakuwa tayari kufanya literature reviews kuhusu hii mambo na later on tuje kudiscuss hapa itakuwa ni njema kwa ajili yetu na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Stock market kwa maana ya DSE ni moja ya platform muhimu kwa sasa kwa issue za uwekezaji. hivyo kuwa na maarifa yake kunafungua milango ya fursa ya kutengeneza faida.
 
Hali ya soko la hisa Tanzania kwa sasa hivi ni tete.
Kabla hujafanya hiyo 'fundamental analysis method au technical analysis method' ni vizuri kwanza uanze kujifunza 'from basic'
Mambo unayopaswa kutilia maanani ni kama haya:


- Jielimishe kuhusu kampuni mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye platform ya Dar-es-salaam Stock Exchange(DSE)
- Angalia uongozi wake na jinsi zinavyoendeshwa
- Nini wanazalisha
- Mapato (profits)

- Soma charts zao uone jinsi thamani ya hisa zake zinavyokwenda

Kwenye link hii chini nimeweka mfano wa hisa za CRDB. Hapo utaona jinsi zilivyopanda na kuchuka kwa kipindi cha
January 13 hadi January 17:
Company | Dar es Salaam Stock Exchange PLC
Kwa kuiga mfano huu unaweza ukacheki makampuni mengine yaliyoorodheshwa.
 
Back
Top Bottom