Naomba kujua kuhusu déjà vu

wakuu,m nna story ndef kdogo lakin niseme tu mamb mengi nayopitia now nlishawah kuyaota ktambo mengne toka o level huko ni ktambo,ila bado mengne meng nayasubir yatokee,lakn vile vile nna kawaida km nikiota ndoto nzur kesho yak tukio baya utokea,km ndoto ni mbaya kesho lazma ntoboe sana,na km nmeonda alaf kesho yasitokee bas yao unikutaga mbelen tna huwaga mambo mazur,baada ya kujiona iv mwenyewe nkajipeleka kwenye meditation ,n hayo tu wakuu
naomba unielekeze jinsi ya kufanya meditation au kuna sehem watu wana fanya meditation mkuu
 
Wakuu hapa kuna vitu tunajichanganya...De javu na Telepathy ni vitu viwili tofauti..
Kwa kifupi, de javu ni ile hali ambapo unaona hali au mazingira na ubongo wako unajaribu kukumbusha (recalling/re-fetching memories) ya jambo au mazingira hayo na kisha kuikosa !!!! Unapoikosa sasa ndipo hali halisi ya mazingira inapojitokeza unahis kama ulishawai kuiona..HIKI HUWA KITENDO CHA KASI SANA KIASI CHINI YA NUKTA 0.1
(Kama nmekuacha uliza)
sijaelewa mkuu
 
mkuu kama umeajiriwa, na unakatwa ile 18%

acha kazi maana njia yako umeshaiona

uwe mtabiri utapiga pesa mingi sana,

trust me, maana na mimi nilishakuonea hii ninayokwambia
naanzaje kua mtabiri? nifafanulie vizuri nielewe
 
Sijui aisee kama ndio deja vu au laa. Ila niliwahi kusoma humu uzi wa @Pasco kuhusu Psychic Powers ambazo kila mtu anazo tangu utoto ila huwa zinapungua/zinazidiana kadri ubongo unavyozidi kujaa mambo mengi ya nje. Tafuta huo uzi utaelewa zaidi.

Hilo suala la kumkumbuka mtu then ukamuona siku hiyo pia ni uwezo wa akili sjui niite ni connection kati ya mtu na mtu ila kwa mimi ilikuwa inanitokea kwa jamaa yangu mmoja tu ambaye nimekaa nae kwa muda wa miaka mitatu ila sikuwahi kujua anapokaa na ilikuwa nikimuuliza hataki kusema.

Huyu jamaa ilikuwa siku nikimuwaza au kumkumbuka ni lazma siku hiyo nionane nae. Lakini baadae nikaja kujua kuwa hakuwa binadam.

By the way tafuta huo uzi wa @Pasco.

Shukran.
Hii story yako pia ianzishie uzi mkuu, jamaa alikuwa nani? na ulijuaje? alikuwa mwema au mbaya kwako?
Karibu
 
Hii story yako pia ianzishie uzi mkuu, jamaa alikuwa nani? na ulijuaje? alikuwa mwema au mbaya kwako?
Karibu

Jamaa alikuwa ni mwema tu japo aliwahi kuniambia kuwa ametumwa na wakubwa wake aje kunichukua anipeleke ujinini ila anashindwa coz kuna nguvu zinanilinda hivyo anashindwa kunichukua.

Ikamlazimu yeye kushindwa kutimiza hilo jambo na akawa anaogopa kurudi ujinini bila ya kurudi na kile alichoagizwa (MIMI).

Mpaka kulala nae nlikuwa nalala nae usiku mambo nliyokuwa nikiyaona acha tu. Majini bwana wana vituko sana.
 
Basi ni sawa wakuu ntalifanyia kazi hili wazo wandugu.

Ila kiukweli hawa viumbe tunapishana nao sana mitaani na haya mambo yapo wakuu.

Tuko pamoja wandugu.

Thanks.
Na mimi unitag mkuu.
 
Sijui aisee kama ndio deja vu au laa. Ila niliwahi kusoma humu uzi wa @Pasco kuhusu Psychic Powers ambazo kila mtu anazo tangu utoto ila huwa zinapungua/zinazidiana kadri ubongo unavyozidi kujaa mambo mengi ya nje. Tafuta huo uzi utaelewa zaidi.

Hilo suala la kumkumbuka mtu then ukamuona siku hiyo pia ni uwezo wa akili sjui niite ni connection kati ya mtu na mtu ila kwa mimi ilikuwa inanitokea kwa jamaa yangu mmoja tu ambaye nimekaa nae kwa muda wa miaka mitatu ila sikuwahi kujua anapokaa na ilikuwa nikimuuliza hataki kusema.

Huyu jamaa ilikuwa siku nikimuwaza au kumkumbuka ni lazma siku hiyo nionane nae. Lakini baadae nikaja kujua kuwa hakuwa binadam.

By the way tafuta huo uzi wa @Pasco.

Shukran.
Mkuu naomba utupe japo kahistoria flan hiv kuhusu huyo jamaa yako wa ajabu kwan mlikutana katika mazingira gani na ilikuwaje ukajua kama sio binadamu?
 
Mkuu, huyu jamaa nilikutana nae maeneo ya Kinondoni mitaa ya studio.

Nilikuwa na baadhi ya jamaa tukiwa tunakunywa ili kuweka kichwa sawa na kuchangamsha mwili kiasi. Ndipo akaja mtu mmoja akatueleza hapo barabarani kuna mwarabu mmoja hatumuelewi elewi tukimuuliza haongei chochote ndipo nikasema acha niende. Kufika tu nikaanza kumsemesha akawa ananijibu.

Nikamshawishi tuondoke na kwenda kwenye kikao chetu ili kujua kama nae anakunywa au laa. Kufika eneo la kilaji jamaa ikawa haongei na yoyote zaidi yangu.

Aisee, ni story ndefu wakuu ila mambo yaliyonitokea kipindi chote ambacho tupo wote ndio yaliyopelekea kujua kuwa hakuwa binadam.

Natumai nimejibu maswali yako mkuu.

Shukran.
inaonekana ni story nuri sana embu mkuu fikiria namna ya kuiandika tupate faida kidogo

mana kusoma icho kipande tuu nimekuw na maswali kama buku ivi kichwani mwangu

fanya ivyo mkuu
 
Mkuu naomba utupe japo kahistoria flan hiv kuhusu huyo jamaa yako wa ajabu kwan mlikutana katika mazingira gani na ilikuwaje ukajua kama sio binadamu?

Mkuu jinsi nilivyokutana nae mbona nimeeleza hapo nyuma na pia jinsi nlivyokuwa nikiishi nae yale matukio na vituko alivyokuwa akivifanya ndio vilinifanya nijue kuwa sio binadam.

Soma post #51 ameni-quote themanhimself nimeeleza jinsi nilivyokutana nae mkuu.

Thanks.
 
Habari zenu .....
Wanajamvi naomba kujua sababu ya kuona vitu au siku zinajirudia yani naweza kukaa siku nikaona kama matukio yanajirudia Yan nikaona kama hiyo siku nilishawahi kuiona na kufanya hayo mambo yanayotendeka kwa muda huo....

Pia naweza kuwa nimemkumbuka mtu halafu namuona hata kama hatujaonana siku au muda mrefu au naweza kuhisi mtu fulani atanipigia simu na anapiga simu siku hiyo .Je hii ndo de javu au kuna kitu kingine.
Ndio yenyewe.
 
Basi ni sawa wakuu ntalifanyia kazi hili wazo wandugu.

Ila kiukweli hawa viumbe tunapishana nao sana mitaani na haya mambo yapo wakuu.

Tuko pamoja wandugu.

Thanks.
Ukifungua uzi fanya kunitag mkuu
 
Hii ni hali inayo mtokea mtu pale ubongo unapofeli kutafsiri muda halisi wa tukio. i.e; present event is interpreted as past event

Cc: Jimena
 
DE JA VU NI NINI?

De Ja Vu ni hali ya kiasili kabisa na ya kiuwezo wa pekee inayomtokea Kiumbe cha Mungu na ni hali ya kufahamu yanayomtokea mbeleni, au muda mfupi ujao kwa kurecall hali hiyohiyo iliyowahi kumtokea kipindi flan katika maisha yake na akairecord katika kumbukumbu bila kujua hiyo siku itajirudi baadaye maishani.

Pasco alieleza vizuri kwa kiasi chake.

Kiimani ama kiroho, hali hiyo hiyo ndiyo itakayomtokea mtu kabla ya kufa kwake kwa kukumbushwa kwa kuona kabisa yaliyotokea maishani mwake tangu kuzaliwa kwake ila hatakuwa na uwezo kwa kuzungumza.

Hali nyingine itakayomtokea mtu ni ile ya sleeping paralysis.
kuna mambo mnayazungumza naona kama yanaukweli ndani yake kwaupande wangu kuna mambo nimesha yazoea sana sasa mfano kila nikipata tatizo lolote liwe kujibizana au hata ugonvi lazima jana yake nitakuwa naota nafukuzwa na simba au namfukuza paka nimesha zoea kujua kesho yangu kama kutakua na tatizo sasa kibaya zaidi mtu nikimuwaza sana au kumkumbuka lazima siku hiyo nimuone japo historia yangu ina utata kidigo kuna wakati sasa hata tukiwa wawili tukiwa umenyamaza ikitokea tu nimewaza wimbo flani basi wewe utaimba kwawakati huo kwakifupi nimekua ni mtu wamachale machale mfano kila ninapo ota ndoto za kutisha mfano kuona baazi ya ngugu ambao wamesha tangulia mbele za haki mfano hasa babu yangu lazima kesho nipate pesa kwa njia yoyote ila sasa huyu babu alitokea kunipenda utotoni na alinitabilia mambo kuhusu maisha yangu ambayo 80% nikweli yanatimia ila alikuwa ni mtemi huko kijijini unyamwezini hebu nisaidieni au kunamambo alinifanyia au ni karama niliyo pewa namungu
 
Mkuu hali hiyo ni bahati sana na inawatokea wachache sana, pia wala hauhusiani na uchawi kama wengi wanavyofikiri ila ni namna ambavyo mwenyezi Mungu anawasiliana nawewe kwa kukuonesha ya mbeleni.

Biblia inasema wazee wenu wataoteshwa ndoto na vijana wenu wataona maono.

Halafu kuhusu hiyo ndoto ni ndoto zenye maana na inahitaji tafsiri tu...na kwa waombaji hasa wanajua maana zake.

Mfano ndoto ambayo ni common kwa watu wengi ni hizi:-

1) Kuota kufukuzwa na ng'ombe mkubwa mwenye mapembe

2) Kuota kudumbukia katika shimo refuuu ila hufiki chini.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom