Naomba kujua kazi ya msemaji wa Jeshi la polisi

accused

JF-Expert Member
Aug 7, 2015
2,496
2,743
Nimekua nikijiuliza siku nyingi kuhusu wadhifa wa SSP Advera Senso.

Natambua cheo chake ni msemaji wa jeshi letu la polisi, ila sijuagi majukumu yake hasa ni nini ,na sababu zangu za kutokutambua ni hizi:

Kila kunakotokea tukio lolote ndani ya mkoa wowote wanaotoa matamshi ni makamanda wa mikoa. So wasemaji wanakua wao.

Hata kwa kanda maalum ya Dar, Mara nyingi anaetoa matamko ni Kamanda Sirro, SSP Advera utamsikia akitoa matamko kwenye issue chache sana.

Kuna wakati ule wa CP Kova, kwa wengine walidhani kabisa yeye ndiye msemaji wa jeshi maana kila siku alikua na Vyombo vya habari.

Naomba kwa wanaojua watujuze ni nini kikomo cha Msemaji wa Jeshi hili na ni wakati gani anatakiwa yeye kuzungumza.

Nawakilisha.
 
Makamanda wenye uelewa na hilo jambo watalitolea ufafanuzi
 
Polisi kuna pande mbili, kuna cheo na madaraka ni vitu viwili tofauti. Kwa maana hiyo basi, usemaji sio cheo, vyeo ni vile vinavyotamkwa kama coplo, segeenti,na kuendelea. Madaraka ni kama station sagenti, mkuu wa kituo (OCD) na kuendelea, usemaji hata kwanye madaraka sidhani kama inaingia, naona hawa ni wanahabari ndaji ya jeshi la polisi, na huwa wamesomea, kazi zao ni kutoa habari, zinazohusu jeshi la polisi, nimejalibu kukuweka sawa ila kuna wajuzi zaidi na mambo ya polisi wanaweza kuja kuweka sawa hili.
 
Nashukuru, though we need to get down in it

Sasa kwanini hafanyagi hivyo? Chukulia mfano wizarani na mashirika mengine ya Uma like Dawasco,Tanesco n.k, wakiwa na lakusema sikuzote huja Msemaji alieajiriwa kwa cheo hicho.
Kulisemea jeshi la polisi.
 
Anasemea matukio ya kitaifa au matukio makubwa ya uhalifu ....matukio mengine wanayo mamlaka ma RPC mikoa husika...ukitaka kila tukio alisemeeee nchini...aiseee waandishi mtakuwa hambanduki MAKAO makuu ya jeshi
 
Polisi wana "divisions" nyingi na tofauti kiutendaji na kimawasiliano, hivyo msemaji kama huyo atashindwa ku-coordinate habari za kutoka sehemu hizo zote.

Hivyo ni sawa kuwaachia makamanda kuwa ndio wasemaji wakuu kwani wao ndio wanaoandaa na kutekeleza "operations" zilizo katika maeneo yao.

Msemaji wa Polisi kama huyo mama yupo kwa ajili ya masuala ya PR na ya kitaifa zaidi ambayo yanatoka makao makuu kwa IGP.

Pia wizara ya mambo ya ndani inacho kitengo cha mawasiliano ya serikali ambapo kunakuwa na mtiririko na mtawanyo wa taarifa na mawasiliano baina ya serikali kuu, IGP na wizara.

Nafikiri utaelewa kuwa kabla ya agizo la kufuta mikutano jana ni lazima kulikuwepo na mkutano wa dharura wa IGP, RPCs , waziri au naibu au katibu mkuu.

Au IGP Mangu na RPCs na wasaidizi wao.
 
Mimi siyo mwandishi mkuu. Ni karaia tu
Anasemea matukio ya kitaifa au matukio makubwa ya uhalifu ....matukio mengine wanayo mamlaka ma RPC mikoa husika...ukitaka kila tukio alisemeeee nchini...aiseee waandishi mtakuwa hambanduki MAKAO makuu ya jeshi
 
Nashukuru kwa elimu kiongozi
Polisi wana "divisions" nyingi na tofauti kiutendaji na kimawasiliano, hivyo msemaji kama huyo atashindwa ku-coordinate habari za kutoka sehemu hizo zote.

Hivyo ni sawa kuwaachia makamanda kuwa ndio wasemaji wakuu kwani wao ndio wanaoandaa na kutekeleza "operations" zilizo katika maeneo yao.

Msemaji wa Polisi kama huyo mama yupo kwa ajili ya masuala ya PR na ya kitaifa zaidi ambayo yanatoka makao makuu kwa IGP.

Pia wizara ya mambo ya ndani inacho kitengo cha mawasiliano ya serikali ambapo kunakuwa na mtiroroko na mtawanyo wa taarifa na mawasiliano baina ya serikali kuu, IGP na wizara.

Nafikiri utaelewa kuwa kabla ya agizo la kufuta mikutano jana ni lazima kulikuwepo na mkutano wa dharura wa IGP, RPCs , waziri au naibu au katibu mkuu.

Au IGP Mangu na RPCs na wasaidizi wao.
 
Baada ya Mbowe kutoa waraka wake mitandaoni, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, ametoa maoni yafuatayo baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi kuhusiana na waraka huo.

Hiii ni moja ya nukuu yake katika Gazeti hilo:

"Kama wana malalamiko polisi hatupo juu ya sheria,wafuate taratibu na wanaruhusiwa kwenda mahakamani maana huko watapata haki yao,si kutumia mitandao ya kijamii maana huo ni ushamba.Mbowe hajui thamani yake badala ya kutumia mitandao kuhamasisha wafuasi wake kukuza uchumi wa viwanda,yeye anaitumia vibaya," alisema.
 
Back
Top Bottom