Naomba kujua haya kuhusiana na mtoto mchanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kujua haya kuhusiana na mtoto mchanga

Discussion in 'JF Doctor' started by Kichwa Ngumu, Mar 12, 2011.

 1. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Karibu wana JF, namba kujuzwa mambo yafuatayo kuhusiana na mtoto mchanga.
  1. Ni muda gani tangia kuzaliwa anaweza kutoka nje?
  2. Ni muda gani tangia kuzaliwa anaweza kuanza kula chakula kingine zaidi ya maziwa ya mama?
  3. Aogeshwe mara ngapi kwa siku?
  4. Nini kitamtokea mtoto kama nitaanza kufanya mapenzi na mamake baada ya siku arobaini tangia kuzaliwa na kama sita tumia condom?
  5. Na mambo mengine ambayo sijayaorodhesha ila yanaweza kunifaa juu ya mtoto mchanga.
  Natambua wapo watakaosupport na wapo watakaonidis, yote nitayapokea.


  Nawasilisha
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Msindikize mama watoto clinic, utapata majibu ya masuali haya pamoja na ushauri mwingine kwa faida yenu nyote.
   
 3. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama hadi afikishe miaka miwili ila baada ya miezi 6 unaweza kumpa vyakula vingine vilaini laini.
  Anaweza kutoka nje baada ya siku 40.
  Ni vizuri kama mtoto ataogeshwa atleast mara mbili kwa siku ila ikitokea amejinyea muogeshe tena maji ya vuguvugu.
  Kuhusu suala la kufanya mapenzi nasikia kuna kubemenda ni kwamba sperms zinakimbilia kwenye maziwa ya mama na zinadhohofisha virutubisho (naweza kusahihishwa hapo maana sina uelewa wa sana).
  Mengineyo.
  Mtoto asishinde na mikojo, mpe nyonyo mara anapohitaji, asikose klinik, mlinde dhidi ya malaria na magonjwa mengine, awe na vyombo vyake maalum na viwe vinachemshwa, nk..
  Msalimie eeh.
  Mwambie aunt husninyo amempenda ghafla.
   
 5. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo sisi sahihi saaana!!...ingawa waliosema hivo(wakunga wazamani) wamelenga kwenye hili>>>>....... ni kwamba kunauwezekano ukaapata mimba tena na kweli maziwa yakapungua/kuisha/kubadilika kabla mto haja nyonya vya kutosha!!!
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kichwa ngumu we ni mama au baba?
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ahsante kwa kunisahihisha.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  haihusiani. Halafu kumbuka malezi ni ya wote baba na mama.
   
 9. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Baba; wa mtoto mmoja kwa hiyo sina uzoefu wa kulea naogopa kumwalibu mtoto
   
 10. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante, anakupenda pia anaomba umtembelee
   
 11. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nitamtembelea. Ajiandae kunipokea.
   
 13. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Mh id zingine bana, sikuangalia id yake nikajua umeamua kumtusi by da way ataelewa kwa ushauri mliutoa?
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Actually sio vizuri kumuogesha mtoto mchanga kila siku!Mara moja au mbili kwa wiki inatosha!
   
 15. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuanzia kuzaliwa mpaka miezi 6 mtoto anyonye maziwa ya mama yake mzazi tu,,miezi inayofuata ndiyo aanza kupewa vyakula laini laini huku akiendelea kunyonya maziwa ya mama yake....na ni vizuri zaidi siku ya clinic ya mtoto mwende wote baba na mama hospital kumpeleka mtoto ili mkapate kumuuliza maswali yote yanayowasumbua dr wa mtoto........watoto ni baraka ndani ya nyumba hongereni sana.......
   
 16. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu huku unakoelekea utakuja kuzua matatizo na mamake!! LOL
   
 17. TATE

  TATE Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza kumtoa nje siku yoyote haidhuru kitu
   
 18. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mengi yameshajibiwa lakini nami ntapenda kurudia kadhaa na kuafafanua kama nitaweza.
  1. Hakuna muda maalum ambao mtoto anaweza toka nje, anaweza hata kutoka siku ya pili tu baada ya kuzaliwa. Cha muhimu ni kwamba, uwezo wa mtoto kutunza joto ni mdogo (hasa watoto njiti), hivyo ukimtoa nje hakikisha umemvika nguo na kumfunika ili asipoteze joto kabisa.
  2. Mtoto anaweza kula chakula kingine mbali na maziwa ya mama baada ya miezi 6. Maziwa ya mama yana kila kitu mtoto anachohitaji katika miezi sita ya kwanza bila kuongeza chakula chochote. Baada ya miezi sita mtoto aendelee kunyonya mpaka miaka mi2 au zaidi huku akila vyakula mbalimbali vinavyoshauriwa kufuatana na umri wake.
  3. Kuoga ni njia mojawapo ya kupoteza joto la mtoto. Ile siku ya kwanza kuzaliwa inashauriwa hasiogeshwe. Kisha waweza kuendelea kumuosha mtoto (epuka maji mengi) kadri inavyohitajika. Ni vyema kumfuta kwa kitambaa kilicholoweshwa maji ya vugu vugu unapombadili mtoto akijisaidia kuliko kumuogesha kila mara.
  4. Kwa kawaida mwanamke baada ya kujifungua inachukua muda kidogo kurudi kwenye mzunguko wake wa mwezi, hii hucheleweshwa zaidi na kunyonyesha..ndio maana kunyonyesha inachukuliwa kama njia mojawapo ya kupunguza uwezekano wa mimba ya mapema. Ukifanya mapenzi na mama mtoto baada ya siku arobaini ataweza kupata mimba. Akipata mimba mfumo wake wa 'hormoni' hutabadilika na maziwa yatapungua hadi kuisha kabisa, kitu ambacho kinaweza kuathiri afya ya mtoto (ndio wanaita kubemenda, sio kweli manii/mbegu ndio zitamuathiri mtoto kupitia maziwa). Sio mbaya kuanza kufanya mapenzi baada ya arobaini, lakini mtumie 'kondomu' ili kuepusha mimba ya haraka ambayo zaidi ya kuweza kuleta athari kwa mtoto, inamuathiri na mama pia.
  5. Mambo mengine: mpende sana mwanao na mama yake, spend nao time ya kutosha, hii inamsaidia mama kutulia kiakili na kihisia na kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto, shiriki kumhudumia mtoto (kuchange dippers, nepi, etec), cheza na mtoto ujenge bond, and enjoy fatherhood!
   
 19. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante sana mkuu
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Google utapata majibu yote maana hospitali hasa za private wala hawatoi elimu yoyote. Mwanangu nimemlea kwa kutumia internet. Very helpful unaregister then wanakuwa wanaku update tokana na umri wa mwanao.
   
Loading...