Naomba kujua gharama ya kutoa mzigo (incubator) bandarini

nyanda5

Member
Nov 25, 2014
49
40
IMG_3047.JPG

Nimeambatanisha Proforma Invoice. Kwa wale wenye uelewa na mambo ya kuclear mzigo bandarini je, itanigharimu kiasi gani kuutoa mzigo bandarini?? Bado sijailipia nimewasiliana na supplier kwenye alibaba kuwa nitafute kwanza agent nijue gharama za kuutoa mzigo ndio nilipie mzigo utumwe. Asante wadau.
 
Karibu kwetu upate incubator kwa bei ya ofa ya mayai 3,000 full automatic kwa tsh 1,500,000
 
Ni offer chief pay after delivery unapatikana wapi?

Mkuu bei mbona iko chini sana au ndio nanenane, mnapatikana wapi? Mimi niko Tabora napenda kujua namna ya kuipata hiyo mashine na namna ya malipo. Kama itakupendeza naomba tupia picha hapa mkuu.
 
Mkuu bei mbona iko chini sana au ndio nanenane, mnapatikana wapi? Mimi niko Tabora napenda kujua namna ya kuipata hiyo mashine na namna ya malipo. Kama itakupendeza naomba tupia picha hapa mkuu.
Mashine hiyo kwa wakazi wa dar ni free delivery kwa sababu tuna wakala wetu hapo pia kwa tabora tunasafirisha zaidi nipe mawasiliano yako au ni pm
 
View attachment 824321

Nimeambatanisha Proforma Invoice. Kwa wale wenye uelewa na mambo ya kuclear mzigo bandarini je, itanigharimu kiasi gani kuutoa mzigo bandarini?? Bado sijailipia nimewasiliana na supplier kwenye alibaba kuwa nitafute kwanza agent nijue gharama za kuutoa mzigo ndio nilipie mzigo utumwe. Asante wadau.
Gharama za ku-clear incubetor yako bandarini ni kama ifuatavyo;

1.Gharama za wakala wa meli (local shipping line agent/consolidator) haizidi $290 (Delivery Order fee, de-consolidation, sumatra charges, car service charges etc).
2.Gharama za bandari;
a). Handling charges, ambayo rate yake ni $7 plus VAT per CBM (Cubic Measurement yaani Urefu x Upana x Urefu). mfano incubetor ina CBM 1.90, kwa hiyo handling charges: (1.90 x $7) + VAT = $15.694
b). Corridor Levy, ambayo rate yake ni $0.3 plus VAT per CBM, kwa incubetor inakua: (1.90 x $0.3) + VAT =$0.58
c). Wharfage charges, ambayo kwa sasa TRA wanaikusanya kwa niaba ya Bandari, rate ya wharfage ni 1.6% ya C.I.F value. Incubetor ina CIF value $700+10=$710, wharfage charges: ($710 X 1.6%) + VAT =$13.41.
3. Ushuru-TRA:
a) VAT -------18% ya CIF value.
b) Rail Development Levy (RDL)---1.5% ya CIF.
c). Customs Processing Fee (CPF)---0.6%.
Note, Import Duty kwa incubetor ni asilimia sufuri (0%).
4. Mwisho mkuu ni gharama za uwakala (agency fee), kampuni yangu itaku-charge tsh.150,000) na tunapatikana kwa anuani ifuatayo;

S.A Link Traders Ltd (clearing & forwarding company)
2nd Floor-Elite City building (Opposite Harbor View Tower),
Samora Avenue/Morogoro Road,
Dar es Salaam- Tanzania.
Email: info@salink.co.tz
Mob: +255718 866 651 ( Call or Whatsapp )
Website: www.salink.co.tz
Facebook page: S.A LINK Traders LTD
 
Back
Top Bottom