Naomba kujua Faida ya Kimaendeleo kwa nchi hasa pale mara kwa mara Rais wake akiwa anaonyeshwa akiwa Kanisani Ibadani

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Mimi niko hapa Kwetu Malawi ila sijajua kama na nyie huko Kwenu Afrika Mashariki nanyi labda Marais wenu huwa wanapenda mno Kupigwa Picha wakiwa Makanisani au Misikitini kila Siku za Ibada ( Maombi ) za Jumapili na Ijumaa huku wakiwa na Nyuso za Huruma kabisa na kama vile wanajutia Jambo fulani hivi.

Nikiwa kama mwana JamiiForums niishie hapa nchini Malawi kwa mwaka wangu huu wa 23 sasa naomba Kuwaulizeni je kuna Faida yoyote ile ya Kimaendeleo kwa nchi / taifa kama kila mara Rais wa Malawi huyu akiwa anapigwa Picha na zinatumwa Mitandaoni na zingine kutumika Magazetini zikimwonyesha kuwa anasali?

Nitashukuru nikijibiwa na mnasalimiwa mno na wana Malawi hapa niishipo.

Karibuni.
 
Picha husika ziko wapi..ila kwa huku kwetu sisi hua anatafuta huruma ya watu maana hua anajinasibu anamuogopa Mungu wakati vitendo anavyowafanyia binadamu wenzake Mungu mwenyewe hapendi..i.e. kupewa kesi ya uhujumu uchumi wakati uchunguzi haujakamilika
 
Kiongozi uinaposema ' huku Kwetu ' una maanisha kuwa tupo sote hapa Lilongwe nchini Malawi au labda unamsema Rais mwingine wa Taifa lingine? Mimi nilidhani hili Jambo naliona tu hapa nchini Malawi nilipo kwa Rais wetu huyu kumbe yawezekana na Kwingineko nao wanakumbana na Jambo hili hili?
 
Iddi amini akihojiwa na mwandishi wa BBC huku akijifanya kuona aibu amewahi tamka ktk maisha yake hawezi na wala ajawahi kuuwa hata sisimizi.Unaweza ukawa Kanisani kimwili huku roho iko nje kufikiria nimtoe nani kafala Leo ili niridhishe nafsi.
MTU muovu hawezi kuwa na Amani maisha ni na hatoweza ukimbia mkono wa Bwana ataulizwa nipe sensa yangu nilikukabidhi kondoo100 uwachunge mbona wengine siwaoni wako wapi watimie 100.
 
Labda ni utaratibu mpya, sijawahi kuona. Labda soon na Huduma pendwa ya kukata gogo bila shoka nayo itakua "The Deal"
 
Iddi amini akihojiwa na mwandishi wa BBC huku akijifanya kuona aibu amewahi tamka ktk maisha yake hawezi na wala ajawahi kuuwa hata sisimizi.Unaweza ukawa Kanisani kimwili huku roho iko nje kufikiria nimtoe nani kafala Leo ili niridhishe nafsi.
MTU muovu hawezi kuwa na Amani maisha ni na hatoweza ukimbia mkono wa Bwana ataulizwa nipe sensa yangu nilikukabidhi kondoo100 uwachunge mbona wengine siwaoni wako wapi watimie 100.

Kiongozi kwahiyo hapa unataka kusema kwamba kumbe yawezekana huyu Rais wetu hapa nchini Malawi ninapoishi miaka yangu mingi hii akawa ni Mnafiki, Mwongo na Mkatili pengine hata haya Maombi yake huwa yanapokelewa na Shetani pasipo Yeye kujua na akidhani kuwa labda Mwenyezi Mungu ni Mwendawazimu atapokea Dua zake wakati hana hata huo Ucha Mungu ndani ya Roho yake na Moyo wake?

Halafu sijui ni kwanini huyu Rais wa Malawi huwa anapenda sana Kuongozana Kanisani na Mke wa Mwenzake japo kwa mara nyingi huwa anaonekana akiwa pia na Mkewe. Yaani Watanzania mnakosa mno Vituko vya hapa nchini Malawi hasa vya huyu Rais wetu na kheri yenu nyie mliobahatika huko mna Rais ambaye hapendi Kujionyesha au Kuonekana akiabudu na Mpenda Sifa na Makamera kama huyu wetu hapa Malawi.
 
Mimi niko hapa Kwetu Malawi ila sijajua kama na nyie huko Kwenu Afrika Mashariki nanyi labda Marais wenu huwa wanapenda mno Kupigwa Picha wakiwa Makanisani au Misikitini kila Siku za Ibada ( Maombi ) za Jumapili na Ijumaa huku wakiwa na Nyuso za Huruma kabisa na kama vile wanajutia Jambo fulani hivi.

Nikiwa kama mwana JamiiForums niishie hapa nchini Malawi kwa mwaka wangu huu wa 23 sasa naomba Kuwaulizeni je kuna Faida yoyote ile ya Kimaendeleo kwa nchi / taifa kama kila mara Rais wa Malawi huyu akiwa anapigwa Picha na zinatumwa Mitandaoni na zingine kutumika Magazetini zikimwonyesha kuwa anasali?

Nitashukuru nikijibiwa na mnasalimiwa mno na wana Malawi hapa niishipo.

Karibuni.
Hawana cha kuposti, wanabaki kujifariji na mapichapicha.
 
Mada nyingine ni za kitoto mno.

Rais akipigwa picha kanisani wewe unapungukiwa au unaongezewa nini maishani mwako?.

Hizi ni mada za instagram.
 
Kiongozi uinaposema ' huku Kwetu ' una maanisha kuwa tupo sote hapa Lilongwe nchini Malawi au labda unamsema Rais mwingine wa Taifa lingine? Mimi nilidhani hili Jambo naliona tu hapa nchini Malawi nilipo kwa Rais wetu huyu kumbe yawezekana na Kwingineko nao wanakumbana na Jambo hili hili?
Namaanisha huku kwetu nilipo mimi..maana mimi sipo Lilongwe mkuu...nchi ingine kabisa maeneo ya Afrika Mashariki
 
Kuna kisa kimoja kilivuma miaka ya nyuma. Siku ya jumamosi moja,Mfugaji mmoja baada ya kuuza mifugo yake akapata pesa nyingi nayo jioni ikaingia akapata Wazo nikienda lala nyumba ya wageni naweza vamiwa nikauwawa nazo pesa zikachuliwa,hivo Salama nitafute nyumba ya ibada ni Salama kulala humo kesho Asubui niendelee na safari ya kurudi kijijini akaingia nyumba ya ibada akamuona mchungaji akamueleza shida yake na kiasi cha pesa alichonacho akapata hifadhi pa kulala ikiwa usiku wa manane Mchungaji akawaka tamaa,nae akafanya njama akamuuwa mfugaji ili arithi asichochuma nae akamfukia shambani akidhani ameukwepa mkono wa Bwana.Asubui yake akiwa anaendesha ibada akawaambia waumini wake tuinue mikono juu tumshukuru Mungu alipoinua mikono juu nayo pingu zikashuka toka mbinguni zikaifunga mikono yake mbele ya waumini wakipigwa butwaa na kushangaa kitendo hicho,hata zilipofanyika jitahada ya kuachanisha pingu zile haikuwezekana.Watu wa rohoni watambua hakika mtumishi huyu kuna jambo ovu amefanya.Kabla mtumishi yule muovu ajakata roho sababu ya Mateso ya rohoni na maumivu mwilini, akasimulia kisa chote cha aliyoyatenda.
Hivo Hakuna MTU muovu atayehesabiwa haki mbele za Bwana, siku zake zitakuwa ni za taabu na masikitiko,hadi atakapotubu na kuziacha njia zake mbaya.Si kila alitajale jina La Bwana atauona ufalme wa Mungu.Maisha ya dunia si zaidi ya kula na kunywa,yanini kuukimbiza upepo ili uiridhishe nafsi isiyotosheka?
 
Mada nyingine ni za kitoto mno.

Rais akipigwa picha kanisani wewe unapungukiwa au unaongezewa nini maishani mwako?.

Hizi ni mada za instagram.

Kila Siku hapa JamiiForums kunaanzishwa Mada ( Threads ) mbalimbali zaidi ya hata ya 1000 ili Kumpa Member chaguo pana la Kuchagua ni ipi inamvutia au imemvutia Kuisoma na bahati mbaya katika hizo Mada zote Wanaozianzisha huwa hawaandiki mahala popote pale kuwa ' Idiot ' Phillipo Bukililo ni lazima uisome isipokuwa huwa unawiwa Wewe mwenyewe Kuzisoma. Je baada ya Kuona ni Uzi wa Kitoto ilikuwaje tena ukaufungua na Kuusoma tena wote kabisa ukauelewa na ukaja na ' Majibu Takataka ' yako haya? Wenzenu tulipokuwa Wadogo ( Wachanga ) tulikuwa tunanyonya Maziwa na pengine ndiyo maana tupo hivi clever and bright, ila kuna uwezekano Mwenzetu Wewe ulinyonya Mikojo ndiyo maana umekuja na Hoja hovyo hovyo kama hii.
 
Mtoto mwingine huyu hapa. Kuna mada zenye logic na zisizo na logic.
 
Picha ya rais akiwa kanisani ni ishara nzuri sana kuthibitisha Mkuu wa nchi ni mchaMungu, hivyo serikali yake inatenda mema tuu na yale yampendezayo Mungu.
P
 
Kama ni hivyo / hivi sasa ni kwanini huyu Rais wetu wa Malawi 95% ya Vitendo vyake, Maamuzi yake na hata Kauli zake haziakisi kwa 100% huwa Ucha Mungu wake unaousema na kuonekana kama vile unautetea hapa? Kwanza naomba kujua na Wewe tuko wote hapa Lilongwe nchini Malawi au Wewe uko nchi gani?
 
Mada nyingine ni za kitoto mno.

Rais akipigwa picha kanisani wewe unapungukiwa au unaongezewa nini maishani mwako?.

Hizi ni mada za instagram.
Sasa nikwambie wewe ndiye mtoto na wewe na hao wapiga picha wa rais ndo mnaotakiwa mkashinde Instagram kurusha kila jumapili picha zake akiwa Kanisani,Rais akipigwa picha kwenye Sikukuu za kidini sio issue kubwa maana hubeba maono kwamba yupo pamoja na wananchi wake ila mnapotaka kutuonyesha kila siku yupo Kanisani ndo inapokuwa ishu.

Hata sisi tunaabudu wazazi wetu wengine wanakesha huko Kanisani kama anapenda kucheza sana na camera mngemshauri awe anaenda kutoa misaada na pole mahospitalini,orphanage centers etc ingeleta maana.
 
Back
Top Bottom