Naomba kujua Faida ambazo Wananchi wanapata kwa kila mara kuangalia Picha za Rais akitoka Dom kuja Dar na Dar kwenda Dom kwa Ndege

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Binafsi nitafaidika zaidi nikiona Picha za Rais yypo maeneo mbalimbali ya nchi yenye Changamoto mbalimbali akionana na Wananchi wake na kutatua Matatizo yao ya Kimsingi.

Mpaka hivi sasa GENTAMYCINE naitafuta Tija ya kila mara tu Mitandaoni tunaonyesha Picha za Rais akipunga mkono akipanda Ndege kutokea Dodoma kuja Dar es Salaam na akitua Dar es Salaam tena anatupungia mikono sana sana naanza Kupatwa na Wasiwasi juu yake na hata wale wanaloona hilo ni Jambo la Kimantiki Kimaendeleo.

Na kama Kutuonyesha Rais akipanda na kushuka katika Ndege huku akitupungia Mikono yake akina GENTAMYCINE kuna Tija mbona akipanda Gari zake kutoka Dodoma kuja Morogoro hatuonyeshwi akisimama katika Gari na Kutuaga na Kutupungia? Mmeambiwa Watanzania wote ni Washamba ( Mambwiga ) wa Kupanda Ndege?

Kwa Sindano yangu hii ambayo najua imeingia kabisa mfupani GENTAMYCINE nipo tayari Kuchukiwa au hata Kuitwa Sukuma Gang au kuambiwa nina Chuki, Wivu au natumika vibaya na Maadui au Mabeberu au hata Kuniwahisha Sebuleni Mbinguni sawa tu, ila mkifanya Jambo la Tija nitawapongezeni sana na mkiharibu nitawasema ( nitawasilibeni ) kama hivi.

Tunahitaji Maendeleo na siyo Mipicha.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,786
2,000
Mwananchi anahusika vipi na utaratibu wa ratiba za majukumu ya Rais ya kila siku ?!!!

Mwananchi wa Mtambaswala na Kibinda anakuwaje "emotional and obsessed" na safari za Rais wake humu nchini ?!!

#KaziIendelee
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Zile helkopita mbili,
V8,VXXX 80,
Basi,
Mafoleni masaa njiani mnasubiri mtu ale mahindi.
Hamkuona shida?

MAMA IKIMPENDEZA AWE ANAAMKIA MAKUNDUCHI ANAKUJA ANATUMBUA JIONI ANARUDI MAKUNDUCHI
50/50 mnune zaidi
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
10,955
2,000
Pesa ipo tatizo Nini kikubwa Ni matumizi ambayo hayatoki nje yanabaki hapahapa..tuleni maisha ila tafuteni hela
 
Manyema

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
366
1,000
Na kwa nn asipande ndege ya rais yeye anatumia zile kubwa Airbus na uhakika delegates yake yote bado haijazi zile ndege. Ni gharama sana kuziendesha hizo ndege especially kwa hizi safari zisizokuwa na tija, by the way akae Dodoma afanye kazi otherwise ahamie Dar mazima tujue moja
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,786
2,000
Hilo dude moja kuliungurumisha Dar Dodoma si chini ya milion 20

Samia akienda Dar Dodoma Tripu 6 kwa Mwezi ni zaidi ya milion 120 pesa za walipa kodi

Hizo pesa zingejenga madawati na zahanati za kutosha tu!
Changamoto nyingine za nchi zinasubiri madawati yaenee ?!!

Nchi kubwa kama hii ina kila aina ya changamoto.....kwani "TRIPU"za kwenda na kurudi Dodoma ni za kucheza?!!!

Yaani hizo "milioni 20"unazozisema unaziona ni nyingi sana kwa matumizi ya raia no.1 katika kutuhudumia watanzania....kwani Rais ni sawa na DED ama DAS?!!!

Khaa kweli malalamiko tumeumbiwa wanadamu ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Born1703

JF-Expert Member
May 17, 2020
890
1,000
Binafsi nitafaidika zaidi nikiona Picha za Rais yypo maeneo mbalimbali ya nchi yenye Changamoto mbalimbali akionana na Wananchi wake na kutatua Matatizo yao ya Kimsingi.

Mpaka hivi sasa GENTAMYCINE naitafuta Tija ya kila mara tu Mitandaoni tunaonyesha Picha za Rais akipunga mkono akipanda Ndege kutokea Dodoma kuja Dar es Salaam na akitua Dar es Salaam tena anatupungia mikono sana sana naanza Kupatwa na Wasiwasi juu yake na hata wale wanaloona hilo ni Jambo la Kimantiki Kimaendeleo.

Na kama Kutuonyesha Rais akipanda na kushuka katika Ndege huku akitupungia Mikono yake akina GENTAMYCINE kuna Tija mbona akipanda Gari zake kutoka Dodoma kuja Morogoro hatuonyeshwi akisimama katika Gari na Kutuaga na Kutupungia? Mmeambiwa Watanzania wote ni Washamba ( Mambwiga ) wa Kupanda Ndege?

Kwa Sindano yangu hii ambayo najua imeingia kabisa mfupani GENTAMYCINE nipo tayari Kuchukiwa au hata Kuitwa Sukuma Gang au kuambiwa nina Chuki, Wivu au natumika vibaya na Maadui au Mabeberu au hata Kuniwahisha Sebuleni Mbinguni sawa tu, ila mkifanya Jambo la Tija nitawapongezeni sana na mkiharibu nitawasema ( nitawasilibeni ) kama hivi.

Tunahitaji Maendeleo na siyo Mipicha.
Em nikisie ulicholenga... Nahisi ulimaanisha awe anakutana na raia awapo ziaran kama alivyokuwa anafanya Aliepita anafika eneo fulan anasikiliza kero za wananchi alaf anatatua ILA huyu yy ni kwa mawingu tu mda wote hana muda na kusikiliza hizo kero au nmekosea mkuu??
 
Umuzukuru

JF-Expert Member
May 30, 2019
489
500
Matatizo yapo miaka dahali sasa yaani tangu uhuru zaidi ya miaka hamsini
Uhaba wa madawati na madarasa
Uhaba wa dawa mahospitalini
Lishe duni
Rushwa
Uongozi mbovu
Unyonyaji wa tabaka la chini kama vile kodi zisizokua na maelezo ya wazi ni namna gani zinavyotumika
Umaskini
Maradhi
Ujinga na ulimbukeni

Shida zipo na bado zipo
Mwache Mama apande ndege
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,340
2,000
Tunajua ya kwamba mashine zipo fresh bado na ATCL wanaingiza mpunga kwa ndege kukodiwa na serikali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom