Naomba kujua dhana ya supply na demand kuhusiana na suala la njaa

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Kwa maisha ya kila siku ya binadamu dhana ya Supply and demand hutawala katika maisha yake.

Kwa mfano supply ikiwa kubwa basi bidhaa/huduma itakuwa nyingi na hapo bei nayo itashuka na wengi watakuwa na uwezo wa kununua bidha/huduma hizo lakini demand ikiwa kubwa na supply ikawa ndogo basi wanunuzi watakuwa wachache na bei kubwa itakuwa kwa vitu vichache.

Sasa niielekeze hili kwa suala la njaa. Ukitembea barabara nzima toka Geita mpaka Musoma mazao yote yaliyopo kando kando ya barabara yamekauka yote kwahiyo dhana ya supply kuwa kubwa hapa haipo hata kidogo na hivyo demand itakuwa kubwa kwa bidhaa chache.

Mfano mimi jana nimenunua debe la mahindi Geita mjini kwa Tshs.18,000.

Niliwauliza kwa nini mnaniuzia bei ghali hivyo wakanieleza kuwa wakulima hawakuvuna kwa sababu ya ukame. Kama mkulima hakuvuna Je? HATAKUWA NA NJAA?

Kwahiyo tunaposema kuwa hakuna njaa mimi mtu wa kawaida ninawashangaa sana. Kama sikuvuna chochote msimu huu kwa nini mnasema njaa hakuna.

Serikali ipite Mkoa kwa Mkoa ili ifanye tathmnini na izungumze na wananchi kuhusu suala hili. Nchi ni yetu sote tushikamane kwa pamoja na tusilaumiane hata kidogo.
 
Back
Top Bottom