Beira Boy
JF-Expert Member
- Aug 7, 2016
- 17,895
- 25,944
Aman iwe nanyi wakuu
Naomba kuijua kura ya turufu ambayo ndo nasikia huwa ina amua nani awe rais hata kama wananchi hawaja mchagua
Je kura hiyo huwa inapigwa na nan na akina nan
Nawasilisha
BOY FROM LONDON
Sent using Jamii Forums mobile app
=======================================
Kura ya turufu (Veto) ni haki ya kukataza Azimio lisipite wala kutekelezwa hata kama limekubaliwa na wengi. Katika nchi nyingi Rais au Kiongozi wa Taifa kwa manufaa ya Taifa ana haki ya kukataza maazimio au sheria zilizokubaliwa na Bunge akiona kasoro au hasara ndani yake
Mfano; nchini Marekani Rais ana haki ya kukataza sheria iliyokubaliwa na Bunge katika kipindi cha siku 10 baada ya Azimio la Bunge. Akipiga Veto Aheria inarudi Bungeni na hapo Bunge linaweza kufuta Veto kwa theluthi mbili za kura au kubadilisha sheria
Mataifa matano yanaweza kutumia kura ya Turufu (Veto) katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Kila moja kati ya hayo linaweza kuzuia maazimio ya Baraza la Usalama