Naomba kufundishwa Kiswahili chenye maandishi ya Kiarabu

Kiswahili ni lugha ya kibantu


Bakari, Kiswahili sio lugha ya kibantu pekee, Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha kadhaa kama, 1- kibantu (lugha za makabila ya wabantu), 2- Kiarabu, 3- Kireno, 4- kijerumani, 5- kihindi.

Katika kiswahili, Kibantu ni takriban maneno 70%, kiarabu 25%, na 5% ni hizo lugha zingine.

Kwa maneno mengine kiswahili ni lugha chotara (hibreed language/ clone language).
 
Bakari, Kiswahili sio lugha ya kibantu pekee, Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha kadhaa kama, 1- kibantu (lugha za makabila ya wabantu), 2- Kiarabu, 3- Kireno, 4- kijerumani, 5- kihindi.

Katika kiswahili, Kibantu ni takriban maneno 70%, kiarabu 25%, na 5% ni hizo lugha zingine.

Kwa maneno mengine kiswahili ni lugha chotara (hibreed language/ clone language).
Asante sana bwana, unachoelezea ni ya kweli kabisa.
Kwa mujibu wa baadhi ya wanachuoni Wachina, japokuwa Kiswahili ni lugha ya mchanganyiko, lakini lugha hiyo ni mojawapo ya lugha za Kibantu maana sarufi yake inafanana na lugha zingine za Kibantu(aina tofauti za nomino, subjective prefix, tense marker na objective prefix na kadhalika). Aidha, mengi ya maneno ya lugha hiyo yanatokana na Kibantu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ufundishaji wa Lugha za Kiafrika nchini China, Prof. FENG anafikiri kuwa "japo Kiswahili kina maneno kadha kutoka kwa lugha zingine zikiwemo Kiarabu, Kiajemi, Kihindi hata Kizungu, lakini lugha hii ni moja ya Kibantu tukiangalia asili yake."
 
kulia kushoto sentensi ina sema "kuwa anatamani" baadhi ya sentensi hazionekani vzr. nitakusomea tu zile zinazoonekana
 
katika sehemu za pwani hassan Unguja na Lamu, hata leo baadhi ya watu hutumia alama hizo za kiarabu kuandika kiswahili.
Marehem baba yangu alikuwa anajua kuandika aina zote mbili kwa kuwa babu yangu hakuwa akitumia hati za Kilatini, kwa hiyo walikuwa wakiandikiana barua za Kiswahili kwa hati za kiarabu, ila mimi nilikuwa tunaandikiana kwa hati za Kilatini. Sahihi usemavyo, ila 90% ya watu hawajui kitu hichi, alipokirasimisha Muingereza Kiswahili mnamo miaka ya 1930 hivi , akachagua Kiunguja Mjini iwe lahaja rasmi ya Kiswahili dhidi ya lahaja ya Kimvita (Kimombasa), na akakifanya kuwa na hati za Kilatini kutoka za kiarabu.
 
katika sehemu za pwani hassan Unguja na Lamu, hata leo baadhi ya watu hutumia alama hizo za kiarabu kuandika kiswahili.
Hata maeneo ya kwetu Rufiji, maana nakumbuka wakati tupo Madrasa mwalimu wetu alikua anatufundisha kuandika kiswahili kwa herufi za kiarabu. Kama kuandika Barua ya uchumba.

pia nilifanikiwa kuziona Barua za Marehemu Babu yangu ameandika kiswahili Kwa herufi za kiarabu,
 
🤣 Hiyo ni "syntax" ya kiarabu!!, katika Kiswahili ilitakiwa iwe hivi:-

"---Muingereza aliporasimisha kiswahili---".
Ni aina ngapi ya maelezo unayajua ?
Unayajua maelezo aina ngapi ?
Je kenda na tisa ipi sahihi ?
Moyo na mtima ?
Aila na familia?

Mh !! Sawa msomi wa Kiswahili ila kina meno !!
 
Sina kii bodi ya kiarabu.Ila inawezekana kuandika kiswahili kwa kiarabu tena ndio inatamkika vizuri.
Sina keyboarf ya kiarabu ntakupigis picha karatasi japo nilisoma hizo herufi zamani.

I- alifi ni kama a kirumi.
Bee ni yuu yenye kanukta.
Tee ni yuu yenye nukta mbili juu.
Thee ni yuu yenye nukta tatu .
Kwa herufi hizo ukiandika tetea, utachukua yu mbili na Alifu moja .
kuna vinukta vinaunds sauti mbali mbali kama thuma kisne nk.
ukikaa na mtu aliesoma kiarabu just a weak utaweza kusoma kiarabu kwa kiswahili.
Baba utachukua yu mbili uziunge.
 
Back
Top Bottom