Naomba kufahamu Zanzibar Kuwa mshiriki CECAFA.

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Ndugu mwenye ufahamu anifahamishe tafadhali.

Mashindano ya CECAFA *council for East and central Africa football Association*,ni mashindano ya kila mwaka yanayoshirikisha National teams(timu za kitaifa) kutoka nchi za Afrika mashariki na Afrika ya kati.

Mfano,Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi,Ethiopia, Libya,na nyingine.

Sijawahi kupata jibu ushiriki wa timu ya Kilimanjaro stars ,je inawakilisha Taifa lipi kati ya Tanzania na Tanzania bara(Tanganyika) ,na je Tanzania bara au Tanganyika ni nchi inayotambuliwa na CECAFA?

Je, vipi tena timu ya Zanzibar heroes inasimama kama Timu ya taifa ya Tanzania visiwani (Zanzibar) ,je Zanzibar ni taifa linalotambuliwa na CECAFA?

Maana kuna mechi ilichezwa kati ya Libya na Tanzania na alama ya bendera zao za taifa.

Tare. 5 dec.kuna mechi ilichezwa kati ya Zanzibar na Rwanda, na alama za bendera zao za taifa.

Tareh 7.DEC.Tanzania imecheza na Zanzibar na zote zikawa na alama za bendera zao.

Na kama ni hivyo kwanini CAF haitambui Zanzibar Heroes?

Sielewi msaada Ndugu.

Abdul Nondo.
0659366125.
 
CECAFA umeinyambulisha vizuri.

Sijui kama ulivyoinyambulisha, hiyo sehemu ya "Football Associations" unaielewa.

Footbal Association si lazima ziwe moja kwa nchi. Tanzania tuna mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.

Hivyo Zanzibar wanatumia Association yao.

Ni moja kati ya matokeo ya Muungano wetu.
 
CECAFA umeinyambulisha vizuri.

Sijui kama ulivyoinyambulisha, hiyo sehemu ya "Football Associations" unaielewa.

Footbal Association si lazima ziwe moja kwa nchi. Tanzania tuna mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.

Hivyo Zanzibar wanatumia Association yao.

Ni moja kati ya matokeo ya Muungano wetu.

Matokeo ya uvamizi . Tanganyika iliivamia Zanzibar na kumkamata Waziri Mkuu wake Muhammed Shamte pamoja na mawaziri wake na kufungwa katika jela za Tanganyika bila kufikishwa mahakamani ,kabla huo uitwao muungano hata haujafikiriwa
 
Zanzibar ni mwanachama wa cecafa
Katiba ya cecafa inatambua vyama badala ya nchi
 
Back
Top Bottom