Naomba kufahamu ukweli kuhusu chanjo za kichocho na minyoo mashuleni

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,005
1,337
Naombeni ukweli kutoka kwenu. Leo wanafunzi wameambiwa kwenda na chakula shuleni ili wakapewe dawa za minyoo na kichocho. Katika mijadala mingi Jana, watu wengi hawtaki watoto wao wapatiwe dawa hizi.

Zaidi hata madaktari wamezuia watoto wao kwenda shuleni kupewa hizo dawa.

Nipeni ukweli juu ya hizi dawa maana sijui chochote.
 
Aulizae anataka kujua

Ni hivi:-

Dawa za minyoo na kichocho wanazopewa watoto mashuleni siyo chanjo bali ni tiba kwani kama mwanafunzi atakuwa na minyoo au kichocho akipewa dawa hizo anapona mala moja.

Pili dawa hizo huwa hazina madhara yoyote ya muda mrefu zaidi ya tofauti ya kujisikia kwa muda mfupi tu.

Dawa za kichocho za parazenquantel huwa zinamfanya mtumiaji kukosa nguvu kwa muda mfupi na saa ingine kutapika inashauriwa hali kama hiyo ikitokea basi mtumiaji anywe bakuli la uji au chai ili apate nguvu

Dawa za minyoo huwa hazina madhara yoyote kama mtumiaji atakunywa dawa hizo ambazo huwa ni Albendazole basi kama ana minyoo itatatoka yote na kama hana basi.

Huwa inashauriwa mtu kunywa dawa za kutoa minyoo tumboni kila baada ya miezi mitatu awe amepima au hajapima ina manufaa zaidi kwa afya yake maana munyoo ni parasite wazuri na huwa wanakula chakula mtu anachokula na kumfanya mtu mwenye minyoo kudhoofu.
 
Back
Top Bottom