Naomba kufahamu Sheria yetu ya hapa Tanzania inasemaje kwa mtu/muajiri anae kashifu wafanyakazi wake

Joninho

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
559
611
Habari zenu ndugu na wanachama wenzangu wa hapa Jamiiforum?
Nimatumaini yangu kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu mmeamka salama,niwatakie jumapili njema nyote .

Nielekee moja kwa moja ktk mada kuu Kama kichwa Cha habari kinavyo jieleza,
Naomba kufahamu Sheria yetu ya hapa Tanzania inasemaje kwa mtu/muajiri anae kashifu wafanyakazi wake kila ikifika mwisho wa mwezi ili asiwalipe mishahara yao kwa kuwaita wezi, mbwa na washenzi.
Rekodi zote za mazungumzo yake akitukana na kudhihaki vijana wa nchi hii zipo, na akijisifia"nendeni popote".
Naomba Wana wa Jamiiforum mnisaidie kujua Sheria yetu inasemaje ktk kutumia lugha ya matusi na kuwakashifu wengine.
 
Pole sana mkuu.

Mtaje basi hata kwa jina kampuni yake
Nitamtaja mkuu na ushahidi wa matusi yake, Hawa waajiri wa shule binafsi tena zisizo nausajili baadhi wanataka kua Miungu watu kutumia tatizo la ajira kuto kuwalipa waalimu ili wawafukuze wapate wapya.
 
Ukitaja hiyo taasisi ujumbe utafika mbali na msaada utapatikana
 
Mkuu shule.haina usajiri hao watoto wanafanyaje mitihani ya taifa?

Au n tution center pia n day care?

Kumbuka matokeo ya g7 yametoka isije kuwa mmeharibu
 
Habari zenu ndugu na wanachama wenzangu wa hapa Jamiiforum?
Nimatumaini yangu kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu mmeamka salama,niwatakie jumapili njema nyote .

Nielekee moja kwa moja ktk mada kuu Kama kichwa Cha habari kinavyo jieleza,
Naomba kufahamu Sheria yetu ya hapa Tanzania inasemaje kwa mtu/muajiri anae kashifu wafanyakazi wake kila ikifika mwisho wa mwezi ili asiwalipe mishahara yao kwa kuwaita wezi, mbwa na washenzi.
Rekodi zote za mazungumzo yake akitukana na kudhihaki vijana wa nchi hii zipo, na akijisifia"nendeni popote".
Naomba Wana wa Jamiiforum mnisaidie kujua Sheria yetu inasemaje ktk kutumia lugha ya matusi na kuwakashifu wengine.
Kitu unachopaswa kujua, sheria ya kazi hairuhusu ubaguzi sehemu za kazi. Kufanya vitendo au kutoa kauli zozote za kibaguzi, matusi nk. Nikinyume cha sheria ya kazi? Kama kweli anayoyasema anaushahidi nayo anapaswa kuwawajibisha kwamujibu wa sheria na taratibu za kazi.

Kuhusu mshahara, nihaki ya mfanyakazi kupewa malipoyake kama makubaliano yanavyotaka alipwe.

Mwisho; ukitaka kumwajibisha mwajiri anayefanya matendo ya hovyo kwa waajiriwa wake. Lipo baraza la usuluhishi la wafanyakazi (CMA) Commission for Mediation and Arbitration wao wanahusika moja kwa moja namaswala yote yanayohusu migogoro/ matatizo yanayowakumba wafanyakazi. Ukiona unahitaji kumchukulia hatua basi tafuta CMA nauwasilishe malalamiko yako.
 
Maelezo mazuri Boss shukrani.
 
Back
Top Bottom