Naomba kufahamu masoko ya kuuza asali kwa jumla

Forbes1990

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
513
989
Habari za Jumapili,

Napenda kufahamishwa masoko ya kuuza asali kwa jumla kuanzia lita 20 na kuendelea. Nimesikia wanunuzi wa kubwa ni viwanda vya madawa na cosmetics. Ukiachilia mbali kampuni zinazonunua asali kwa matumizi ya binadamu.

Hivyo basi naomba mnisaidie wakuu.

Asanteni sana.
 
Samahani mie nataka kujua tu kipindi gani hua ndo msimu wa asali huko Tabora na Kijiji au wilaya inapopatikana kwa wingi ile original kabisa, natanguliza shukran wakuu
 
Nafikiri ungeandika tu kuwa unayo au unaweza kupata Asali nzuri (first class); Kiasi gani unayo na mahali/Mkoa ulipo. Kwa mtu anayehitaji au anayejua soko akujulishe
Wanunuzi wengine wamo humu humu...
 
Ndugu. Kwa kufikiri kwangu, naona kuwa soko rasmi la Asali kwa Tanzania bado ni changamoto. Kwa sasa ni kuwa wafugaji wengi tunauza ktk soko la mtaani.

Kama uko mikoa ya nyanda za juu kusini nitumie ujumbe nikuelekeze MTU anaenunua kuanzia Lita 20.
Hakikisha uwe na Asali iliyotazamwa kwa reflectometer ili iwe na water content isiyozidi 17.

Pia itategemea unazo Lita ngapi. Kama ni chache ni vema ukauza katika soko lilo jirani na unakoishi. Hakikisha ubora na viwango kwa kuwa Asali inaliwa bila kupikwa.
 
Samahani mie nataka kujua tu kipindi gani hua ndo msimu wa asali huko tabora na Kijiji au wilaya inapopatikana kwa wingi ile original kabisaaaa, natanguliza shukran wakuu
Asali inaanza kurinwa (kuvunwa) trh 01/7 hadi september ya kila mwaka, wenyewe wanaita msimu.

Asali orijino inapatikata Tabora mjini ikitokea wilaya ya Sikonge na Inyonga.

Unapohitaji asali 'orijino' weka sharti la kununua asali mbichi.
 
Ndugu. Kwa kufikiri kwangu, naona kuwa soko rasmi la Asali kwa Tanzania bado ni changamoto. Kwa sasa ni kuwa wafugaji wengi tunauza ktk soko la mtaani.

Kama uko mikoa ya nyanda za juu kusini nitumie ujumbe nikuelekeze MTU anaenunua kuanzia Lita 20.
Hakikisha uwe na Asali iliyotazamwa kwa reflectometer ili iwe na water content isiyozidi 17.

Pia itategemea unazo Lita ngapi. Kama ni chache ni vema ukauza katika soko lilo jirani na unakoishi. Hakikisha ubora na viwango kwa kuwa Asali inaliwa bila kupikwa.
Huyo mnunuzi ananunua hadi plastiki mia tano kwa mkupuo?
 
Back
Top Bottom