Naomba kufahamu kuhusu Vyura wa Kihansi

Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

duuh they are very lucky
mix with yours
 
hapo ndio nashindwa kuelewa kwa nini wana gharama namna hiyo

Gharama yake ni kuwaondoa kwenye makazi yao halisi kwa ajili ya kujenga ya kufanya human activities, yaani ni kama wewe vile upelekwe kuishi ndani ya maji(not your natural habitat, itahijika meli kebu au nyumba itakayokufanya kusiwe na tofauti kati ya majini na nchi kavu ili uishi). Ilitakiwa Bwawa la Kihansi lisijengwe kwa ajili ya hawa vyura. Ona leo umeme bado wa mgao mabwawa yanakauka na bado vyura wanagharamiwa.

Wasiwasi wangu ni kuwa je hawa vyura wanaotoka marekani ni wale wale?, hawajafanyiwa croning na kutuletea bugs ambao tutakosa hata dawa yake pindi wakiisha fanya mutation na kuanzisha ugonjwa mwingine mmbaya zaidi ya Ukimwi kama vile "Ukosefu wa akili vichwani" - UAV, ambao hautakuwa na tiba kabisa unaoambukizwa kwa njia ya hewa "airborne disease"
 
hilo nalo neno tena neno kubwa
mix with yours
 
Njowepo na Bona, sikujua kama kweli kuna watu katika JF ambao hawajui maana ya kutunza mazingira na viumbe wake katika karine hii. Kusema kweli kama mwana ecolojia ni meshangaa sana kuona hamjui faida ya kuwatunza vyura hao. Mngekuwa mmetembea kidogo nchi kama Misri naona mngesgaa kuona jiwe la picha ya Sphinx ambalo japo limemomonyoka lakini linatunzwa kama lulu. Na watu wana miminika duniani kuja kuliangalia na nchi ya Misri inapata watalii wengi sana. Ushauri wangu ni kwamba muende shule ili mjue maana ya utunzaji mazingira. Kama ni umaskini unaletwa na mambo mengine lakini sio vyura vya kihansi.
 
tutake radhi tafadhali.....inaelekea ambaye hajaenda shule ni wewe....hapa tunaongelea Misri au tunaongelea habari za nchi yetu......ok wewe mwanaikolojia uliyeenda shule na ukatembelea Misri tupe faida ya wale vyura....#*&^@
 
Kama umesoma historia ya nchi hii Wazungu walichukua mmea wenye jina la "busy lizzie" ambao ni ornamental (wa mapambo). Walipochukuwa haukuwa na thamani yo yote katika Milima ya Usambara lakini leo huko Ulaya mmea ule ni biashara ya maelfu ya madola na maeuro. Na Tanzania kama nchi imeambulia nini? Zeeeeeeeero. Angalia na vipepeo vya hapo hapo kwenye milima ya Usambara leo ni biashara kubwa sana na miaka michache tu nyuma havikuwa na thamani yo yote. Angalau kwenye vipepeo kidogo watu walikuwa wameamka na ndio tunapata kamgao kadogo.

Kama Mwenyezi Mungu ameamua kumuweka chura huyu wa kipekee duniani hapo Kihansi lazima anazo sababu zake, kwa nini sisi binadamu ndiyo tuwe mstari wa mbele kuwamaliza? Leo tukimmaliza chura huyo, kesho Sanje mangabay (kima wa kipekee kwenye milima ile) na keshokutwa mwengine na mwengine......... hatimae tutakuwa weupeeeeee

Lazima tuhifadhi bioanuwai aliyotujaalia Mungu
Lazima tuhifadhi mazingira na hasa yale yenye viumbe adimu duniani. Siku moja kama sio sisi basi hata wajukuu zetu watakuja kuona faida zake. Na tukiharibu watakuja kutulaani.
 
Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

Preta;
Katika mfumo wa kimazingira (ekologia) viumbe wote kwa namna moja au nyingine wana uwiano na mazingira yao. Ina maana kwamba kila kiumbe aliyepo duniani ni muhimu sana kwa nafasi yake na anawezesha wengine pia kuwepo kwa uwiano sahihi (food chain, food web and maintanance of ecosystem functions). Huu uwiano wa viumbe hai pamoja na mazingira yake unasababisha mambo mengi sana ambayo kwa wakati mwingine huwa siyo rahisi kuyaona. Kwa mfano, wanyama wengi sana, wakiwemo vyura ni chakula cha wanyama wengine kama ndege, nyoka na hata mammalia. Pia vyura wanakula wadudu wengi sana na kusaidia moja moja katika kuthidibiti mfumuko wao. Mtiririko mzima wa maisha ya viumbe hai tokea mwanzo mpaka sasa (evolution) bado haujakamilika sawa sawa na viumbe wengi sana, wakiwemo vyura ni muhimu kuelezea hatua mbali mbali za huu mtiririko huu.

Nikirudi kwenye shwali lako moja kwa moja, vyura kama wanyama, wapo katika kundi linaloitwa Amphibia. Hawa ni wale ambao hawawezi ishi mbali na maji (isipokuwa wachache sana). Wanahitaji maji kwa kuwa wanapumulia ngozi ambayo ili waweze pumua inabidi iwe na nyevu nyevu (kama mapafu yetu). Pia kuzaa kwao ni lazima maji yawepo kwa kuwa mayai yao hayana gamba kama lile la yai la kuku au mjusi. Zaidi ya hayo, watoto wao karibu wote ni viluilui ambavyo vinapumulia mapezi (gills) kwa kuchukua hewa iliyomo majini. Kwa hiyo kwao maji ni muhimu sana.

Kama alivyodokeza mdau mmoja hapo juu, baada ya ujenzi wa bwawa la umeme la Lower Kihansi, ilikuja gundulika kuwa kule maji yalikokuwa yakijibamiza na kutoa mvuke, kuna wanyama walioathiriwa na huo ujenzi, hasa baada ya mvuke kukoma. Wanyama waliogunduliwa walikuwa na hawa vyura kibiologia wanaitwa; Aspergillus nectophrynoides. Sababu kubwa ya kuangamia kwao ni kupungua kwa mvuke (water splash) iliyotokana na maporomoko ya mto Kihansi na si fungus kama wengine wanavyosema hapa. Mbaya sana hawa vyura walikuwa ndiyo wanagunduliwa kwa mara ya kwanza na ikaonekana kuwa hakuna sehemu ingine Duniani waliko isipokuwa hapo tu. Ukiwa na haraka unaweza sema, so what?! Lakini kama nilivyosema; kibiologia, vyura karibu wote wanataga mayai. Wanaozaa ni wachache sana wakiwamo hawa. Kuzaa ni ishara ya kuwa juu ya wenzako (advanced charactericticis) na kwa hiyo zinaashiria kitu ambacho hatukijui na kinaweza kuwa muhimu sana katika ugunduzi zaidi ambao unaweza pia kupaisha kiwango cha maisha ya binadadmu kwa ujumla. Hii sababu, na zile kwamba hawa ndugu ni chakula muhimu kwa viumbe wengine na pia wanakula wengine ni moja ya reasons za kuwatunza. Reasons zingine ni nyingi sana, lakini kubwa pia ni kwamba kama viumbe hai wanastahili kuishi na kuheshimiwa.

Nimejaribu kutafsili kutoka kwenye kiinglish (kidhungu). Kama kuna swali uliza vyovyote vile.

NB: Usiniulize habari za mbu na Plasimodium sp.!
 
Mkuu umejitahidi sana na umeeleweka ila hapo kwenye mvuke nadhani si sahihi, hao vyura wanategemea hali ya unyevu nyevu ili kuishi na si mvuke. Mvuke unapatikana baada ya maji kuwa ya moto.
 
Nilishafika kihansi kama mmoja wa hao watafiti ambao walipewa kazi ya kuangalia, 1-Kama hao vyura bado wapo, 2- Kuona kama fungus ambao ndio chanzo cha kufa kwa hao vyura pale Kihansi bado wapo. Nilikaa siku 7 pale camp na nikapanda kule goji kutafuta hao vyura usiku na mchana bali tulikuta vyura wengine wengine tu, tulichofanya ni kuchukua swab ya wale vyura tuliochokua ili tuweze kujua kama nao wameadhiliwa na hao detrimental fungus. Utafiti bado haujakamilika na utachukua muda mrefu sana na ndipo serikali ikaamua kurudisha hai vyura baada ya kujenga aquarium pale UDSM. Kule marekani Boston wale vyura waliakuwa kwenye aquerium ambazo ni fungus free kwa hio walinusuriwa wasipotee kwani hawa ni unique species hapa duniani, na tulikuwa tunawalipa wamarekani kwa kuwafuga hao vyura dola laki 2 kwa mwaka ndipo JK akaamuru warudishe Tz. Pale UDSM pamejengwa aquerium kama zile za marekani kwa hio hao vyura waliokuja juzi watawekwa pale, hio aquarium ina kila kitu sawa na kihanzi yaani AC, water sprashes na Drosophia(wadudu) kama chakula chao.

Naomba muanishe faida zao zinazowafanya wapate huduma zenye gharama kubwa, ambazo zingeweza kuwapunguzia waTz makali ya maisha
 
Preta;
Katika mfumo wa kimazingira (ekologia) viumbe wote kwa namna moja au nyingine wana uwiano na mazingira yao. Ina maana kwamba kila kiumbe aliyepo duniani ni muhimu sana kwa nafasi yake na anawezesha wengine pia kuwepo kwa uwiano sahihi (food chain, food web and maintanance of ecosystem functions). Huu uwiano wa viumbe hai pamoja na mazingira yake unasababisha mambo mengi sana ambayo kwa wakati mwingine huwa siyo rahisi kuyaona. Kwa mfano, wanyama wengi sana, wakiwemo vyura ni chakula cha wanyama wengine kama ndege, nyoka na hata mammalia. Pia vyura wanakula wadudu wengi sana na kusaidia moja moja katika kuthidibiti mfumuko wao. Mtiririko mzima wa maisha ya viumbe hai tokea mwanzo mpaka sasa (evolution) bado haujakamilika sawa sawa na viumbe wengi sana, wakiwemo vyura ni muhimu kuelezea hatua mbali mbali za huu mtiririko huu.

Nikirudi kwenye shwali lako moja kwa moja, vyura kama wanyama, wapo katika kundi linaloitwa Amphibia. Hawa ni wale ambao hawawezi ishi mbali na maji (isipokuwa wachache sana). Wanahitaji maji kwa kuwa wanapumulia ngozi ambayo ili waweze pumua inabidi iwe na nyevu nyevu (kama mapafu yetu). Pia kuzaa kwao ni lazima maji yawepo kwa kuwa mayai yao hayana gamba kama lile la yai la kuku au mjusi. Zaidi ya hayo, watoto wao karibu wote ni viluilui ambavyo vinapumulia mapezi (gills) kwa kuchukua hewa iliyomo majini. Kwa hiyo kwao maji ni muhimu sana.

Kama alivyodokeza mdau mmoja hapo juu, baada ya ujenzi wa bwawa la umeme la Lower Kihansi, ilikuja gundulika kuwa kule maji yalikokuwa yakijibamiza na kutoa mvuke, kuna wanyama walioathiriwa na huo ujenzi, hasa baada ya mvuke kukoma. Wanyama waliogunduliwa walikuwa na hawa vyura kibiologia wanaitwa; Aspergillus nectophrynoides. Sababu kubwa ya kuangamia kwao ni kupungua kwa mvuke (water splash) iliyotokana na maporomoko ya mto Kihansi na si fungus kama wengine wanavyosema hapa. Mbaya sana hawa vyura walikuwa ndiyo wanagunduliwa kwa mara ya kwanza na ikaonekana kuwa hakuna sehemu ingine Duniani waliko isipokuwa hapo tu. Ukiwa na haraka unaweza sema, so what?! Lakini kama nilivyosema; kibiologia, vyura karibu wote wanataga mayai. Wanaozaa ni wachache sana wakiwamo hawa. Kuzaa ni ishara ya kuwa juu ya wenzako (advanced charactericticis) na kwa hiyo zinaashiria kitu ambacho hatukijui na kinaweza kuwa muhimu sana katika ugunduzi zaidi ambao unaweza pia kupaisha kiwango cha maisha ya binadadmu kwa ujumla. Hii sababu, na zile kwamba hawa ndugu ni chakula muhimu kwa viumbe wengine na pia wanakula wengine ni moja ya reasons za kuwatunza. Reasons zingine ni nyingi sana, lakini kubwa pia ni kwamba kama viumbe hai wanastahili kuishi na kuheshimiwa.

Nimejaribu kutafsili kutoka kwenye kiinglish (kidhungu). Kama kuna swali uliza vyovyote vile.

NB: Usiniulize habari za mbu na Plasimodium sp.!

Ahsante kw maelezo mkuu. Lakini kwa mbali nahisi kujiuliza kama cost-benefit balance inai-favor nchi kama Tanzania kufanya miradi kama hii...
 
Ndiyo. Kwenye international treaties/convention, ni lazima kama ume-sign na ni member utekeleze kama ilivyo. Hao vyura ni moja ya threatened species na kwa hiyo zinahitaji utunzaji wa hali ya juu sana. Mfano mzuri wa vitu vinavyotunzwa sana ni wale vifaru wa kule Ngorongoro crater. Wanalindwa sana. Kibiologia, vyura na Tembo kama wanyama wako kwenye ngazi (level) moja linapokuja suala la uhifadhi.
 
Preta;

Aspergillus nectophrynoides[/COLOR][/URL]. Sababu kubwa ya kuangamia kwao ni kupungua kwa mvuke (water splash) iliyotokana na maporomoko ya mto Kihansi na si fungus kama wengine wanavyosema hapa......

Naomba nikusahihishe mambo mawili.

Jina sahihi la Chura wa Kihansi kwa kilatini ni Nectophrynoides asperginis

Kupungua kwa unyevu katika maporomoko ni moja ya sababu. Sababu nyengine ni chytrid fungus ambao husababisha magonjwa yanayoitwa "chytridiomycosis". Baadhi ya vyura waliokufa Kihansi mnamo miaka ya nyuma walichukuliwa na kufanyiwa utafiti - walionekana kuwa na ugonjwa huo wa chytridiomycosis. Ugonjwa huo ndio unamaliza vyura kwa kasi duniani.

Umewahi kufika Kihansi? Suala la unyevu tayari lilishadhibitiwa kwa kiwango kikubwa kwani kule juu kuna "specially designed sprinklers" ili kujaribu kurejesha ule uwiano uliokuwa unawahifadhi vyura hapo zamani.
 
Ni kweli. Nilikosea jina lake na nasikitika kwa usumbufu. Hiyo niliyotaja ni species nyingine kabisa. Ila sababu halisi ni upungufu wa water spray (mvuke/?!). Zile sprinklers zenu ni fake haziendani na ualisia ambao toad hao wame-evolve nao miaka yote. Ugonjwa huo uliibuka baada ya kisanga za water spray kupungua kutokana na diversion ya maji, no one knew anything before about the disease as was for the toad. More research is needed anyway. Afterall, in events of natural disturbances such as diseases outbreaks, always the fittest will survive. Umeuliza kuhusu kufika Kihansi jibu ni ndiyo.
 
Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

Mdau kama uko dar nakushauri nenda pale waterfront kuna jamaa mlinzi kampuni ya eagle kama sikosei analinda huu upande wa parking za bm wa crdb mweusi hv jicho lake moja bovu yeye ndo anawafahamu hao vyura vilivo coz ndo alikuwa anawatunza pale sua mkataba wake uliivyoisha ndo kaajiriwa na hyo kampuni ya ulinzi uwezi amin mi nilishangaa manake nilikuwaga namuinaga kwenye tv tu
 
Wadau naomba anaejua habari za hawa vyura anihabarishe, nikimaanaisha ni wa nini, faida zao na ni kwa nini wamekuwa maarufu hivyo...nimesikia wanazaa but sijajua haswa kama umaarufu wao ni shauri hiyo...jana nimewaona wakishuka kutoka kwenye KLM na escort ya kutosha wakitokea Marekani..je ilikuwa ni lazima waende Marekani?.....:A S-confused1:

Hao vyura ni nOma niMesKia waNaweZa kuBeba guNia lA McHele lA kiLo hamSini mpAka sitini.
 
Back
Top Bottom