Kitombise
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 8,268
- 24,264
Habarini za weekend hii?
Tatizo langu ninaloliwasilisha hapa ni juu ya mtoto wangu kuwa mzito kuzungumza au kushindwa kunyoosha sentensi vizuri ili aeleweke kama ilivyo kwa watoto wengine.
Kwa sasa ana umri wa miaka mitatu (3), watoto wenzake hapa mtaani tunaoishi nao wao wanajua kuongea mpaka hata wale aliyowatangulia kiumri tayari wanajua kuongea kumzidi yeye. Hii hali mimi nimekuwa nikiiona ya kawaida tu, nikijua kuwa atajua kuongea kadri anavyozidi kukua.
Kilichonifanya mpaka kuja hapa kuomba msaada wenu wa ushauri au wa kitabibu ni juu ya mmama mmoja jirani yangu kuniambia mwanao ana kilimi, hivyo inamfanya ulimi kuwa mzito kuongea hali inayomfanya ashindwe kueleweka vizuri. Ameniambia nimpeleke hospital au nitafute mtu mzima mtaalamu wa mambo hayo amtibie.
Jamani naombeni ushauri juu ya hili, ili nichukuwe hatua mapema, maana nahitaji kumpeleka nursery mwezi wa 6.
Sent using Jamii Forums mobile app
USHAURI ULIOTOLEWA NA MDAU:

Wakwetu pia ana tatizo Hilo Hilo. Huwa tunampeleka hospital kwaajili ya training tofauti tofauti. Ushauri tuliopewa sisi Ni kuwa tumuandakie daily routine ya kufata icho ndio cha kwanza cha muhimu.
Usijali atakuja kutamka ayo maneno kama baba mama na kadhalika ila ukitaka aweze mapema mtafutie wataalamu ili wakufundishe jinsi ya kumsaidia mwanao. Sisi wakwetu mpaka anatimiza three years alikua hajui kujisaidia iwe ni haja kubwa au ndogo ila imesaidia sasa ivi anaenda choo mwenyewe anafanya shughulu zake mwenyewe hata home work ya shule kuna muda akijisikia anafanya mwenyewe bila usimamizi. Usikate tamaa atakaa vizuri tu.
Unajua kama mzazi ukisikia mwanao anatatizo fulani inakuwa inaumiza Sana na kufikirisha kesho yake itakuwaje?
Sent using Jamii Forums mobile app