wanafunzi wanaotoka nje wengi hawako patient oriented kwa sababu ya sera za huko. Wana shule vichwani ila kuitranslate na kitu anachokiona inakuwa ishu. Wengi hawahusiki kwenye simpo procedures sasa wakija huku wewe ndo wewe na mgonjwa ko ndo hapo wabongo tunawapiga bao kwani tulishaanza kujifunzia wagonjwa toka fourth year. Pia kuna magonjwa huku ni common huko hayapo na guidelines za treatment ni tofauti. Kama unatoka nje fanyia intern mnh ili ubadilike from sophisticated to manual zaidi. Huko kwingine utaumia sana mpaka utakapozea siyo leo. Otherwise shule ni ile ile na brain zetu ni zile zile za sengerema
Shule ya russia na tz tofauti though principles are the same. Huku tumejikita zaidi ktk infectious diseases, yani tropical medicine. Halafu tz ni mahala ambapo wanafunzi wanaruhusiwa kufanya majaribio na kutibu wagonjwa, russia wanatumia midoli tuu! Bongo teknolojia hamuna, ila kwa experience ya real time practice na kujifunza ndo penyewe.
Kuna vitu vingine huwa vinanishangaza sana! kwana Urusi ni Banana Republic - unaweza kweli ukalinganisha dunia ya kwanza na TANZANIA, wewe ujasoma Urusi haya mambo ya kusema eti wanafunzi walio somea huko hawako patient oriented una maana gani? Unataka kutueleza wana JF kwamba madaktari waliohitumu Urusi walikwenda kusomea kutibu miti na siyo binadamu!
Kwa nini unataka kuwadhalilisha madkitari wenzako (kama wewe ni daktari kweli) walio soma Urusi au Uchina eti shule zao ziko vichwani tu awana uwezo wa kutafsiri wanacho kiona! Mimi nafikili unapashwa kuwaomba msamaha kwa lugha yako hisiyo ya kistaraabu, kwani unafikili walikuwa wanajifunza kwenye dummies!
Kwa mawazo yako kwani Medicine ni nini hasa, siku kukalili majina ya kigriki na kilatini (i.e majina ya magonjwa, dalili zake na matibabu, mwili wa binadamu na organs zote and what have you) tangu lini Medicine ikawa na mahesabu na formula kama za Engineering - mambo mengi ni ya kukalili tu kama historia, mimi siwasemi vibaya madkitari, nisichotaka ni kule wabongo kudhalau wabongo wenzao walio soma nje hasa Urusi, wanayafanya haya kwa madhumuni ya kujirinda tu na ubinafsi, nataka uelewe kwamba Serikali yetu imeanza kuwapeleka wanafunzi Urusi tangu tupate Uhuru, Serikali siyo wajinga - haipendezi nyinyi kujiona zaidi na wenzenu si lolote si chochote, mambo ya kusema kuwapiga bao yanatoka wapi kwani kuna mashindano gani hapa.
Mwisho labda nikuhulize: Unaposema Tanzania(Africa) magonjwa ambayo yako common huku na hayako Ulaya kwa hiyo Mtanzania aliyesomea Urusi itamuwai vigumu kuyatibu, sasa hapo unataka kutueleza nini! Mswahili asijuwe magonjwa ya kitropiki!!! Inakuwaje Wachina, Warusi, Waingereza wanapokuja TANZANIA kama madktari kwa kujitolea au kulipwa wanakuwa na uwezo mkubwa ku-diognise na kutibu magojwa yote ya kitropiki wakati wenyewe ni Wazungu, leo hii unatwambia Mswahili aliye somea Urusi/Uchina hawezi kutibu magonjwa ambayo yako NATIVE nchini mwake! Attitude zako hizo kama unaweza kuwa RMO au Mkurugenzi pale wizara ya afya naona hawa watu waliosoma Urusi/Uchina watapata wakati mgumu sana, kasumba hii haifai hata kidogo.
Mkuu sio kwamba mtanzania aliyesomea ulaya atashindwa hapana si kweli, lakini itamchukua mda kidogo tofauti na yule pale ambaye kila siku anayaona, ni mawazo yangu tu.
Mkuu leo, ukitoka bongo na taifodi yako ukaja ulaya na ukaenda hospitali na uwaambie tu unaumwa tumbo hivi, itawachukua mda madaktari kugundua unaumwa taifodi. Lakini daktari wa bongo ukimweleza jinsi tumbo linavyouma hata hakupimi atakwambia una taifodi. Sijui unanielewa nataka kujenga hoja gani hapa?
Na ndiyo maana nchi nyingi kama umesomea nje ya nchi yao udaktari ukirudi nyumbani lazima upigwe kozi ikiendana sambamba na mtihani, sijui TZ nayo iko hivo
Mkuu nakuelewa vizuri tu, madaktari wazungu ambao wako Ulaya inawachukuwa muda kutambua magonjwa ya kitropic; lakini mbona nilikuwa naona wanawauliza wazungu ambao wanaumwa magonjwa yenye utata kidogo, kama wamewahi kutembelea Africa/Asia walipo kuwa holiday, majibu yao ndiyo huwa yanawasaidia madaktari hao ku-zero in kwenye tatizo lenyewe kama ni:Malaria,Yellow fever na kwa wale walikuwa wanatoka India/Bangladesh/Paskistani wanapimwa TB.
Tukija kwa madaktari waswahili walio somea Urusi, mimi siamini kwamba inawachukua an eternity kutambua magojwa ya kitropic ambayo yako NATIVE kwa nchi walio zaliwa, mkuu sina hakika kama wakirudi nyumbani wanapigwa kozi ikiendana na mitihani - kuna aja gani ya mitihani tena, kwa nini wasiugane na wenzao kwenye awamu ya intern.
Kitu kingine, why pick on Madaktari walio soma Urusi, mbona hawazungumzii walio soma Uingereza, Merikani, Australia nk. Mimi nalisema hili kwa kuwa niliwahi kuona daktari mstaafu aliyewahi kusomea Urusi akiojiwa kwenye TV, alisema ilimchukua muda sana kupewa cheo cha RMO! Na alipo teuliwa bado wanzake walikuwa awa amini kama kazi hiyo angeimudu - sasa hii ni kasumba gani? zama hizi tena bado kuna watu/madaktari wenye mawazo remnant ya vita vya baridi (East vs West).
Mkuu
Nakupata vyema mkuu, lakini nchi nyingi ukisoma nje unapigwa kozi na kijimtihani. Anyway
Hawaongelei waliosoma uingereza kwa nafikiri kwa sababu ni wachache mno kwa kizazi hiki, maana kusoma udaktari nchi hizo baba yako lazima awe bilionea maana sifikiri hata kama kuna scholarship na kama zipo basi ni ndogo sana sana.
Lakini nchi za ulaya mashariki na urusi bado zinatusaidia kutupa nafasi za kusoma ktk maeneno hayo, na ndio wengi waliosoma udaktari nje ya nchi wamesoma kutoka huko na ndiyo maana wanaongelewa sana, na wauingereza hawaongolewi kwa sababu ni wachache sana ama hawapo kabisa.
Lakini naweza kushawishika kukubaliana na mtoa maada kwa mazingira yake. Lakini hii halihusiani sana na masomo ya darasani bali mazingira aliyosomea.
Nitatoa ushuhuda
Mie sijawahi kusoma biology nimesoma technical toka secondary , lakini tukiwa ktk nchi fulani ulaya huwa kuna wakenya wanakuja kukimbia kwa msimu wanarudi, basi mkenya mmoja akauugua wakampeleka hospitali waganga na watalaamu na mashine zao wakijikusanya wakamfanyia uchuguzi hawapati kitu, siku mbili zimepita wanakuna kichwa jamaa yupo hoi na uhoi unazidi, rafikii yangu mwingine mkenya akanichukua twende tukamcheck jamaa, kukuta jamaa wa njano tukawaambia madaktari huyu either ni yellow fever ama malaria, walivyompima wakakuta na yellow fever.
Lakini madaktari walikuwa wamejikita sana kwenye ini, kuchunguza. Hivyo sisi tukawa tumegundua gonjwa japo sio madaktari lakini ni kutokana na mazingira tuliyokulia.
Hivyo Daktari aliyesoma Tz kwa kuona magonjwa hayo hayo kila siku ni rahisi kuyang'amua mapema wenda kuliko wa ulaya kwa sababu wa ulaya amefanya na kusoma ktk magonjwa tofauti kabisa.
Mfano, Unaweza somaulaya na kufanya kazi miaka mingi ya kutosha lakini hujawahi kukutana na mgonjwa wa malaria, sasa wakikushusha moja kwa moja pale bongo kwa mentality za kibongo utaonekana hujui.
Udaktari naufananisha kwa mbali na watu waliosoma sheria, nafikiri huwezi chomoka na sheria yako ya tz ukaenda moja kwa moja kudefend kesi tuseme us, ili ufanye hivyo itabidi wakupe mda upate kuzipitia sheria za nchi husika, vivyo hivyo kwa madaktari kama umesoma ulaya kwenye msisitizo wa magonjwa tofauti itabidi wakupe mda ili kuweza kwendana na magonjwa ya nyumbani, sasa huu mda wa mpito ndo wanaonekana hawajui,LAKINI kwa mentality za kibongo.
Mkuu
Nakupata vyema mkuu, lakini nchi nyingi ukisoma nje unapigwa kozi na kijimtihani. Anyway
Hawaongelei waliosoma uingereza kwa nafikiri kwa sababu ni wachache mno kwa kizazi hiki, maana kusoma udaktari nchi hizo baba yako lazima awe bilionea maana sifikiri hata kama kuna scholarship na kama zipo basi ni ndogo sana sana.
Lakini nchi za ulaya mashariki na urusi bado zinatusaidia kutupa nafasi za kusoma ktk maeneno hayo, na ndio wengi waliosoma udaktari nje ya nchi wamesoma kutoka huko na ndiyo maana wanaongelewa sana, na wauingereza hawaongolewi kwa sababu ni wachache sana ama hawapo kabisa.
Mkuu
Nakupata vyema mkuu, lakini nchi nyingi ukisoma nje unapigwa kozi na kijimtihani. Anyway
Hawaongelei waliosoma uingereza kwa nafikiri kwa sababu ni wachache mno kwa kizazi hiki, maana kusoma udaktari nchi hizo baba yako lazima awe bilionea maana sifikiri hata kama kuna scholarship na kama zipo basi ni ndogo sana sana.
Lakini nchi za ulaya mashariki na urusi bado zinatusaidia kutupa nafasi za kusoma ktk maeneno hayo, na ndio wengi waliosoma udaktari nje ya nchi wamesoma kutoka huko na ndiyo maana wanaongelewa sana, na wauingereza hawaongolewi kwa sababu ni wachache sana ama hawapo kabisa.