Naomba kufahamu kuhusu maneno haya "punga" na "popoma".

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,200
1,747
Je Yana maana gani?!
Je yalianzaje?!

Maana nimeyasoma jamii forums pekee lakini mtaani sikuwahi kuyasika.
 
Punga
1 kuota mfano upepo, jua au moto.
Yaani unakaa tu ili upepo ukupulizie, jua likuwakie au upate joto la moto.

2 kuaga, kupungia mkono, au kusalimia, mfano wanasiasa wanapopita kwenye umati wa watu, wakiyumbisha mkono.

Popoma
Sidhani kama ni neno la Kiswahili.
 
Je Yana maana gani?!
Je yalianzaje?!

Maana nimeyasoma jamii forums pekee lakini mtaani sikuwahi kuyasika.


Neno PUNGA:- kutoka kamusi ya karne ya 21.

1----Shuke/suke la maua yatoayo mbegu za kiume katika mimea ya jamii ya nyasi mfano mahindi.

2---Toa shetani kichwani.

3---pumzika mahali penye upepo mwanana au hewa nzuri.

4----pepea mkono, pepea kitambaa cha mkononi.

5----Pungua ukali wa joto mfano joto la jua.


Popoma halimo. Hilo ni neno la mtaani kumaanishi mtu asiyefikiri au mtu mwenye upeo mdogo wa kufikiri, kilaza, kaputi nk,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom