Naomba kufahamu kama Katiba ya JMT inaruhusu Mtu kumkashifu Mungu na kuachwa tu?

blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
10,434
12,589
Wadau thread title iko wazi kabisa.

Ni kuhusu huu wimbo mpya wa Ney Wa Mitego. Hivi Mungu yupo.

Ametukana watu kule kwamba ni wapumbavu. Yeye anadai tumuache.

Sisi tunaoamini Mungu ni wapumbavu. Sasa hivi Katiba inasemaje juu ya hili. Au ndo vile Serikali haina dini so kila mmoja anaweza ropoka tu.

Hili limekaaje. Je, BASATA wameona ni sahihi kabisa Mungu kukashifiwa?

Yule msanii anakula bangi!?

Karibuni kwa maoni.
 
Inategemea ni katika Utawala Upi, nimesema utawala sio uongozi
 
Jesusfreak08, Kwa hiyo huyo anayemtukana Mungu aachwe tu kwa sababu Mungu hapiganiwi? Dini gani ambayo Mungu akutukanwa hawawezi kumpigania? Mtu akere wanaomwamini Mungu halafu aachwe? Kweli?
 
Bado sijasikia wimbo. Kama ni kweli, Mungu atamshughulikia soon!
Kutukana na kukashifu hadharani iyo ni dalili ya ukosefu wa maadili.
 
Anamuambia Mwenye Enzi " Au ushakula kona shaetani ametake over"..

Dah.. SMH!!!!
 
Wadau thread title iko wazi kabisa.

Ni kuhusu huu wimbo mpya wa Ney Wa Mitego. Hivi Mungu yupo.

Ametukana watu kule kwamba ni wapumbavu. Yeye anadai tumuache.

Sisi tunaoamini Mungu ni wapumbavu. Sasa hivi Katiba inasemaje juu ya hili. Au ndo vile serikali haina dini so kila mmoja anaweza ropoka tu.

Hili limekaaje. Je BASATA wameona ni sahihi kabisa!?? Mungu kukashifiwa. !?

Yule msanii anakula bangi!?
Karibuni kwa maoni.
Serikali haina dini, elewa hilo. Ikiwa hivyo watu wataanza kujitetea mahakamani kwamba walirogwa na wachawi au walitumwa na Mungu kufanya jambo fulani
 
hii nchi siyo ya kidini kila mtu anamuua anachotaka kama we unaamini mungu bas endelea hivohivo na msimamo wako kama yeye haamin bas mwache n msimamo wake mind your own goddam business and everything will be cool.....miafrika hatuendelei sabb tunafatiliana acha kufatilia mambo ya watu.....ndo mana mizungu iko mbali....
 
Serikali haina dini, elewa hilo. Ikiwa hivyo watu wataanza kujitetea mahakamani kwamba walirogwa na wachawi au walitumwa na Mungu kufanya jambo fulani
Hii ishu ni pana mkuu.

Serikali haina dini ila waliokojolea misahafu walikamatwa. Walioimba maneno ya kikristo katika nyimbo za bongo fleva nyimbo zao zilifungiwa.

Nahisi hapa kanuni ni moja.

'Sikiliza muziki kwa sauti kubwa utakavyo ila hakikisha mimi sisikii' na hapo tupo chumba kimoja.

Yaani ni kusema, serikali haina dini ila hatutarajii atokee mtu akashifu dini ya mwingine.
 
Serikali haina dini, elewa hilo. Ikiwa hivyo watu wataanza kujitetea mahakamani kwamba walirogwa na wachawi au walitumwa na Mungu kufanya jambo fulani
Aisee.. Serikali hii ambayo tuliongozwa na Rais maombi ya siku tatu dhidi ya Covid 19!!?
 
Hii ishu ni pana mkuu.

Serikali haina dini ila waliokojolea misahafu walikamatwa. Walioimba maneno ya kikristo katika nyimbo za bongo fleva nyimbo zao zilifungiwa.

Nahisi hapa kanuni ni moja.

'Sikiliza muziki kwa sauti kubwa utakavyo ila hakikisha mimi sisikii' na hapo tupo chumba kimoja.

Yaani ni kusema, serikali haina dini ila hatutarajii atokee mtu akashifu dini ya mwingine.
Waliokojolea misaafu hawakukamatwa kwa kosa la kukojolea misaafu, walikamatwa kwa usalama wao wenyewe dhidi ya wahalifu wafia dini ambao wanaweza wakajichukulia sheria mikononi na kukuadhibu kwa kanuni zao binafsi, umeelewa?
 
Serikali haina dini, elewa hilo. Ikiwa hivyo watu wataanza kujitetea mahakamani kwamba walirogwa na wachawi au walitumwa na Mungu kufanya jambo fulani
IlA kila kiongozi huapa kwa jina la Mungu tena Akiwa ameshika kitabu kitakatifu sawa na imani yake! ????!
 
Mungu hujipigania haihitaji msaada wako katikakuonyesha ukuu wake. Kama amekosea atamshungulikia kwa njia zake. Tatizo ni pale watu tunapotaka kumpigania Mungu kama vile yeye hana uwezo.
Kama baali Ni Mungu na ajitetee.
 
Back
Top Bottom